Nini kinasababisha msichana kumuita mwanaume kaka?

proskaeur

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
1,571
4,925
Wakuu habari za muda huu,

Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada,

Ni hivi hapa chuoni ninaposoma kuna msichana fulani ni mwaka wa kwanza mimi niko mbele yake kidogo nilijenga nae urafiki nikamuomba namba lengo likiwa ni kumtongoza, lakini kilichotokea ni kama alinipiga counter attack coz siku ya kwanza tu kabla sijarusha ndoano akaanza kuniita kaka, sasa hapo ndio nikaishiwa pozi jinsi ya kuibadilisha hiyo kaka.

Kwa wazoefu na mambo haya naombeni msaada nifanyeje ili nikimtongoza asije kuanzisha stori za mara ooh sijui nilikuheshimu kama kaka yangu coz msichana nimetokea kumuelewa kiukweli.

Msaada tafadhali kama ishawai kukutokea.

Je ulifanyaje? Au mimi nifanye nini ili anielewe.

Nakaribisha mawazo na ushauri!
 
Wakuu habar za muda huu!!

ngja niend moja kwa moja kweny mada,,ni hivi hapa chuoni naposoma kuna demu fulan ni mwaka wa kwanza mimi niko mbele yake kidgo nilijenga nae urafiki nikamuomba namba lengo likiwa ni kumtongoza,,lakin kilichotokea ni kama alinipiga counter attack coz cku ya kwanza tu kabla cjarusha ndoano akaanza kuniita KAKA ,,sasa hapo nd nkaishiwa pozi jinsi ya kuibadrsha hiyo KAKA

Kwa wazoefu na mambo haya naomben msaada nifanyj ili nikimtongoza asije kuanzisha stori za mara ooh cjui nilikuheshimu km kaka yangu coz demu nimetokea kumuelewa kiukwel ,,msaada tafadhali km ishawai kukutkea je ulifanyaj!? au mi nifany nn ili anielewe

Nakaribish mawazo na ushauri!!!

Embu nipe namba yake nikurahisishie kazi.
 
Kama msichana siyo dada wa kwa kuzaliwa tumbo moja au ndugu pinga kwa nguvu zote kuitwa kaka au wewe kumuita dada...

Muite kwa jina lake... Na wewe mzoeshe akuite kwa majina yako..

Vinginevyo wewe utaitwa kaka rafiki yako ataitwa mpenzi...
 
Akikuita kaka mwambie mbona unanizeesha alaf weka sura ya mbuzi......

Kaza mpk ilo jina la kaka lipotee alaf apo ndo uwanze kutupia samjo maana bila ivyo kupata mbunye ni ngumu joh alaf madem kama hawo wanakuwaga seriouse na masomo church ndo usiseme
 
umenchekesha,eti church ndo usiseme!!mi kama mtu sijampenda,yani naanzaga kumuita kaka fastaaaa tu!!
 
mkuu labda ajaelewa jambo dogo tu hapo.... kwenye mawazo yake achukue tafsiri ya kaka from anaza maza
na mtongozo unaendelea vizur tu
 
Wakuu habari za muda huu,

Ngoja niende moja kwa moja kwenye mada,

Ni hivi hapa chuoni ninaposoma kuna msichana fulani ni mwaka wa kwanza mimi niko mbele yake kidogo nilijenga nae urafiki nikamuomba namba lengo likiwa ni kumtongoza, lakini kilichotokea ni kama alinipiga counter attack coz siku ya kwanza tu kabla sijarusha ndoano akaanza kuniita kaka, sasa hapo ndio nikaishiwa pozi jinsi ya kuibadilisha hiyo kaka.

Kwa wazoefu na mambo haya naombeni msaada nifanyeje ili nikimtongoza asije kuanzisha stori za mara ooh sijui nilikuheshimu kama kaka yangu coz msichana nimetokea kumuelewa kiukweli.

Msaada tafadhali kama ishawai kukutokea.

Je ulifanyaje? Au mimi nifanye nini ili anielewe.

Nakaribisha mawazo na ushauri!
Wewe itika ili ujenge ukaribu na yeye, we jifanye mjinga. Proximity inajenga attraction kubwa.
 
Back
Top Bottom