Nini maana ya neno UCHOCHEZI?

Ndugu wana jukwaa,

Napata shida sana kuelewa maana ya hili neno.

Nawasilisha hoja.
 
Fafanua zaidi manake mi najua kuna uchochezi wa kuni ili moto uwake vizuriii hasahasa sisi wa vijijini kama unapika mboga korofi let's say kisamvu cha maziwa au maharage makavu
 
Mkuu kama umeshawahi kupikia kuni, huwezi ukauliza hilo swali...
 
usione hakuna majibu.
kwani kujibu tu maana ya uchochezi na kwenyewe ni uchochezi.
 
Kwa waliofatilia press ya halima naombeni mniorodheshee maneno yanayosemwa kuwa ni ya uchochezi ili tujue ukweli . walianza kina lema , juzi Lowasa Leo halima na wengine wengi wa cyber crime tueleweshane jamani ili tupate elimu tusije kujikuta na sisi tunaongea mambo tukijua tuko sahihi kumbe tunafanya uchochezi halafu tujikute sero bureeeeee
 
Uchochezi ni kumpinga,kumkosoa magufuli na serikali yake
 
Kila zama na mambo yake Wahenga waliwahi kunena zamani. Zama hizi, pamoja na mambo mengine kimeamua kitumie neno Uchochezi ili kuthibiti sijui wahalifu. Na neno hili linakuzwa kulingana na matumizi yake kwa vitendo kukua. Nina Maswali kadhaa kwa wale ambao wanaamini katika Uchochezi zaidi.

1. Nini maana ya Uchochezi?

2. Ili uwe Mchochezi unatakiwa uwe umefanya kitu gani?

3. Kuna kitu gani kinachotumika kusema huu ni Uchochezi chenye kushika, kuonekana na hata kupimika?.

4. Kuna tofauti gani kati ya mambo haya kisheria? 1. Uchochezi, 2. Maoni na 3. lugha ya kuudhi?

5. Tano, wakili wa Tundu Lissu alisema ili uonekane wewe ni mchochezi inatakiwa ionekane umemchochea nani? Na alikuwa sehemu gani?. Je, kuna kipimo gani cha kuonekana kuwa mtu huyo umemchochea wewe?

6. Baada ya Uchochezi yule aliyechochewa alifanya jambo gani?

7. Nani mwenye mamlaka ya kusema huyu ni Mchochezi?. Dola kwa ujumla au na Wananchi pia.

8. Kisheria ikithibitika kuwa wewew ni mchochezi unaweza kufungwa hadi miaka mingapi?.

Nazidi kujifunza kama ninavyojifunza mwenye mamlaka ya kusema huyu ni gaidi na yule siyo gaidi?. Japo hapa kuna vipimo angalau japo mtu katika Taifa lingine akifanya anaweza kuitwa jina lingine.

Kati ya NDOTO niliyokuwa nayo nikiwa mdogo ni kusoma sheria lakini mazingira na hali ikawa tofauti.....

Nawakilisha
 
VIPIMO VYA UCHOCHEZI VINAPATIKANA KWENYE MIKOJO:New discovery in TZ!
 
Uchochezi, kihasi (negatively) ni uhamasishaji jamii katika kutotii / kuasi mamlaka iliyoko madarakani kutokana na kile ambacho unaamini kwamba yanakiuka maadili, haki, maslahi ya jamii, au kukwaza matarajio ya jamii (kuchonganisha jamii na mamlaka) na kichanya (positevely) ni kuhamasisha jamii kutotenda yale yenye kuwakwaza katika kujiletea mabadiliko / maendeleo ya maisha.
Ili kufanya hivyo, kihasi (negatively), lazima utumie lugha ya kukebehi, chuki, kushusha hadhi, ubabe (liwalo na liwe), matusi, nk. nk. dhidi ya unaowatuhumu na kichanya (positevely), lazima uonesha manufaa ya kutenda hayo kwa lugha ya upendo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…