WINGER_TEREZA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 242
- 450
Habari wanajukwaa. Naomba nijielekeze moja kwa moja kwenye mada, Kuna baadhi ya Wabunge wakiwa wanachangia mijadala kadhaa pale bungeni (hasa katika bunge hili la bajeti) Mbunge anaweza kuwa ameuliza swali fulani na kutaka majibu toka serikalini na Waziri anaweza kujibu hilo swali ila Mbunge anaweza kuwa hajaridhika na majibu hayo na utamsikia akisema "nashikilia shilingi toka kwenye mshahara wa Waziri" au baada ya kuuliza swali anaweza kuongezea kabisa kwa kusema "kama sitoridhika na majibu ya swali hili toka kwa Waziri nakusudia kushikilia shilingi toka kwenye mshahara wa Waziri".
Pia katika siku za hizi karibuni nilimsikia Spika wa Bunge, Mh Job Ndugai, alisema kuwa endapo Waziri wa fedha, Dr Mwigulu, asipotoa maelezo sahihi kwanini pesa zinazo tolewa na nchi wahisani katika kupambana na changamoto za mazingira why hazitumiki na kupelekea wakati mwingine kukaa mda mrefu hazina na hatimaye kurudishwa zilikotoka ili hali kuna uhitaji wa hizo pesa kwa sababu ya vikaa zisivyo isha huko Wizarani.
Katika hilo Spika alisema atashikilia shilingi yeye mwenyewe toka kwenye mshahara wa Waziri endapo Waziri asipokuja kutoa maelezo yakina kwanini pesa hizo za "bure" zinarudigi zilikotoka. Hapa nilipo nasubiri siku ya kuwasilishwa kwa bajeti ya Wizara ya fedha na Mipango au bajeti kuu ya serikali kama Dr Mwigulu atadadavua kwa kina suala hilo kama alivyo ahidi au atakubali shilingi yake ishikiliwe na Spika (japo ambalo sidhani kama atakubali litokee kwani mbunge tu wa kawaida akitishia kushikilia shilingi Waziri, Waziri uhaa na kutoka majibu ya kumlidhisha huyo mbunge ASAP)
Swali langu: Ni nini maana ya kushikilia shilingi toka kwenye mshahara wa Waziri? Na yapi ni madhara ya yake?
Asante.