Wala tusiwe na shaka haya ni mapambano ya kifikra....fikra dhalimu dhidi ya fikra sahihi za ukombozi na kujitambua!!..
Hebu tufikiri kidogo. Msigwa kama msemaji mkuu wa kambi ya upinzani wizara ya maliasili alisema sana kuhusu ujangili wa tembo wetu na kumhusisha moja kwa moja katibu mkuu wa CCM Ndg Kinana.Kama kawaida wabunge wa CCM waling'aka wakamwita ni mchochezi, anamtuhumu mtu ambaye hayupo bungeni na hivyo hawezi kujitetea!!
Je, haya nayo ya Sugu serikali haiwezi kujitetea? Si ipo bungeni kwa nini isijitetee? Je, si ni bora wakatunga kanuni ya kusema jambo/mambo ambayo wanataka kusikia tu? Na, je tutaweza kuyafanya masikio yetu na macho kuwa selective kwamba tuone na tusikie tunayotaka tu?......tuchague kuwa vipofu au viziwi basi!...hii ndiyo option pekee salama kwao.....Otherwise tuache fikra zigongane na kukwaruzana ili kupata mwafaka na hiki ndicho chanzo cha maendeleo yeyote ya kweli!!!!
Hapa wanajamii hakuna cha uchochezi wala nini, ni uwoga wa watawala wetu tu, ni uwoga wa CCM na serikali yake tu na kwa kweli wanamfanya huyu mama Spika Makinda, mwana CCM mwenzao akiongoze chombo hicho katika mazingira mugumu sana bila sababu na wao bila kujua wanamfanya huyu mama sometimes aonekane kama zezeta....
Ni bora wakaacha bunge kikawa chombo huru cha mawazo ya wabunge.....wasiharibu Bunge letu kwa kuwafanya wabunge wetu wawe wanasema yanayowafurahisha watawala tu