Nini maana ya bunge la 11 mkutano wa 7 kikao cha 32?

kidunula1

JF-Expert Member
Apr 2, 2016
6,299
6,321
Amani kwenu wadau

Kichwa chajieleza hapo juu. Kwa wajuzi wa taratibu za bunge naomba anifafanulie kama nilivyouliza hapo juu. Zaid naomba kujua lile lifimbo likubwa lina rangi ya dhahabu,hubebwa na askari wa bunge ni kitu gani na kina kazi gani? Asante!
 
Ninavyoelewa ni hivi;

Bunge la 11 tangu tupate uhuru, tukianza kwa Mwinyi kulikuwa na mabunge mawili(2) '85-'90, '90-'95, Mkapa mawili(2) '95-'00, '00-'05, Kikwete pia mawili(2) '05-'10, '10-'15. Jumla ni mabunge 6, Hili la JPM ni la saba(7) '15-'20 tangu kipindi cha Mwinyi. Kipindi cha Nyerere (nadhani) kulikuwa na mabunge manne.

Mwingine aeleze kuhusu mikutano na vikao.
 
Hapa Nimejifunza mwenyewe... Bunge la 11 wamehesabu kila term ya uchaguzi mkuu wanapochaguliwa wabunge imefikia mara kumi na moja . Mkutano wa saba ni bunge hili tangu 2015 limekutana mara7 na katika hii mara ya saba wamekaa (kikao) mara 32. Nadhani umenierewa!
 
Ninavyoelewa ni hivi;

Bunge la 11 tangu tupate uhuru, tukianza kwa Mwinyi kulikuwa na mabunge mawili(2) '85-'90, '90-'95, Mkapa mawili(2) '95-'00, '00-'05, Kikwete pia mawili(2) '05-'10, '10-'15. Jumla ni mabunge 6, Hili la JPM ni la saba(7) '15-'20 tangu kipindi cha Mwinyi. Kipindi cha Nyerere (nadhani) kulikuwa na mabunge manne.

Mwingine aeleze kuhusu mikutano na vikao.
Means kila muhula wa miaka 5 inahesabika kuwa bunge 1 syo? Maana hata mimi hiyo lugha huwa inanichanganya sanaaa
 
Back
Top Bottom