Nini maana ya Tanzania kutangazwa kuwa Nchi ya Uchumi wa Kati (MIC) na Benki ya Dunia?

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,470
5,471
Leo WB imeitangaza Tanzania kuwa katika kiwango cha nchi ya Pato la kati,(MIC) Midle income Country.Kwa wengi hii ni habari njema sana na inaweza kuakisi uhalisia au isiakisi uhalisia.

Kwa mujibu wa WB,nchi ya pato la kati ni nchi yenye pato la kati ya USD 1006 na kuendelea kwa mwaka kwa kila raia wake.Hili ni pato la wastani la taifa.Kwa tafsiri ndogo ni kwamba pato la taifa limeongezeka na pato la wananchi pia limeongezeka,kwa wastani.

Pamoja na uzur wa habari hii kuna eneo ambalo linapaswa kutazama ili kuona kwa hakika kama jambo hili ni la kufurahia nalo ni swala la midian income pamoja Deviation ya National income (Distribution ya National Income). Katika kupima hili lazima tujiulize pato la chini kabisa nni kiasi gani na pato la juu kabisa ni kiasi gani kwa kuzingatia standardsza kitaifa kutoka katika takwamu za mishahara,na walipa kodi.

Ni lazimi pia tuwe na takwimu sahihi zinazohusiana na hali za maisha ya watanzania kwa kuzingatia vigezo tulivojiwekea wenyewe.Mfano rahisi ni kwa kuangalia Je kima cha chini cha mshahara ni kiasi gani na idadi ya watu walioko katika kiwango hiki cha malipo ni wangapi?Je idadi ya nguvu kazi ni kiasi gani na idadi ya wategemezi ni kiasi gani?Je idadi ya watu walioko katika sekta isio rasmi ni wangapi na pato lao la wastani kiasi gani?

Kuna maswali mengi yanapaswa kujibiwa kabla ya kushangiliwa kwa hatua hii tuliofikia.

Tunapaswa kujiuliza juu ya wastani wa malipo ya kodi per Capita, Mfano kama Pato letu la kodi ni Trilioni 20 kwa mwaka je mchango wa kodi per capita ni kiasi gani?Je ni kwa kiwango gani watu wanapata huduma bora za afya, elimu, maji n.k.?Je kwa idadi ya watu iliopo je tunayo miundo mbinu ya afya, elimu etc inayoweza kuwahudumia watu hawa vizuri? Vipi kuhusu idadi ya ajira mpya na idadi ya watafuta ajira wapya je zinalandana? Je ni sekta gani inachangia zaidi katika pato la taifa? Je ndio sekta hio hio inayozalisha ajira nyingi? Je uchumi wetu unategeme pato la kuotoka nje au ndania?Ni bidhaa na huduma gani ambazo zinachangia zaidi katika eneo hilo?

Ni vizuri tukatafakari kwa kina juu ya tangazo hili na kutumia fursa katika kuongeza usawa katika kipato,sio kwa kuwanyang'anya wenye nacho bali kuwajengea uwezo wasiokuwa nacho. Lazima tutambua sekta kipaumbele katika ajira na uzalishaji na kama taifa tuwe kipaumbele hasa katika ujenzi wa jamii yenye usawa.

Lazima tutambue maeneo ambayo ni korofi katika kuleta usawa na kisha tukuchukue hatua kwa pamoja kama taifa katika kuyashughulikia hasa maeneo ya uchumi, demokrasia, uwazi, haki za binadamu, uhuru na usawa.

Tujadili kwa pamoja maana ya tangazo hili la benki ya dunia na nmna ambavyo tunaweza piga hatua katika kusonga mbele kama taifa.
 
uchumi umekuwa ila mifukoni mwa watu ni vumbi la kongo na mikeka ya M-bet iliyojaa mamilioni.
 
Duniani kwenye level za kiuchumi zimegawanyika katika makundi matatu
1. Nchi Tajiri au developed countries
2. Nchi za kipato cha kati au middle income countries
3. Nchi maskini zinajulikana pia kama nchi zinazoendelea au developing countries

Nchi zinazoendelea zimegawanyika mara tatu
1. Kuna nchi maskini
2. Nchi maskini wastani
3. Nchi maskini sana

Pia kwenye group la nchi za kipato cha kati nako Kuna makundi kama ifuatavyo:
1. Kuna nchi uchumi wa kati katika level ya chini (*Tupo tupo sasa Tanzania*)
2. Uchumi wa kati wastani
3. Na uchumi wa kati level ya juu (Hizi ni zile ambazo zinakaribia kuwa nchi Tajiri)

Pia kwenye hizi nchi Tajiri nazo zimegawanyika kutokana na nguvu za kifedha, viwanda na ukubwa wa majeshi hasa kutumia silaha kama za Nyuklia. Hapa Kuna magroup kama vile
1. G8
2. G5
3. OECD countries
4. Kwa sasa hivi pia Kuna BRICS (Brazil, India, China na South Africa).

In Magufuli We Trust
T2020JPM

Vitalis Konga(Mwana Vasamwenda)
Njombe Mjini

FB_IMG_1593660668771.jpg
 
Kuwaacha watu wanapotosha, vyombo vya habari vinageuka vuvuzela na wanasiasa wana tumia tangazo la World Bank kupongeza na wengine kuponda sio jambo jema kwa taifa.

Kwa nini serikali inashindwa kutoa ufafanulizi wa maana halisi ya nchi kuwa katika LOWER-MIDDLE INCOME ECONOMY (ambalo ni kundi TZ tupo) na MIDDLE INCOME ECONOMY (lengo la TZ kufikia 2025)?

Sasa kila mtu anasimama kusifia kuwa lengo limefikiwa wakati sio kweli. Magazeti nayo yameingia kwenye kundi la kupotosha habari hiyo, jee ni kwa manufaa ya nani?

Tunaposema uongo wakati balozi za nchi wahisani zipo zinauona uongo, mashirika ya kimataifa yatoayo misaada na mikopo yanatuangalia tunajiweka kundi gani?

Masuala ya uchumi tuyachukulie kitaifa na sio kivyama tutakwama.

IMG_20200702_063530.jpg
 
Kuwaacha watu wanapotosha, Vyombo vya habari vinageuka vuvuzela na wanasiasa wana tumia tangazo LA World bank kupongeza na wengine kuponda sio jambo jema kwa taifa.

Kuna tofauti kubwa sana. Lengo nikufikia middle income. So far ndio tuko kwenye middle-lower. Gap bado ni kubwa lakini bado naipa serikal pongezi kwa hatua ilitotufikisha
 
Kuwaacha watu wanapotosha, Vyombo vya habari vinageuka vuvuzela na wanasiasa wana tumia tangazo LA World bank kupongeza na wengine kuponda sio jambo jema kwa taifa.
Kwa nini serikali inashindwa kutoa ufafanulizi wa maana halisi ya nchi kuwa katika LOWER-MIDDLE INCOME ECONOMY (ambalo ni kundi TZ tupo) na MIDDLE INCOME ECONOMY (lengo la TZ kufikia 2025)?
Sasa kila mtu anasimama kusifia kuwa lengo limefikiwa wakati sio kweli. Magazeti nayo yameingia kwenye kundi la kupotosha habari hiyo, jee ni kwa manufaa ya nani?
Tunaposema uongo wakati balozi za nchi wahisani zipo zinauona uongo, mashirika ya kimataifa yatoayo misaada na mikopo yanatuangalia tunajiweka kundi gani?
Masuala ya uchumi tuyachukulie kitaifa na sio kivyama tutakwama.
Kwa nini usitolee ufafanuzi wewe kama unafahamu?
 
Hivi lower middle income si ni subset ya middle income.Ndani ya middle income kuna makundi ambayo ni lower na upper.

Sasa mnasemaje Tz haijafika middle income. Halafu hakuna nchi iliyopewa title ya middle income pekee hapo.Middle income zote wameziita either lower middle income au upper middle income.

Nyie ndo mnataka kupotosha watu! Tz ni nchi ya kipato cha kati.
 
Unaonekana unatamani watu wajue kuhusu utofauti wa vitu hivyo viwili, ili upotoshaji usiendelee kuwepo.

Ni vyema sasa kama wewe mdau ungeanza kutolea ufafanuzi ili wachache waliopo humu tuanze kuelewa alafu na sisi tukawaeleweshe wenzetu huko mtaani.
 
Back
Top Bottom