Nini maana ya mzazi?

Kungwi Mtoto

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2018
Posts
796
Reaction score
780
Naomba kujua kati ya hili neno anayetakiwa kuitwaa.. (mzazi).. je ni baba mzazi au mama mzazi na kwa nini???

,kwa fikra zangu naona baba hawezi kuwa mzazi ila ni mama tu kwani baba hawezi kuzaa balo anapanda mbegu ambazo anayezizaa ni mama na si baba..
 
Anayetangulia kuzaa ni baba...
Mama anajifungua tu na ndo maana mtoto anatumia jina la baba - sio la mama
Mama anajifungua, baba anazaa.
Hivyo mzazi ni baba.
 
Baba na mama wote ni wazazi. Yaani namaanisha mama hawezi kuitwa mzazi pasipo na baba kuhusika, na vivo hivyo baba hawezi kuitwa mzazi pasipo makatiko ya mama.
Mama tunamuita mlezi kutokana na nafasi yake kwa mtoto in the particular time, ingawa baba ama mtu mwingine yeyote anaweza akachukua nafasi ya mlezi ikiwa atakubali ama atakua radhi kuwajibika kama mlezi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na mimi naongezea swali;
Wale wenye watoto waliozaliwa na wanawake wengine kwa kupandikiziwa mbegu 'surrogates', mwanamke yupi hapa ni mzazi kati ya mtoa yai na mbeba mtoto tumboni?
 
Wote ni wazazi.... sababu kila mmoja anamtegemea mwenzie.

Sent from Jamii Forums using siemens kidole juu.
 
Makatikoo!!!
 
Na mimi naongezea swali;
Wale wenye watoto waliozaliwa na wanawake wengine kwa kupandikiziwa mbegu 'surrogates', mwanamke yupi hapa ni mzazi kati ya mtoa yai na mbeba mtoto tumboni?
Duh hilo nenoo.. ila yule c alikamuliwa mbegu but huyu mke alizaa... kuzaa ni kukamua au kuingia labour?
 
Na mimi naongezea swali;
Wale wenye watoto waliozaliwa na wanawake wengine kwa kupandikiziwa mbegu 'surrogates', mwanamke yupi hapa ni mzazi kati ya mtoa yai na mbeba mtoto tumboni?
Mama anaepandikizwa yai ambalo limesharutubishwa huyu kibaiolijia sio mzazi,,, yaani ni kama flash disk yenye nyimbo umechomeka kwenye bufa ili usikie kilicho ndani ya flash yako
 
Noted
 
nenda kamwambie baba yako huu upuuzi wako uone kama utalala hapo
 
Unazungumzia kuzaa au mzazi? Haya ni maneno mwawili tofauti na maana zake pia.
 
Mama anaepandikizwa yai ambalo limesharutubishwa huyu kibaiolijia sio mzazi,,, yaani ni kama flash disk yenye nyimbo umechomeka kwenye bufa ili usikie kilicho ndani ya flash yako
Wazungu ndio wametuambia hivyo ila siungi mkono hii.
 
kamuulize faiza ally ila yule dada angezaa na mondi pangenoga sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…