Bowie
JF-Expert Member
- Sep 17, 2016
- 4,373
- 6,084
Kwa muda wa miaka mingi huwa kuna biashara ya Mahindi hufanyika mpakani mwa Tanzania na Kenya Sirari, kuna wakati mahindi yanatoka Tanzania kwenda Kenya na wakati mwingine yanatoka Kenya kuingia Tanzania, halmashauri ya wilaya ya Tarime huingiza pesa nyingi kutokana na ushuru wa mahindi hayo.
Hivi karibuni biashara ilishamiri sana kwa mahindi hayo yaliyokuwa yanaingizwa kutoka Kenya kuja Tanzania lakini kwa muda wa wiki mkuu wa kituo cha forodha cha Sirari amepiga Marufuku kwa mahindi hayo kuingia Tanzania na hiyo imeletaa athari kubwa kwa wafanyabiashara wadogo waliokuwa wakifanya biashara hiyo.
Ningeomba Waziri husika aangalie suala hilo kwani kuna maamuzi yanayochukuliwa na baadhi ya viongozi wa serikali bila kuona inaleta kero na athari gani kwa wananchi.