Nini kimemsibu ndugu yetu Mh Humphrey Pole Pole..

Nini kimemsibu ndugu yetu Mh Humphrey Pole Pole..

Mara ya mwisho nilimwona kwenye Video Clip moja hivi ikimwonyesha akiongoza magari barabarani kama trafiki maeneo ya Dar, ilikuwa zaidi ya miezi miwili iliyopita.

Jambo moja ambalo nina uhakika nalo ni kwamba, Pole Pole kwa sasa hana Amani wala furaha yoyote toka apewe ukuu wa wilaya kwa sababu, jamii imeishia Kumshangaa, Kumdharau na kumchukia. Na pia nina uhakika wa 100% kuwa Pole Pole yupo humu JF kila mara kwa kutumia ID fulani fulani hivi ili awe huru kuandika kile anachokiamini na most like ni KUKOSOA!
Huu ndo ukweli unaouma
 
Which Means mkuu kaizima ndoto ya Humphrey kiaina
alipelekwa musoma kuwa mkuu wa wilaya.....hakuna alama yoyote aliyoacha musoma......tangu ateuliwe ubungo....hata kuongelea suala la maji hakuna...

na ubungo ni chuma chikoli moto,huku kubenea,huku mnyika
 
Achana naye ,,,unawaza vitu ambavyo havitakusaidia badal kuwaza nawezaje kuingeza pesa kwenye account yangu,, wew unamuwaza mtu du,,,,,
Sijawahi ona
Watz wengi wanawajadili watu badala ya kujadili vitu/maendeleo. Ajabu wengine ni wanamme. Inatia aibu.
 
Duh, DC kawa trafic?? Alitokwa povu jingi sana huyu sijui alitegemea fadhila za JK kwa Mbatia zimtokee kwa JPM na apewe uwaziri wa katiba na sheria??
hahahaa ....bodaboda wanavyokunywa viroba...wangempitia
 
Watz wengi wanawajadili watu badala ya kujadili vitu/maendeleo. Ajabu wengine ni wanamme. Inatia aibu.

Siyo kila mmoja ana stress za maisha mkuu, worse enough hatumjadili kwa ubaya. Ni kiongozi wangu na mbwembwe zake nazijua ila naushangaa ukimya wake.

Huyu ni mkuu WA wilaya yangu so sioni tatizo kuulizia ukimya wake elihali kwangu nanunua maji.

Kingine, humu jf mbona tuna topic nyingi sana za kuzungumzia maendeleo? Hujaziona au wataka kila anaepost iwe Mada ni moja tu? Kujua kwingi mwishoe gizaa
 
Wanafiki utawajua ,unamtakia nini ,akitoka kwenye vyombo vya habari utasikia oh jamani anajikweza ,akikaa kimya oh jamani haonekani,nenda ofisini kwake kama una shida nae.
 
Siyo kila mmoja ana stress za maisha mkuu, worse enough hatumjadili kwa ubaya. Ni kiongozi wangu na mbwembwe zake nazijua ila naushangaa ukimya wake.

Huyu ni mkuu WA wilaya yangu so sioni tatizo kuulizia ukimya wake elihali kwangu nanunua maji.

Kingine, humu jf mbona tuna topic nyingi sana za kuzungumzia maendeleo? Hujaziona au wataka kila anaepost iwe Mada ni moja tu? Kujua kwingi mwishoe gizaa
Kamuulize diwani na mbunge wako kwanza kabla ya kurukia kwa mkuu wa wilaya na umemuuliza Polepole kama mtu binafsi na sio mkuu wa wilaya,acha visingizio.
 
Atakuwa anacheki spidi ya gari kwa kuwa wazee wamesha muonya kuwa steringi imekatika anatafuta namna ya kujiokoa asije kufia mtaloni.
 
Mkuu wetu hafanyi kazi na media bana muacheni apige kazi kimya kimya
 
Watz wengi wanawajadili watu badala ya kujadili vitu/maendeleo. Ajabu wengine ni wanamme. Inatia aibu.
Habari nyingi zinatengenezwa na watu...wewe unataka ajadiliwe nani??? Wale wanaomjadili Trump ndo unaona wanafanya kitu kizuri coz ni wazungu?? Fikiri kwa umakini jmi
 
Wangembakisha Musoma tu. Alikuwa anapanda boti kwenda kutafuta makokoro a. k.a. Nyavu zisizo stahili kwa uvuvi
 
Pole pole alikua na kiherehere mwaka Jana had kuikana katiba aliyoitetea na alivokuwa kimbele front alikua anatetea UDC ufutwe chakushangaza kaukubali. Apotee tu maana hana jipya
 
sasa hivi anahangaika kukamata malori ya mkaa akiwa na watendaji wa halmashauri.

maisha hayaaa!!!! from hero to .....

kuanzia kukaa na akina warioba,salim mpaka kukaa na maafisa tarafa na watendaji wa kata!!!!

kondakta akifoka anaufyata
.....
.......Mkuu umeuwa bendi ha ha ha ha ha
 
Ila humu ndani mnanipa raha sana....wazungu wanasema. You can make some people fools sometimes but not all the time!Sasa Mungu anawaona kwa jinsi alivyokuwa anaupinga ukuu wa wilaya.....
 
Back
Top Bottom