Nini kimepelekea mauti yake!

Jilanga

JF-Expert Member
Feb 13, 2011
255
40
Wakuu jamvini, imekuwa desturi na mazoea pale tunapopata taarifa ya kifo/vifo kuhuji nini basi kimepelekea kifo/vifo! Je lengo haswa ni kujua uzembe ama staili ya kifo ili nasi tujifunze siku nyingine ikibidi tukwepe kama ambavyo wahenga wasemavyo, "Tujifunze kupitia makosa/matukio ya wengine" au huwa tunauliza kwa kuwa imezoeleka hivyo!
NASUBIRI MTAZAMO WENU!
 
Nadhani ni lugha tu..ukisema nini kimepelekea...au nini kimesababisha...lengo ni lilelile..anyway..najipitia tu
 
Nadhani ni lugha tu..ukisema nini kimepelekea...au nini kimesababisha...lengo ni lilelile..anyway..najipitia tu
Lengo la kuuliza ni ili tujifunze kutokana na kifo/vifo ama ni mazoea tu?
 
Hii inatokana na umri, afya au tabia za marehemu. Tunaamini kuwa kijana wa miaka 18 hadi 45 bado hajawa sana katika hali ya kuandamwa na magonjwa ya uzee kama vile kisukari, kansa,BP nk. Tunaposikia kifo cha mtu kama huyu huwa tunasafirisha mawazo yetu kuwa amekufa kwa ajari kuliko wazee ambao wengine vifo vyao tunakuwa tunavitarajia.
Vilevile huwa tunaangalia afya ya marehemu ktk siku za nyuma mfano aliugua kwa muda mrefu au ameugua ghafla kupelea kifu chake. Hapa tunajirizisha kuwa mtu anayesumbuliwa na maradhi ya muda mrefu bila kupona ndiye mwenye nafasi kubwa ya kufa, hivyo hushangaa zaidi mtu aliyemzima kiafya na kufa gafla.
Pia tabia za marehemu pia zinaweza kuleta maswali mengi ktk kifo chake. Mfano ukisikia mtu ambaye hakuwa mwizi au muhuni ameuawa lazima utakuwa na maswali mengi zaidi kuliko akiuwawa mwizi.
Ni ukweli kabisa kuwa kujua sababu ya kifo cha mtu hutufanya watu tuwe makini ili tuweze kuzuia au kuwa makini na hali hizo zilizosababisha kifo. Kingine kinachotupa faida ni kuona utukufu wa mungu ktk kugawa pumzi kuwa hachagui masikini wala tajiri na hata uwe mjanja kiasi gani mwisho tutakufa tu.
 
Mkuu kuna kitu kinaitwa, The law of cause and effect, I think it is all about obeying that law.
 
Back
Top Bottom