UFAFANUZI.1/Nadhani unamaanisha Dr.Ferdinand Masao ambaye kwa sasa ni marehemu. 2/Fitna, Chuki, Mizengwe dhidi yake kutoka kwa Baadhi ya Watanzania wakiwemo Madaktari, Maafisa wa wizara ya Afya, viongozi kadhaa kutoka serikali ndiyo vilichangia sana Dr.Masao kufariki. Stress za maisha akipambana kutaka kufanikisha ndoto zake zilipelekea kuugua na kufariki. Alikuwa na ndoto njema sana na pana sana kwa Tanzania, hakuwahi kukata tamaa kabisa.3/Hakuwahi kuwatendea ubaya wowote watanzania, alitumia Muda wake, Utaalamu wake, Kipaji chake na Juhudi zake binafsi katika kuanzisha Hospitali ya kutibu na upasuaji wa moyo ili huduma hiyo iwepo nchini na watu wasiendelee kupelekwa nje, Lakini alichokumbana nacho, kinatia huzuni sana. Alifanyiwa kila aina ya Fitna, alikosa watu wakumtetea, alisakamwa mpaka basi.4/Kiukweli kabisa, Tanzania tumeitupa Lulu ya thamani sana, Dr.Masao alikuwa ni lulu tena lulu ya thamani sana. Katika hili laana iko juu ya nchi yetu. Mbegu ya Fitna tuliyoipandikiza itatutafuna mpaka basi. Kila mtaalamu atakayeibuka hapa Tanzania atapigwa vita vibaya sana. Usishangae ya Dr.Mwaka kupigwa vita badala ya kusaidiwa kusonga mbele. Ni mwendelezo ule ule.