Nini kinacho-define mafanikio katika maisha ya mwanadamu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini kinacho-define mafanikio katika maisha ya mwanadamu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Nzi, Apr 10, 2012.

 1. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Salaam wana JF!

  Kama wasafiri hapa duniani, binadamu tumekuwa tukipigana na kujitahidi kwamba tunapata mafanikio ili siku pale parapanda litakapolia, basi mtu aweze kuondoka na kuacha alama, kwamba jamaa alikuwa amefanikiwa au hajafanikiwa kimaisha n.k.

  Je, mafanikio katika maisha ya binadamu ni nini?
  Yanakuwa defined vipi?
  Ni yapi yanayotufanye tuseme fulani kafanikiwa kimaisha?


  Je, kuwa na mali nyingi - magari, nyumba, pesa n.k. ni mafanikio katika maisha?
  Je, kusafiri na kutembelea nchi na sehemu mbalimbali duniani (hata nje ya dunia, mwezini, angani n.k.), ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na kazi nzuri (yenye mshahara mnono au kazi unayoipenda), ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na watoto wengi, ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na marafiki wengi (kuishi vizuri na binadamu wenzako), ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na machapisho mengi (vitabu, articles n.k.), ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na wake/waume au wapenzi wengi ni mafanikio katika maisha?
  Je, kuwa na mume au mke, ni mafanikio katika maisha?
  Je, kushika neno la Mungu na kumwamini Yeye, ni mafanikio katika maisha?


  Je, kuna universal meaning ya mafanikio ya maisha?

  Hakika ninapata ugumu katika kudefine mafanikio katika maisha!

  NB: Mtanisamehe sana kama mada kama hii imeshawahi kujadiliwa; kama ndiyo, basi ifutwe.
   
 2. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Mafanikio kwangu yalipatikana kipindi nilipompokea Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yangu.
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,404
  Trophy Points: 280
  Mafanikio ni kuwa na pesa mingi bwana!!
   
 4. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Mafanikio ni kuwa na taaluma/kipaji, Afya njema,fedha au kipato cha uhakika na Familia bora kama huna baadhi au vyote kati ya hivyo hapo juu haujafanikiwa.Kwa hiyo endelea kuvisaka.
   
 5. papason

  papason JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 2,317
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Hiyo ni relative terminology!

  binafsi nikipata wake wanne ni mafanikio makubwa kweli kweli......

  mwingine akipata baiskeli mbili ni mafanikio ya ajabu kweli kweli!
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Pesa nyingi tu?! Hujali binadamu wenzako wanaokuzunguka? Ukifa, pesa zitakuzika?!
  Ukifa, nani atakusifia kwamba una mafanikio ukifa kama wewe mafanikio kwako ni kuwa na pesa mingi?!?
   
 7. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo ipi ndio maana halisi? Kuwa na hivyo vyote au kuwa na kimoja kati hivyo?
  Je, nikiwa na afya njema, nakuwa nimefanikiwa kimaisha?
  Je, nikiwa na taaluma/kipaji, nakuwa nimefanikiwa kimaisha?
  Je, nikiwa na fedha au kipato cha uhakika, nakuwa nimefanikiwa kimaisha?
  Je, nikiwa na familia bora, nakuwa nimefanikiwa kimaisha?
   
 8. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Angalau umenipa mwanga kidogo. Lakini:
  Kwa hiyo hakuna universal meaning?
  Kwa hiyo unataka kumainisha hakuna binadamu aliye na mafanikio katika maisha kwa sababu maana ya mafanikio inatofautiana baina ya wanadamu au?
   
 9. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  Mafaniko kwangu ni kuweza kutimiza njozi nilizonazo.

  Kuna vitu fulani natamani kuvifanya au kuvifikia, nitajiona nimefanikiwa siku nikivimaliza.

  Mtizamo wangu wa maisha ni kama movie, unaletwa duniani kucheza part fulani, ukiimaliza lazima uondoke.

  Cha kujiuliza, ulikuja hapa duniani ili ukamilishe nini? Ukishajua umekuja ili ufanye nini, basi kamilisha kusudio hilo.
   
 10. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,858
  Likes Received: 4,537
  Trophy Points: 280
  Asante kwa maelezo. Ila hivyo vitu unavyotamani kuvifanya au kuvifikia ni vipi? Swali lako la mwisho, limebeba ujumbe mzito na wa maana sana. Kwa hiyo ukishafahamu wewe umeletwa duniani kucheza role gani (kusudio fulani), hiyo ndiyo inakuwa njia na mwanga katika kupata mafanikio? Hivyo unataka kusema ili kuweza kufanikiwa katika maisha, binadamu anapaswa ajitambue kwanza?
   
 11. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  mafanikio kwangu ni kwa namna gani uwepo wangu duniani utaweza kuwafikia watu wengi, tena kwa jinsi nzuri na kwa namna moja au nyingine kuwawezesha kubadili maisha au hata muonekano wa mitazamo yao kwa namna bora zaidi ya walivyokuwa kabla ya uwepo wangu. Hayo kwangu mimi ndio mafanikio ya ziara yangu fupi hapa duniani!
   
 12. sun wu

  sun wu JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 2,025
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 0
  "Success should be measured not so much by the position that one has reached in life... but by obstacles which he/she has overcome while trying to succeed."

  Mkuu inategemea kama mimi nimejitahidi bila elimu wala bila mtaji wowote nikijitahidi na kuweza kufungua kibanda cha nyanya nitakuwa-more successfully kuliko yule aliyeweza kujenga hoteli kwa kutumia mikopo au urithi na support ya wazazi.

  Nikiwa siwezi kuongea vizuri nikajitahidi kutoa single moja nitakuwa more successfully huenda kuliko hata Whitney au Michael ambao walikuwa na vipaji
   
 13. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Watu wanaweza kuwa na definitions mbalimbali za mafaninikio.Lakini wengi hasa wasio mjua Mungu, wanadhani mafanikio ni yale yanayohusiana na kuustarehesha mwili.Kama unavyosema, kuwa na magari,nyumba nzuri nk.But that is nonsense, kwakuwa maisha ya duniani ni mafupi na safari towards a more permanent life ya umilele.Sio vibaya kuwa na nyumba na magari,lakini la msingi ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wa kweli.Remember there are so many gods,hata Maitreya ni mungu kwa wengine,but he is not a true God.So mafanikio ya kweli duniani ni kuwa na uhusiano mzuri na Mungu wa kweli.Mengine yafuate baada ya hapo.
   
 14. S

  SURUMA JF-Expert Member

  #14
  Apr 11, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,908
  Likes Received: 124
  Trophy Points: 160
   
 15. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #15
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
   
 16. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #16
  Apr 11, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,598
  Likes Received: 3,888
  Trophy Points: 280
  mafanikio =success??
  kama ndivyo ...maana yake kuna kitu ulikuwa unapigania au kustruggle ndio umefanikisha...

  kitu hicho ni kipi??

  kila mmoja ana priorities zake

  wakati maskini anatafuta mali.....tajiri anatafuta amani!!

  personally nadhani mafanikio ni kuwa na FURAHA NA AMANI IDUMUYO!

  You may be hungry but peacefull, you may not have money but joyfully

  watoto wa maskini wanaochezea mpira wa kufunga funga na kamba fuaha yao ni sawa kabisa na watoto wa matajiri wanaochezea mpira wa dukani!!

  Amani ya kweli inapatikana kwa kumjua Mungu
   
 17. b

  b2k Member

  #17
  Apr 11, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hili swali halina jibu kamili. its is relative to what you are refering to. muda mwingine mtu huwa anasema amefanikiwa pale anapotaka jambo fulani na akalipata. kwahiyo unapopata unachokitaka kwa wakati huo basi hayo ni mafanikio.
   
 18. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #18
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  afya njema sio mafanikio bana, itoe kwenye kundi hili.
   
 19. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #19
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  kama nimemuelewa mleta mada, ni kwamba anazungumzia mafanikio yakiwa judged na watu wengine, sio self satisfaction.
   
 20. Lukansola

  Lukansola JF-Expert Member

  #20
  Apr 11, 2012
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 5,456
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  mafanikio gani unaulizia, jinsi anavyojisikia mtu binafsi au anavyoonekana kwa watu wengine?
   
Loading...