Nini kimemsibu binti Karume?

kipara kipya

JF-Expert Member
May 2, 2016
17,339
21,435
Baada ya uchaguzi mkuu, aliibuka mwanasheria machachari alikuwa akichambua vifungu vya sheria na katiba ya nchi kwa utaalamu mwingi dhidi ya serikali ya CCM. Lakini cha ajabu tangu uchaguzi wa marudio ufanyike na Shein kupitia CCM kutangazwa mshindi huyu binti Karume haonekani tena wala kusikika kwenye vyombo vya habari.

Wadau mwenye kufahamu alipo atujulishe na kwanini yupo kimya wakati mapambano bado yanaendelea!
 
Baada ya uchaguzi mkuu,aliibuka mwanasheria machachari alikuwa akichambua vifungu vya sheria na katiba ya nchi kwa utaalamu mwingi dhidi ya serikali ya ccm,lakini cha ajabu tangu uchaguzi wa marudio ufanyike na shein kupitia ccm kutangazwa mshindi huyu binti karume haonekani tena wala kusikika kwenye vyombo vya habari,
Wadau mwenye kufahamu alipo atujulishe na kwanini yupo kimya wakati mapambano bado yanaendelea!
Kwa mtu anaejua na kuheshimu sheria hawezi tena kuhoji uhalali wa kisheria kwa rais alieapishwa,itakuwa anajipunguzia hadhi miongoni mwa wasomi wenzie,kazi kawaachia Sefu na Lowassa
 
Alimpa Dr Shein miezi 6 ya kuongoza baada ya uchafuzi wa 25 March 2016. Alimuahidi Dr Shein private jet kama atavuka miezi sita ya uongozi wake. Yuko kwenye count down!
 
Baada ya uchaguzi mkuu, aliibuka mwanasheria machachari alikuwa akichambua vifungu vya sheria na katiba ya nchi kwa utaalamu mwingi dhidi ya serikali ya CCM. Lakini cha ajabu tangu uchaguzi wa marudio ufanyike na Shein kupitia CCM kutangazwa mshindi huyu binti Karume haonekani tena wala kusikika kwenye vyombo vya habari.

Wadau mwenye kufahamu alipo atujulishe na kwanini yupo kimya wakati mapambano bado yanaendelea!
Baba yake mdogo Balozi Ali Karume ameteuliwa na Dr Shein kuwa Waziri wa mawasiliano. Lazima Fatuma aufyate sasa hivi. Na Serikali ya Zanzibar anaitambua!
 
CCM mnajipa moyo hapa tu, kinachoendelea Zanzibar na Kwenye ulingo wa siasa kimataifa najua mnatamaani kiwe ndoto na sio ukweli.
Sasa hivi mmefunga macho mkijiaminisha wakati wa kuyafungua moto utakuwa umezima, hauzimi!
 
Fatma karume alisahau kama urais sio dr. Shei pekee isipokuwa urais ni taasisi kubwa sana kuliko alivyokuwa anafikiria.

Nahisi atakuwa ameungana na mnyika tangu alipomtusi Jk naye kapotea katika game, kweli huu mchezo hauhitaji hasira wala kupayuka payuka.
 
CCM mnajipa moyo hapa tu, kinachoendelea Zanzibar na Kwenye ulingo wa siasa kimataifa najua mnatamaani kiwe ndoto na sio ukweli.
Sasa hivi mmefunga macho mkijiaminisha wakati wa kuyafungua moto utakuwa umezima, hauzimi!
Ndio kipindi hiki tulihitaji mchango kuliko wakati wowote!
 
Back
Top Bottom