Nini maana Ya DISTINCTION katika matokeo?

Nini maana Ya DISTINCTION katika matokeo?

Jerindeo

Member
Joined
Aug 15, 2013
Posts
74
Reaction score
33
Wadau naomba mnisaidie kujua maana hasa ya DISTINCTION, CREDIT na PASS. Nina mdogo wangu amemaliza Ualimu na tunajaribu kupata maana ya ufaulu uliowekwa imekuwa ni shiiiida tu.

Matokeo ya Ualimu GPA ya 4.1 imeeitwa CREDIT wakati ACSEE GPA 3.7 ni Distinction. Ha Ha Ha Ha, BRN ni chiboko ya Kidato cha sita manake mwenye GPA ya 1.7 kapewa CREDIT wakati mwalimu mwenye GPA ya 3.3 kapewa kiwango cha chini kabisa cha ufaulu cha PASS. Jamani hiki ni nini, tunasema alimu hawana uwezo kumbe Kidato cha Sita wamewezeshwa na hata Walimu wakiwezeshwa wataonekana wanaweza.

Tizama Kidato cha Sita http://necta.go.tz/matokeo/2015/ACSEE2015/s0155.htm

Linganisha na Ualimu http://necta.go.tz/matokeo/2015/GATCE2015/510.htm
 
Duuuh. Mbona haileweki kabisa? Wadau mnaoelewa hili msaada please
 
noun (plural distinctions)
That which distinguishes; a single occurrence of a determining factor or feature, the fact of being divided; separation, discrimination.
The act of distinguishing, discriminating; discrimination
specifically, a feature that that causes someone or something to stand out as being better; a mark of honour, rank, eminence or excellence; being distinguished.
 
Namm nataka kujua ili ufanye mtihani wa kidato cha sita unahitaji credit ngapi na je masomo kama elimu ya dini au literatuer credit zake zinahesabiwa au laa
 
Namm nataka kujua ili ufanye mtihani wa kidato cha sita unahitaji credit ngapi na je masomo kama elimu ya dini au literatuer credit zake zinahesabiwa au laa

Kwa tuliomaliza 2012 kurudi nyuma ilikuwa ili ufanye mtihani wa kidato cha sita lazima uwe na C tatu na kuendelea,masomo ya dini huwa hawayahesabu
 
Nami ni muhitimu wa ualimu, na madaraja haya ya ufaulu nimeyafuatilia kwa makini na karibu sana..

KWA UALIMU:
1. DISTINCTION ni daraja la juu la ufaulu lenye GPA kuanzia 4.5 - 5.0
2. CREDIT ni daraja la ufaulu la pili baada ya distinction lenye GPA kuanzia 3.6 - 4.4
3. PASS ni daraja la ufaulu lenye GPA kuanzia 2.0 - 3.5..
4. SUPPLEMENTARY (SUPP) ni daraja analopewa mtahiniwa mwenye GPA yoyote lakini amefeli (amepata F) kuanzia somo moja mpaka manne.
5. FAIL ni daraja analopewa mtahiniwa aliyefeli (aliyepata F) kuanzia masomo matano au zaidi..

KWA O NA A LEVEL:
1. DISTINCTION (GPA 3.6 - 5.0)
2. MERIT (GPA 2.6 - 3.5)
3. CREDIT (GPA 1.6 - 2.5)
4. PASS (GPA 0.3 - 1.5)
5. FAIL (GPA 0.0 - 0.2)
 
Duh, kweli hapo ni mtihani mwingine. Inakuaje nchi ile ile ina band tofauti za GPA? Kuna nchi maximum GPA yao ni 4.0 sio 5.0 kama hapa TZ, laiti ualimu na o-level,A level zingetofautiana maximum GPA yaani 4 na 5 nadhani utata huu usingekuwapo lkn hapa pana BRN tu sbb GPA ni ile ile lkn band tofauti.
 
Mnashangaa haya kuna ya dip mwaka wa kwanza,nta level 5 ni kubwa 4.0 na mwaka wa pili ,nta level 6 gpa kubwa ni 5.0
 
Duh, kweli hapo ni mtihani mwingine. Inakuaje nchi ile ile ina band tofauti za GPA? Kuna nchi maximum GPA yao ni 4.0 sio 5.0 kama hapa TZ, laiti ualimu na o-level,A level zingetofautiana maximum GPA yaani 4 na 5 nadhani utata huu usingekuwapo lkn hapa pana BRN tu sbb GPA ni ile ile lkn band tofauti.

Mkuu, mfumo wa GPA kwa O na A Level umeanza kutumika mwaka 2014, na ni kazi ya BRN kama usemavyo
 
Back
Top Bottom