Nini kinacho-define mafanikio katika maisha ya mwanadamu?

Asante kwa maelezo. Ila hivyo vitu unavyotamani kuvifanya au kuvifikia ni vipi? Swali lako la mwisho, limebeba ujumbe mzito na wa maana sana. Kwa hiyo ukishafahamu wewe umeletwa duniani kucheza role gani (kusudio fulani), hiyo ndiyo inakuwa njia na mwanga katika kupata mafanikio? Hivyo unataka kusema ili kuweza kufanikiwa katika maisha, binadamu anapaswa ajitambue kwanza?

mbona unakwenda off track bana, wewe umetaka kujua mafanikio ni, sasa unajadili njia inayoweza kumfikisha mtu kwenye mafanikio.
 
kwangu mimi mafanikio hasa ya kimaisha ni pale unaporidhika na hali uliyo nayo!mimi binafsi nimeshindwa kuelewana na baadhi ya ndugu zangu wa kuzaliwa kisa wananiona mimi kama sina maendeleo ya kutosha kumbe roho yangu ina maendeo kwa kuwa najua siku moja nitaondoka hapa duniani'
Mafanikio ni kuwa na uwezo wa kujisimamia mwenyewe'mafanikio ni kuwa na uwezo wa kukataa kuiba mali ya umma'mafanikio ni kuwa na uwezo wa kujitambua!
 
Kuna quote ya kutoka kitabu cha kikristo, Biblia, 2 Timothy 4: 7 sehemu yake inasema "[SUP]7[/SUP]Nimepigana ile vita njema, nimemaliza shindano, nimeitunza imani." kwa mtazamo wangu aliyetimiza hayo (kwa mtazamo wowote ule) basi huyo amefanikiwa.

 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Kiukweli mafanikio yana mtazamo mpana sana kama vile KIROHO,KIFAMILIA,KIFEDHA,KIAFYA,KIFIKRA na maisha ya furaha na amani bila kusahau mchango wako katika jamii.Japo kila mtu anaweza kutafsiri kwa namna ajuavyo lakini mara nyingi tumeona watu wakifanikiwa katika baadhi ya vitu na sio vitu vyote.....mfano mtu ana elimu nzuri lakini kifedha hali mbaya,au unafedha nyingi afya mbovu.Tukumbuke sio rahisi kufikia utimilifu wa ubinadamu lakini lazima kupata balance ya maisha kwa maana kwamba uwe na maisha yenye furaha kwa uwiano mzuri katika nyanja tofauti.
 
kama nimemuelewa mleta mada, ni kwamba anazungumzia mafanikio yakiwa judged na watu wengine, sio self satisfaction.

Asante kwa kunielewa. Hakika hayo juu ndiyo msingi wa mada. Ukiondoka,watu watakuzungumzia vipi juu ya "mafanikio" uliyoyapata ulipokuwa hai? Wataya-define vipi hayo mafanikio?

Vitu vingine vimeingia tu katika mijadala. Lakini msingi mkuu ni namna watu wanavyo-define "mafanikio" ya mtu mwingine.
 
mbona unakwenda off track bana, wewe umetaka kujua mafanikio ni, sasa unajadili njia inayoweza kumfikisha mtu kwenye mafanikio.

Mkuu,hiyo ilijitokeza kama mazungumzo baada ya habari. Lakini habari kuu,bado ipo vilevile.

Ila kuna jambo nimejifunza hapa kwamba,watu wengi hawajali namna watu wanavyo-define mafanikio yao. Wenyewe wanaamini kwamba maana ya mafanikio katika maisha yao,ni kwa kuzingatia matakwa yao,na namna wanavyoya-define wenyewe.
 
mafanikio kwangu ni kwa namna gani uwepo wangu duniani utaweza kuwafikia watu wengi, tena kwa jinsi nzuri na kwa namna moja au nyingine kuwawezesha kubadili maisha au hata muonekano wa mitazamo yao kwa namna bora zaidi ya walivyokuwa kabla ya uwepo wangu. Hayo kwangu mimi ndio mafanikio ya ziara yangu fupi hapa duniani!

Kwahiyo wewe siku utakapotangulia mbele za haki;watu watayaeleza mafanikio yako katika misingi ya kuishi vyema na watu na kuweza kubadili maisha yao?
 
Watu wanaweza kuwa na definitions mbalimbali za mafaninikio.Lakini wengi hasa wasio mjua Mungu, wanadhani mafanikio ni yale yanayohusiana na kuustarehesha mwili.Kama unavyosema, kuwa na magari,nyumba nzuri nk.But that is nonsense, kwakuwa maisha ya duniani ni mafupi na safari towards a more permanent life ya umilele.Sio vibaya kuwa na nyumba na magari,lakini la msingi ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wa kweli.Remember there are so many gods,hata Maitreya ni mungu kwa wengine,but he is not a true God.So mafanikio ya kweli duniani ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wa kweli.Mengine yafuate baada ya hapo.

Kwahiyo kwako kuwa na uhusiano mzuri na Mungu ni mafanikio? Je,siku husipokuwepo,watu watasema ulifanikiwa duniani kwakuwa ulikua mcha Mungu? Kwa wale wasioamini Mungu,wata-define vipi mafanikio yako?
 
mafanikio =success??
kama ndivyo ...maana yake kuna kitu ulikuwa unapigania au kustruggle ndio umefanikisha...

kitu hicho ni kipi??

kila mmoja ana priorities zake

wakati maskini anatafuta mali.....tajiri anatafuta amani!!

personally nadhani mafanikio ni kuwa na FURAHA NA AMANI IDUMUYO!

You may be hungry but peacefull, you may not have money but joyfully

watoto wa maskini wanaochezea mpira wa kufunga funga na kamba fuaha yao ni sawa kabisa na watoto wa matajiri wanaochezea mpira wa dukani!!

Amani ya kweli inapatikana kwa kumjua Mungu

Kwahiyo kwako mafanikio unaya-define vile unavyojisikia na kuona na si watu wanavyona?
Je,kwa kuwa na FURAHA NA AMANI IDUMUYO,siku ukifa,watu wataelezea mafanikio yako katika misingi hiyo?
 
hili swali halina jibu kamili. its is relative to what you are refering to. muda mwingine mtu huwa anasema amefanikiwa pale anapotaka jambo fulani na akalipata. kwahiyo unapopata unachokitaka kwa wakati huo basi hayo ni mafanikio.

Je,watu watasemaje juu yako? Juu ya mafanikio yako.
 
kwangu mimi mafanikio hasa ya kimaisha ni pale unaporidhika na hali uliyo nayo!mimi binafsi nimeshindwa kuelewana na baadhi ya ndugu zangu wa kuzaliwa kisa wananiona mimi kama sina maendeleo ya kutosha kumbe roho yangu ina maendeo kwa kuwa najua siku moja nitaondoka hapa duniani'
Mafanikio ni kuwa na uwezo wa kujisimamia mwenyewe'mafanikio ni kuwa na uwezo wa kukataa kuiba mali ya umma'mafanikio ni kuwa na uwezo wa kujitambua!

Mkuu naamini uko kwenye right track though u should make ur family understand u. Kama tunaishi ili tufe, basi we are nothing bt unlucky creatures.. Mafanikio ya mtu yanategemea uelewa wake wa maisha na malengo aliyojiwekea kutokana na huo uelewa.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Kuna quote ya kutoka kitabu cha kikristo, Biblia, 2 Timothy 4: 7 sehemu yake inasema "[SUP]7[/SUP]Nimepigana ile vita njema, nimemaliza shindano, nimeitunza imani." kwa mtazamo wangu aliyetimiza hayo (kwa mtazamo wowote ule) basi huyo amefanikiwa.


Nimeipenda hii bt nimegundua hapa Paulo hakuongelea "third party". Maana ya maisha hukamilika pale ambapo umejitahidi kufanya maisha ya wengine pia yanakua bora. This is my belief!
 
  • Thanks
Reactions: Nzi

Similar Discussions

Back
Top Bottom