Nini maana ya kuweka "handle" kwenye Twitter?

Mabobish

JF-Expert Member
Jul 25, 2018
366
280
Habari za jioni, Wadau naomba kueleweshwa maana ya " kuweka handle" kwenye Twitter. Neno nimelikuta mara nyingi kwenye tweeter , utasikia jamaa anahamasisha kwa kusema " weka handle nikufollow.

Binafsi kidogo msamiati huu siulewewi na napenda kufanya hichokinachokuwa kinahamasishwa yaani kuweka handle. Naomba mwenye kuelewa juu ya mada tajwa hapo juu anisaidie nipate uelewa wa jambo hili, "Aulizae ataka kujua" msiporomoshe mitusi na kejeli
 
Handle ni Kishikio/Kifungo au tunaweza kusema kikoa. Kishikio/Kifungo hutumika kuambatanisha akaunti ya mhusika. Mfano, wa Kishikio ni @ na ikiwa @isergio tayari ni kifungo ambacho ndio hufahamika vyema kama handle.

Unapoombwa handle basi utaambatanisha kifungo @mabobishs hapa kitaweza kutengneza idhini ya uingiliwaji katika akaunti yako na kutazamwa au kufuatwa.
 
Back
Top Bottom