Nini maana ya ndoto hii

baby success

JF-Expert Member
Jul 14, 2022
549
1,791
Habari za jioni wakuu

Nahitaji msaada kujua maana ya NDOTO HII

Ni hivi mwezi uliopita nikaota ndugu yangu yaani kaka yangu anaumwa sana basi siku hiyo ikapita siku ya pili yake nikapigiwa simu nikaambiwa anaumwa kweli siku iliyo fuata nikaota niko mkoan ambako huyo kaka yangu anaishi nikamkuta kaka yangu kakonda harafu kaka kamuegemea kaka yangu mwingine yaani kiujumla alikuwa hawezi kukaa mwenyewe tu bila kumwegemea mtu sasa nikawa namwangalia yule mgonjwa usoni nikagundua sio yeye ILA wanafanana tu yaani nikwamba mimi nikawa namuona mtu anayefanana na kaka yangu ndio kakaa pale harafu kaka yangu mwenyewe hayupo ILA wengine wote waliokuwepo pale hawakua wamegundua chochote kuhusu hilo bac me nikawa nawaambia huyu sio ndugu YETU ndugu YETU hapa hayupo wakawa wametuka bac NDOTO ikaishia hapo

Baada ya week huyo mgonjwa akafariki bac nikapigiwa simu na kufunga safar ya huko mkoani japo nilikuta wemesha zika yaani wakati nafika walikua wamezika kama jana yake bac nikafika MCHANA ucku ulivyo fika me nikasema nilale jikoni sababu huko mkoani kuko na baridi mno bac tukalala watu kama 6 ilivyo fika mida kama ya Saa Nane au tisa ucku hivi nikahisi baridi sana nikaamka na kukaa kalibu na sehem palipokua na moto na kuzivuruga zile chenga za moto ILI niote moto ILA natulia vzr nikasikia mshindo nje tii! tii! Tii!

Yaana kama mtu mwenye uzito mkubwa anakimbia nje ya mlango nikakaa kama robo Saa hivi BADO mshindo ukawa UNAENDELEA nikarudi kulala KWA woga huku mapigo ya moyo yakinienda mbio nikawa nawaza ni nini hicho hata sipati JIBU na sikumuamsha mtu baadae nikapitiwa na usingizi nikastuka Saa kumi na moja nikakuta kuko kimya.

Kulivyokucha nikamfata kaka yangu mmoja na kumuuliza nini kilikua kinaendelea nje ucku akajibu hajui KILA mtu nilimuuliza akasema hajui.

Yaana mpaka leo nikifikiria sipati JIBU na juzi tu nimemuota kaja nyumban harafu akawa anatufokea familia harafu kuna kitu akawa anakiongea sema nimekisahau me nikawa nakemea nikawa namtaja yesu akasema wee usitaje jina hilo hata sisi tunaliogopa bac akapunguza ukali akatulia me nikaanza kumwambia wewe kaka yangu hukuaga hivyo unakumbuka?akakaa kimya tu na kuinamishwa kuachwa chini na akageuka na kuondoka bila kunijibu chochote ingawa alivyo kua hai alinipenda sana mimi kuliko mtu yeyote pale nyumban lakin akaondoka tu bila kugeuka nyuma
Wenye ujuzi kujeni.

Na kuhusu mwandiko nisameheni bure.
 
Mh! Kama Ni kweli basi roho ya kinabii inakunyemelea!
Ukiwa na uwezo wa kuona visivyoobekana,tusio na uwezo huo tutakuona umechizika.
 
Sio lazima niwe sahihi lakini huenda ni imani ile ya kiafrika cc msukule
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom