Nini maana ya 'hons' degree?

Nini maana ya 'hons' degree?

veteran

Member
Joined
Apr 6, 2015
Posts
13
Reaction score
7
Habar wana jukwaa,

Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikijiuliza maswali bila ya kufanikiwa kupata majibu Na majawabu,

Nimekuwa muumini mzuri wa kupitia CV mbalimbali za wanazuoni,viongozi,Na wanataaluma wa fani mbalimbali wa ndani ya nchi.nimekutana Na neno hons haswa ktk ngazi ya bachelor degree au masters degree.

Naomba nifahamishwe

1. Nini maana ya hons degree
2. Ni vipi vigezo vya mtu kupewa hons degree
3. Na je ni kila chuo kinatoa hons degree?

Shukrani Na naomba kuwasilisha....
 
Hons degree zipo nchi za Ulaya au South Africa.

Kwa bahati mimi nilisoma South Africa, University of Free State. Kwa kawaida degree ya kwanza ni miaka 3 inaitwa first degree NA SIO 'hons' kama inavyoitwa huku kwetu. Baada ya hapo mwanafunzi anasoma mwaka mmoja ili apate hons. Yaani anaandaliwa kufanya masters degree. Kwa kwetu ni usanii.

KWA MAANA HIYO KWA SOUTH AFRICA AU U.K MWANAFUNZI ANARUHUSIWA KUFANYA MASTERS KAMA AMEFANYA MIAKA 4 INCLUDING 1 YEAR YA HONS.
 
Hons degree ni degree Ya heshima.ambaye anapewa Mwanafunzi ambaye hana supplementary wala carry over.
 
anapewa yule mtu ambae kila semister GPA inapanda mpaka semister ya mwisho bila kujali sup wala carry,kila chuo hapa bongo wanatoa hii
 
Mi nikajua ni degree yenye uheshimiwa kama wabunge wa bongo....
 
Ili upate hons degree lazima ufaulu masomo yote na wala usirudie somo lolote. Pia hons degree inatolewa kwa Mwanafunzi ambaye amesoma kwa miaka mitatu na GPA yake haijashuka.Mimi nimemaliza Mwaka 2012 udsm nimepata hons degree. Ila kuna Rafiki zangu nimemaliza nao hawana hons degree kwa vile hawakufanya vizuri kwenye mitihani yao.
 
Unaweza uka carry na kupata hon degree,unatakiwa performance yako iwe inapanda kila semister,na hii ni ngumu sana coz unaweza ukapiga vizuri semister ya kwanza A ila ya pili ukapata kalai za kutosha ukawa umepoteza sifa
 
Ni kama hivi au??
 
Attachments

  • 1434088005603.jpg
    1434088005603.jpg
    61.1 KB · Views: 877
veteran, mimi nimesoma Chuo cha Taifa.

GPA yangu ni ya mawimbi, yaani inapanda na kushuka, nimewahi kupata sapu moja lakini cha ajabu nina Degree with Honours na vigezo vyote ambavyo nimekuwa nikivisikia kwangu haviaplai... Labda kimoja cha kusema kuwa endapo GPA yako inazidi 3.5 basi unafuzu kuwa na shahada yenye heshima maana mimi nimegota kwenye 3.8, Shahada ya Kwanza ya Taaluma za Kiswahili.

Karibu!
 
Last edited by a moderator:
Wahitimu wa mwakajana wengi wamepewa honourable degrees hata kama ana lower second kwasababu ndo first product ya shule za kata. Kwahiyo wamewapa heshima yao.
 
Hons degree zipo nchi za Ulaya au South Africa.

Kwa bahati mimi nilisoma South Africa, University of Free State. Kwa kawaida degree ya kwanza ni miaka 3 inaitwa first degree NA SIO 'hons' kama inavyoitwa huku kwetu. Baada ya hapo mwanafunzi anasoma mwaka mmoja ili apate hons. Yaani anaandaliwa kufanya masters degree. Kwa kwetu ni usanii.

KWA MAANA HIYO KWA SOUTH AFRICA AU U.K MWANAFUNZI ANARUHUSIWA KUFANYA MASTERS KAMA AMEFANYA MIAKA 4 INCLUDING 1 YEAR YA HONS.

mmmmmmmmmh...
 
veteran, mimi nimesoma Chuo cha Taifa.

GPA yangu ni ya mawimbi, yaani inapanda na kushuka, nimewahi kupata sapu moja lakini cha ajabu nina Degree with Honours na vigezo vyote ambavyo nimekuwa nikivisikia kwangu haviaplai... Labda kimoja cha kusema kuwa endapo GPA yako inazidi 3.5 basi unafuzu kuwa na shahada yenye heshima maana mimi nimegota kwenye 3.8, Shahada ya Kwanza ya Taaluma za Kiswahili.

Karibu!

Upo sahihi mkuu
 
Last edited by a moderator:
Hons degree ni degree Ya heshima.ambaye anapewa Mwanafunzi ambaye hana supplementary wala carry over.

kibongobongo hii inawezekana kweli? kwani bongo mwanafunzi na hizo supplimentary na carry over ni sawa na kuuliza rushwa / ufisadi ccm.
 
Hons degree zipo nchi za Ulaya au South Africa.

Kwa bahati mimi nilisoma South Africa, University of Free State. Kwa kawaida degree ya kwanza ni miaka 3 inaitwa first degree NA SIO 'hons' kama inavyoitwa huku kwetu. Baada ya hapo mwanafunzi anasoma mwaka mmoja ili apate hons. Yaani anaandaliwa kufanya masters degree. Kwa kwetu ni usanii.

KWA MAANA HIYO KWA SOUTH AFRICA AU U.K MWANAFUNZI ANARUHUSIWA KUFANYA MASTERS KAMA AMEFANYA MIAKA 4 INCLUDING 1 YEAR YA HONS.

Dah..wewe ndio wataka kutuokota kwelikweli!
 
wewe ndio ndorobo kweli. Yaani unaulizwa dawa ya maralia, wewe unatoa dawa ya mafua.
 
Mimi nina lower second with honours kutoka udsm,na nimechezea supp za kutosha pia toka niko second year,lakini pia nadhani ni vile GPA yangu ilikua haishuki chni ya 3.
 
Back
Top Bottom