Nini kinaendelea Ngorongoro?

Hakuna lililopotezewa hapa, ukosefu wa kupata taarifa kwa wakati ndio sababu ya ukimya.
 
Niliwahi sema huko nyuma kwamba waTanzania tunaongozwa na mihemko alafu tunasahau mazima baada ya muda mfupi tunadandia kingine.

Ilitokea loliondo, ikaja ngorongoro, then ikahamia kwa Dugange ajiuzulu, ghafla ripoti ya CAG ikaibuka then kwa Sasa upepo ukahamia kwa Dp World!! Believe me Leo hii Diamond platnumz akisema anajiunga kwenye siasa awe mbunge attention yote itahamia huko na tutasahau kabisa bandari!!

Ni nchi ya ajabu sana hii
 
Wabongo wana firigiswa kila kona


Ova
 
Ulichokiandika hapa ni tafsiri yako, haki yako.

Lakini kwangu nina mtazamo tofauti kabisa, hasa kwa hili la bandari tulilokaa nalo kwa zaidi ya miezi miwili, na halioneshi dalili ya kupoa mpaka majibu ya maana yapatikane.

Usiishi kwa mazoea, hasa kama suala linalojadiliwa linahusu rasilimali za watanganyika.
 
Tuanze kuuliza sehemu nyingine walikochagua kuweka makazi ili kama kujiondokea kwenda burundi au kwingine tuanzage mapema kabisa.
 
Hii Nchi inamilikiwa na watu wachache sana.., wanaobaki ni bendela.
 
 

Attachments

  • facebook_video_1692774220244.mp4
    1.5 MB
Nafikiri Waraka umegusa mpaka mbugani huko,karejee kusoma vizuri.
 
Wenyeji wanasema waarabu wamejaa ngorongoro kuchimba madini ya pozzolana na ruby.wananchi wametakiwa kuondoka kwa lazima ili waarabu wa neemeke.hakuna cha uhifadhi tena
 
Tulia yeye yupo kule Mbeya anatetea Mkataba wa Bandari badala ya kusimamia heshima ya Mhimili wa Bunge.

Tuna Spika wa aina yake kuwahi kutokea.
 
Alifanya/sema je/nini!??
 
Ngorongoro hali sio shwari kabisa kuna mambo mbalimbali yanayoendelea huko ya uvunjifu wa haki za binadamu

Moto unaowaka Ngorongoro hakuna tofauti na DP world sema issue ya Ngorongoro hatujaipa airtime

Ni wakati sasa watanzania tupaze sauti kwa kuendelea kuandika mitandaoni hali halisi ya Ngorongoro na tusiwategemee waandishi wa habari waliokambishwa asali

Ngorongoro hali sio shwari kabisa.
 
Huko Ngorongoro ni mwendo kamata, weka ndani, peleka kusikojulikana, piga, vunja maboma ya wamasai na piga marufuku kutoa habari!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…