Nini kimepelekea kutokuwepo kwa kesi za aina hii?

Nini kimepelekea kutokuwepo kwa kesi za aina hii?

WINGER_TEREZA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Posts
242
Reaction score
457
Habari wana jukwaa, naomba nijielekze kwenye mada moja kwa moja. Wakati wa serikali ya awamu ya tano chini ya hayati Magufuli ilikuwa ni nadra sana kupita week tatu, mwezi au miezi miwili bila kukamatwa na hatimaye kupelekwa mahakamani raia wa kawaida, wanasiasa au wanaharakati wakikabiliwa na kesi kadhaa. Leo nitaongelea aina mbili au tatu ya kesi hizo

Mosi, kesi za uchochezi

Miongoni mwa kesi maarufu zilizokuwa zikilindima kila uchwao pale "mahakam ya Kisutu" ni kesi za uchochezi. Yaani mtu alikuwa akitoa maoni yasiyokuwa yanaonekana kwenda kinyume na mitazamo ya wakubwa kule juu basi anaitwa mchochezi au mvuruga amani ya nchi. Hii ilipelekea kukamatwa kwa watumiaji wengi wa mitandao ya kijamii hasa facebook, Twitter na Instagram juu ya jumbe zao walizokuwa wanazichapisha katika mitandao hiyo. Ila hali imekuwa ni tofauti kwa serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kwa sasa zinakaribia kufika siku mia moja tangu Mhe. Samia aingie katika Ikulu za Chamino na Magogoni lakini hakuna mtu hata mmoja aliyetuhumiwa kutenda makosa ya uchochezi ilihali sheria, kanuni na taratibu zilizokuwa zinatumika awamu ya tano ni zilezile za awamu ya sita!. Kitu pekee kilichobadilika ni mtu mmoja tu, kutokuwepo kwa Mwendazake!.

Pili, Kesi za uhujumu uchumi na utakatishaji fedha

Hizi kesi ni kulwa na doto maana ukituhumiwa kutakatisha fedha kinachofuata ni matokeo yake ambayo ni kuhujumu uchumi. Katika utawala wa awamu ya tano ilikuwa ni kawaida kwa wafanya biashara, hasa wafanya biashara wakubwa, kukubwa na kadhia ya kutuhumiwa kutenda makosa haya ya uhujumu ujumi na matokeo yake kulikuwa na kesi nyingi pale "mahakama ya kisutu" zilizokuwa na muelekeo wa aina utakatishaji fedha na uhujumu uchumi.

Kwa upande mwingine hali nitofauti katika serikali hii maana hadi leo takribani siku zinakaribia 100 tangu Mhe. Samia aingie Ikulu hakuna hata kesi ya aina hii iliyoripotiwa ilihali mahakama, sheria, wafanya biashara na wasimamizi wa sheria ni walewale!.

Swali langu ni nini kimepelekea kutokuwepo kwa aina hizo za kesi ilihali wasimamizi wa sheria na sheria ni zilezile? Je wasimamizi wa sheria walikuwa wanafanya kazi kwa uoga wakati wa utawala wa Mwendazake au walikuwa wanalazimika kufanya hivyo kwa kupokea maekezo toka juu?

Wasalam.
 
Jamaa alitaka nchi itulie utadhani yupo sebuleni kwake anabangua "koosho"!Binadamu tumeumbwa na hulka tofautitofauti yeye aligoma. Akajipa presha "akasafiri"!Gone!😂😂😂😂
 
Mkuu hizo ndizo legacy maarufu za jamaa ambazo zimeondoka sambamba na yeye.
 
Nashauri hata hizo zilizopo zifutwe tu.

Maana kama zile za lissu haziendelei si bora zifutwe?

Zibaki hizi za akina sabaya na wengine
 
Kila alikpokosolewa aliamini ni uchochezi
 
Mwendazake mpumzisheni tu jamani, binadamu tumwogope Sir God na technology Watanzania hata bado hawajaamini...Daaah!
 
Back
Top Bottom