Nini maana ya neno Uhuru?

complex31

JF-Expert Member
Jun 15, 2016
379
1,208
Kwa miaka mingi tumekua tukisheherekea uhuru bila ya kujua ya kwamba hatuna uhuru asilimia mia moja kutoka kwa Nchi zenye utajiri na uchumi mkubwa duniani.

Nianze na Marekani
Marekani ilipata uhuru mwaka 1776 kutoka kwa Uingereza na rais wao wa kwanza aliitwa Washington ili kuridhisha kuwa wako huru kutoka kwa mkoloni wao waliweza kubuni na kuja na vitu vyao vipya ili waweze kujiita Marekani.

Walibadilisha Lugha, majina kama Lift wanaita Elevator, Petrol wanaita Gas, siting room wanaita living room, police wanawaita Cop na mengine mengi.

Walibadilisha majina ya vipimo vya sayansi kama kilogram wanaita Pound, kilometer wanaita Mile.

Uingereza kwa upande wa barabara magari yanapita kushoto (keep left) marekani ni kinyume chake magari wanaendesha upande wa kulia (keep right).

Kwenye maswala ya consumption vitu kama ice cream wanauza kwa ukubwa sio moja kama kama Uingereza hivo hivo mafuta ya gari wanapima kwa gallons ndio maana kwa upande wa consumption ya vitu marekani inaongoza kwa matumizi makubwa.

Tuje kwetu Tanzania toka tumepata uhuru mwaka 1961 asilimia kubwa bado tunatumia formular za kikoloni pia hatuna mpango wa kutafta vitu vyetu wenyewe kama walivofanya mataifa kama America, China na mengine.

Mfano majengo ya serikali yanatumika yale ya mkoloni (ikulu ya Dar) majengo ya shule kama Kibaha, Pugu
Mavazi tunayovaa tunaiga kutoka Ulaya, muziki na mengine.

Mitaala ya shule pia tunatumia ambayo haina ticha na haibadiliki kulingana na wakati mpaka leo hii mwanafunzi wa kidato cha pili anafundishwa Litmus paper au Luminous na Non-luminous flame.

Kuna haji kupitia wizara husika kuanzishwe mpango mkakati wa jinsi ya kua na vitu vyetu .
 
Africa hatuna Uhuru wa kiuchumi kutokana na kutokuwa na Sera nzuri kwenye maswala ya ubunifu wa viwanda hata ordinary industries. Sasa nchi kama China sasa hizi wako kwenye Technology industrial. Sisi bado hata penseli za shule tunaaguza. Kwaio bado hatuwezi kuwa huru for 100%
 
Uhuru : ni kufanya ama kusema ulitakalo bila kushututishwa na bila kukera wengine.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwelo uhuru ni mtu lusema chochote hata bila ya kufanyia research unachokisema. Nimeona hapo jamaa anasema eti Wamarekani wanatumia miles na pound kama vipimo vya umbali na uzito wakibadilisha kutoka kwa Waingereza🤣🤣🤣
 
Mambo ya research hayahusiani na uhuru.

Muhimu uhuru wako usiingilie uhuru wa wengine.
Kwelo uhuru ni mtu lusema chochote hata bila ya kufanyia research unachokisema. Nimeona hapo jamaa anasema eti Wamarekani wanatumia miles na pound kama vipimo vya umbali na uzito wakibadilisha kutoka kwa Waingereza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom