Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,507
- 5,545
Leo WB imeitangaza Tanzania kuwa katika kiwango cha nchi ya Pato la kati,(MIC) Midle income Country.Kwa wengi hii ni habari njema sana na inaweza kuakisi uhalisia au isiakisi uhalisia.
Kwa mujibu wa WB,nchi ya pato la kati ni nchi yenye pato la kati ya USD 1006 na kuendelea kwa mwaka kwa kila raia wake.Hili ni pato la wastani la taifa.Kwa tafsiri ndogo ni kwamba pato la taifa limeongezeka na pato la wananchi pia limeongezeka,kwa wastani.
Pamoja na uzur wa habari hii kuna eneo ambalo linapaswa kutazama ili kuona kwa hakika kama jambo hili ni la kufurahia nalo ni swala la midian income pamoja Deviation ya National income (Distribution ya National Income). Katika kupima hili lazima tujiulize pato la chini kabisa nni kiasi gani na pato la juu kabisa ni kiasi gani kwa kuzingatia standardsza kitaifa kutoka katika takwamu za mishahara,na walipa kodi.
Ni lazimi pia tuwe na takwimu sahihi zinazohusiana na hali za maisha ya watanzania kwa kuzingatia vigezo tulivojiwekea wenyewe.Mfano rahisi ni kwa kuangalia Je kima cha chini cha mshahara ni kiasi gani na idadi ya watu walioko katika kiwango hiki cha malipo ni wangapi?Je idadi ya nguvu kazi ni kiasi gani na idadi ya wategemezi ni kiasi gani?Je idadi ya watu walioko katika sekta isio rasmi ni wangapi na pato lao la wastani kiasi gani?
Kuna maswali mengi yanapaswa kujibiwa kabla ya kushangiliwa kwa hatua hii tuliofikia.
Tunapaswa kujiuliza juu ya wastani wa malipo ya kodi per Capita, Mfano kama Pato letu la kodi ni Trilioni 20 kwa mwaka je mchango wa kodi per capita ni kiasi gani?Je ni kwa kiwango gani watu wanapata huduma bora za afya, elimu, maji n.k.?Je kwa idadi ya watu iliopo je tunayo miundo mbinu ya afya, elimu etc inayoweza kuwahudumia watu hawa vizuri? Vipi kuhusu idadi ya ajira mpya na idadi ya watafuta ajira wapya je zinalandana? Je ni sekta gani inachangia zaidi katika pato la taifa? Je ndio sekta hio hio inayozalisha ajira nyingi? Je uchumi wetu unategeme pato la kuotoka nje au ndania?Ni bidhaa na huduma gani ambazo zinachangia zaidi katika eneo hilo?
Ni vizuri tukatafakari kwa kina juu ya tangazo hili na kutumia fursa katika kuongeza usawa katika kipato,sio kwa kuwanyang'anya wenye nacho bali kuwajengea uwezo wasiokuwa nacho. Lazima tutambua sekta kipaumbele katika ajira na uzalishaji na kama taifa tuwe kipaumbele hasa katika ujenzi wa jamii yenye usawa.
Lazima tutambue maeneo ambayo ni korofi katika kuleta usawa na kisha tukuchukue hatua kwa pamoja kama taifa katika kuyashughulikia hasa maeneo ya uchumi, demokrasia, uwazi, haki za binadamu, uhuru na usawa.
Tujadili kwa pamoja maana ya tangazo hili la benki ya dunia na nmna ambavyo tunaweza piga hatua katika kusonga mbele kama taifa.