Blessed Son
Member
- Apr 23, 2015
- 34
- 23
Naomba kujuzwa maana ya hilo neno maanq mara nyingi nimekuwa nkisikia kuwa mtu fulani anataka "kuadopt" mtoto
Ni kumchukua mtoto ambae hujamzaa akawa mwanao, akapata haki zote kama mwanao wa kumzaa na akawa sehemu ya warithi wako... Wanasema 'kuasili' kwa Kiswahili.
Umefanya vema, mrejesho ni muhimu...Mkuu Blessed Son umeelewa? thumb up Mbilimbi Mbovu
Mkuu, huu ufafanuzi ni kwa mujibu wa Sheria zetu? Huku huwa unamchukua mtoto, mnalimaliza kifamilia na maisha yanaanza... Ubaya wake ni kuwa mtu akijisikia anaweza kutelekeza mtoto muda wowote!Ni kuasili mtoto, mtoto asiye wako wa kuzaa unamchukua kisheria anakuwa wako.
Kwann watu wanaadopt?
1.kuzaa watoto wa jinsia moja
2.kutokuwa na uwezo wa kuzaa/kuzalisha.
3. Mapenzi/upendo n.k mtoto ambaye umem-adopt huwez kumuona nikosa kisheria.
Pia mtoto unayem-adopt lazima umzidi miaka 21. Atapata haki sawa kama mtoto wako wa kuzaa. Sifa za ku-adopt lazima uwe na uwezo wa kumtunza ikiwa ni pamoja na kumsomesha mtoto unayetaka kum-adopt n.k
Mkuu, huu ufafanuzi ni kwa mujibu wa Sheria zetu? Huku huwa unamchukua mtotot, mnalimaliza kifamilia na maisha yanaanza... Ubaya wake ni kuwa mtu akijisikia anaweza kutelekeza mtoto muda wowote!