TinyMonster
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 242
- 154
Ni wizara muhimu sana katika nchi kama ingekuwa ni timu ya mpira tungesema ndio namba 6, maana ukivuruga viwanda na biashara wizara nyingine na taasisi za serikali haziwezi kujiendesha kutokana na ukweli kwamba makusanyo ya kodi yakikwama kutokana na biashara kutokuwa nzuri uchumi unayumba.
Ni mara ya tatu JPM anabadili waziri, lakini nini hasa ni tatizo? Waziri mpya Bwana Bashungwa ambaye nae ni mwanajamvi mwenzetu hapa JF anatakiwa afahamu na kubadili kitu gani?
Ni mara ya tatu JPM anabadili waziri, lakini nini hasa ni tatizo? Waziri mpya Bwana Bashungwa ambaye nae ni mwanajamvi mwenzetu hapa JF anatakiwa afahamu na kubadili kitu gani?