Nini kilikuwa kinakusukuma uende shule?

Nini kilikuwa kinakusukuma uende shule?

EJM_

JF-Expert Member
Joined
Jul 8, 2011
Posts
3,836
Reaction score
2,108
Watoto wengi wanapokuwa shule za msingi huwa hawapendi kwenda shule. Mara nyingi hii inachangiwa na tatizo la kuamka asubuhi wakati bado ana usingizi au kubanwa kwa muda mrefu wakati anataka kucheza.

Sasa hebu we kumbuka nini hasa kilikuwa kinakufanya uende shule kila siku pamoja na kwamba ilikuwa inakukera sana kuamka asubuhi?
 
nilikuwa napenda sana kwenda shule
sababu nilikuwa sipendi mno kazi ya kuosha vyombo
 
nilikuwa napenda sana kwenda shule
sababu nilikuwa sipendi mno kazi ya kuosha vyombo
Hahahahahaaa haya siku hizi hupendi kufanya kazi gani na unai substitute na nini?
 
Nilikuwa sipendi kwenda shambani..... :hat:
 
Dingi ndio alikuwa ananifanya niende shule,nisipoenda ni balaa!
 
hadi kesho sipendi kuosha vyombo
bora nikamue ng'ombe
Vyombo vilikufanya nini wewe mpaka unavichukia hivyo? Wakati unaanza maisha nani alikuwa anakuoshea?
 
Dingi ndio alikuwa ananifanya niende shule,nisipoenda ni balaa!
Vipi dingi alikuwa akisafiri au kenda likizo home inakuwa sherehe na burudani eeh?
 
yaani nilianza kuosha vyombo nikiwa mimba
nikavichukia for good!

Kama hamna wa kumtegea naosha, ila kama kuna mtu mwingine sioshi vyombo hata kwa fimbo
Vyombo vilikufanya nini wewe mpaka unavichukia hivyo? Wakati unaanza maisha nani alikuwa anakuoshea?
 
usinikumbushe
mdingi alikuwa mkolono kama nini
siku akijisikia anakushtukiza na chemsha bongo

zile table za nyuma ya daftari nilizishika mapema mno sababu yake

dah! Ila ilinifanya nkapenda hethabu
Dingi ndio alikuwa ananifanya niende shule,nisipoenda ni balaa!
 
Mi kwa kweli zilikuwa ni fimbo za babu Kaiwanga huyu mwalimu babu alikuwa anachapa na makonzi kwa sana yani hata nikiwa na usingizi kiasi gani nikimuwaza tu huyoo mwenyewe naenda shule
 
Mi kwa kweli zilikuwa ni fimbo za babu Kaiwanga huyu mwalimu babu alikuwa anachapa na makonzi kwa sana yani hata nikiwa na usingizi kiasi gani nikimuwaza tu huyoo mwenyewe naenda shule
Hahahaha kwahiyo wakati wa likizo ulikuwa unafanya sherehe eeh?
 
usinikumbushe
mdingi alikuwa mkolono kama nini
siku akijisikia anakushtukiza na chemsha bongo

zile table za nyuma ya daftari nilizishika mapema mno sababu yake

dah! Ila ilinifanya nkapenda hethabu
Kama nakuona vile unaosha vyombo huku unalia mpaka leo.....

Dah halafu table ngumu ilikuwa ya 7 na ya 9 kwahiyo unauliza hizo kila ukipigwa maswali
 
Visichana virembo,we acha tuuu.Hasa kakiwa kageni shuleni ni balaa.
 
Unapokua na kukuta watoto wa rika lako wanaenda shule lazma na wewe utamani. Wakati huo, nilikuwa nacheza sana mpira wa miguu na hicho ndicho kilikuwa kinanifanya nisikose shule. Mpira asubuhi kabla ya kwenda mstarini, mpira mapumziko, mpira wakati wa kutoka.
 
Visichana virembo,we acha tuuu.Hasa kakiwa kageni shuleni ni balaa.
Dah believe me pamoja na mambo meeengi lakini hili lilikuwa mojawapo la yaliyokuwa yananifanya niende shule, yaani nikiwaona tu darasani roho yangu inasuuzika
 
Back
Top Bottom