Slim5
JF-Expert Member
- Jan 7, 2014
- 28,440
- 38,437
Habari za jioni wana-JF!
Ndugu yangu anapitia kipindi kigumu sana wakati huu. Ana mke, ndoa ina miaka 11. Wana nyumba yao kihonda, morogoro na wanaishi huko, watoto 2! Shemeji kachachamaa, anataka waachane, kaanzisha timbwili hili hii wk ya pili sasa, hapiki hapakui! hana salamu hana jehanamu! kitanda kila mtu chake, ndg yangu anasema hakumbuki mara ya mwisho kupewa papuchi ilikuwa lini, ndg yangu anavumilia tu! Leo shemeji yangu kamtumia sms ndugu yangu, amemwambia kama hataki kutoa talaka kwa hiyari, basi ataitolea mahakamani!
Ndugu yangu kavurugwa. Kwanza shemu ni mzuri. Pili ndugu yangu kafulia, hana kazi tangu January (hii imechangia shem kupagawa), tatu ndugu yangu hajui hatima ya watoto wake (anawapenda sana)! Anavoumia ndg yangu ndio ninavoumia mimi, nimemuomba ndg yangu aje dsm (nikiamini distance na mkewe inaweza kumpa relief), aje tukae na kufikiria, labda nikimtafutia na kibarua inaweza kuwa ahueni, sasa hivi hapa shem katoa mpya: "kabla hujaenda dsm, kwanza tumalizane kabisa, nipe talaka yangu ndio usepe, ole wako uondoke bila ya kumalizana na mimi, utajuta maishani kwa nitakachokufanyia!"
Ndugu yangu ilikuwa nimpokee leo Dsm, ameshindwa kuja kutokana na maneno makali ya shemu. Kwa maelezo ya ndg yangu anasema chanzo cha shem kupagawa ni 1. ugumu wa maisha! 2. kaibeba dunia na dunia inambeba (nimeambiwa alimuanzishia biashara ya saloon, huko akakutana na mashangingi ya mjini, yakamuonyesha dunia, shemu sasa hashikiki!)
Mwenye mchango ama fikra, mimi na ndg yng msimamo wetu ni ndoa hii iendelee!