Nini kimepelekea Joni kupooza ghafla na Edo kuibuka kwa fujo?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,216
Kwa tulioanza kuzoea " mpela mpela " ya Joni tokea alipokabidhiwa funguo ya Magogoni mwaka jana November tulijua kuwa sasa SPIDI hii hii ya 120 itabaki kuwa ni ile ile hadi Watanzania wa kila Sekta tutakaponyooka na kurudi katika ile misingi yetu ya Kinidhamu ambayo tulikuwa nayo miaka ya Uongozi wa Hayati wawili tunaowalilia kila siku Sokoine na Nyerere.

Hata hivyo ni ghafla tu tuliopenda hii spidi ya " amsha amsha " ya Joni tumeanza kuingiwa sana na wasiwasi hasa baada ya Joni kurudi tu kutoka kuhudhuria Sherehe za kuapishwa kwa " Mzee Mbishi " Afrika ya Mashariki ambapo kusema ukweli huyu Joni wa sasa si yule wa kabla hajaondoka kwenda kwa tuliowapiga mwaka 1978 hadi 1979.

Yafuatayo ni matukio ya Joni yanayotutia mno shaka sisi Wafuasi wake tuliotukuka wa staili yake ya " kanyaga twende " :

  1. Hivi Joni ni wa kuona UOZO kama ule wa JNIA halafu asichukue hatua pale pale?
  2. Hivi Joni ni wa kuchelewa kweli " kumtumbua " Mtu kama alivyosita kwa Watu wa JNIA?
  3. Hivi Joni ni wa " kumtumbua " Mtu tena Waziri halafu hata asitokee katika Vyombo vya Habari wakati kwa Mkuu wa Mkoa tu wa Shinyanga ambaye ni Mke wa Wajina mwenzie Joni aliweza kumtumbua mbele ya Kamera zote za Tanzania?
  4. Hivi Joni kweli ni wa kukaa kimya kiasi hiki hadi kushindwa kutoa tamko lolote la kumhusu Mr. Fingerprints ambaye anawapa shida Mawaziri na Wabunge wa Chama Tawala jinsi ya kumjibu na kumtetea?
  5. Hivi Joni kweli ni wa kupitisha Wiki nzima bila hata kupiga " mkwara " au hata " kumtumbua " Mtu?
  6. Hivi kweli Joni ni wa kuongea na Umma au hata pale Magogoni huku akiwa " Mpole " na mwenye kutia " Huruma " kiasi hiki / kile?
Joni umekumbwa na nini? Unatusononesha sisi tuliokuwa tunapenda na tayari tumeshaanza kuizoea formation yako ya Kiuongozi ya " Total Football " ambayo haina masihara na kwa kiasi Kikubwa sana imeleta nidhamu tangia uanze kulala hapo Magogoni.

Lakini wakati hali ikiwa hivi kwa Joni nimeshtushwa mno na kuibuka kwa ghafla kwa Edo tena akiwa ndiyo " mtamu " kama " mcharo ". Tokea Joni alipokabidhiwa funguo mwaka jana Edo alinywea na kupotea kabisa japo alikuwa akiibuka kwa nadra sana kama " nyambizi " ya Kijeshi lakini kimtazamo alionekana kupotea katika ramani ya Siasa nchini.

Huku Joni akiwa amepooza kama siyo kunywea ghafla Edo ameibuka upya akiwa na matukio yanayotia matumaini kama :

  1. Edo sasa amekuwa ni Mtu mwenye Furaha sana.
  2. Edo sasa anajiamini.
  3. Edo sasa hata kutabasamu anatabasamu.
  4. Edo sasa na yeye anapiga " mkwara ".
  5. Edo sasa anaanza kupamba vyombo vya Habari.
  6. Edo sasa ni kama kazaliwa upya kwani anaonekana ni mwenye afya nzuri.
Natambua kabisa kuwa humu wengi wenu mmebobea sana katika Siasa na ni " Wajuvi " wazuri mno wa mambo mbalimbali ya Kiuongozi na Kiutawala hivyo nawaombeni basi muweze kutupa huo utaalam wenu ili na sisi " mbayuwayu " tuweze kuelimika. Je nini kimemnyamazisha ghafla hivi Joni na kumuibua kwa nguvu mpya na ya kasi ya hatari Edo? au tuseme makali ya Joni sasa yameisha na hayawezi kunoleka tena ila nyota ya Edo imeshasafishika upya na Damu ya Yesu na sasa ni mwendo mdundo hadi 2020 pale Magogoni?

Karibuni nyote na " tiririkeni " tafadhali.
 
Uongozi ni busara...sio kuzunguka katika ofisi za umma na kutukana kila mtu,baadae na mawaziri nao wakawa wanazunguka nchi nzima wanatukana kama vile watumishi ni tatizo sana,sasa anatambua kwamba watumishi ni asilimia ndogo sana ya watanzania,mamilioni ya watanzania wanataka uchumi wao uimarike,hautaimarika kwa kuwatukana watumishi,muda si mrefu zao la pamba litaingia sokoni,hajawahi kutoa kauli yoyote kwenye zao hili na hata bei,bado korosho,kahawa.


..hapa hatujagusa ajirà kwa vijana,bei ya sukari,aliahidi kushusha bei ya vifaa vya ujenzi ili watu wajenge,badala yake wizara ya ardhi imetuma timu ya watu wakanyanganye wananchi viwanja kwa kushindwa kuviendeleza,uchumi umempiga chenga,wafanyabiashara wana wasiwasi wa kupoteza wana wasiwasi kuleta Miraji yao wanajua muda wowote watafilisiwa,hakuna anayeagiza mzigo kama zamani,wanaiogopa bandari ya dar hivyo mapato yameshuka,nchi bila mapato utaiendeshaje?
 
Hili la msambaza pingu linamshusha hazi sana alibidi atoe tamko Kali Na biti ata kwa wazee wa kupambana na takrima tu Na aunde kamati ya kulishughulikia haraka Na pia katulia naona wanaomwangusha ni wasaidizi wake jeshi la mtu mmoja alifai katika mapigano ya ardhini maadui wake ni wengi sana
 
Edo ndio kwanza anaanza kupasha maungo moto kwa ajili ya mechi ijayo.
John kila uchao hali inazidi kubadilika na anashusha morali ya wachezaji wa timu yake.

Angalia mapato yanaendelea kushuka. Hebu hiulize nondo zilizotolewa wa CAG kwa John . Tafajari Bunge limeruhusu kamati zake kufanya safari za nje. Ahadi ya kugawa bure sukari imeota mbawa. Zigo la kuuza nyumba za Serikali bila kufuata kanuni mwaka 2006, limekuwa kaa la moto kichwani kwa John.

Muda unaanza kutafsiri hali halisi.

"HAPA MABADILIKO TU"
 
Joni alikuwa anaenda chaka kwenye uchumi mpaka sasa hatuelewi ni namna gani shilingi yetu itaimarishwa dhidi ya dola bila kusahau mfumuko wa bei bado sukari na ishu zingine baada ya kutafakari akaamua kumwita mtaalamu wa uchumi kutoka chuo kikongwe. Vuta subira Tanzania ya viwanda inakuja!!!.
 
Back
Top Bottom