Heshima kwenu wakuu wa jukwaa hili.
Mi si mtaalam wa IT japo nina idea kidigo.
naomba kufahamishwa kazi za hivyo vitu kwenye computer...
kwa mfano kwa processor zipo za aina ngapi au zipi ni nzuri zaidi au zina uwezo mkubwa?
hivyo hivyo na RAM na Hard Disk...
asante sana Watu8 na Chief-Mkwawa ... sasa nilifungua CPU ya desktop hapa ndani ina RAM mbili, sasa nauliza ni nini faida ya RAM kuwa mbili?
na je naweza kuongeza nyingine maana naona ni kama kuna sehemu ya kuongeza nyingine
Inategemea na aina ya processor kama Ni dual chanell inasaidia kuongeza speed.
Kama ulivyoona juu kazi ya ram Ni kuhifadhi mafile ya program zinazotumika inamaana kuna mafile mengi sana yanayoingia na kutoka kwenye ram hivyo jinsi ram inavyokuwa na speed ndio kazi zinavyofanyika upesi
Unapokuwa na slot mbili za ram na processor/motherboard inayosuport dual chanell inamaana processor itawasiliana na ram zote mbili kwa mpigo hivyo kazi itafanyika upes upesi.
Pia kuna motherboard Ina slot hadi 4.
Slot zinapokuwa nyingi Ni faida pia kwa power user wanaohitaji ram kubwa kama 32gb (ddr3) na 512gb kwa ddr4 sababu hakuna single ram ya 512gb ILA zipo za 128gb ambazo ukiunganisha 4 ndio unapata 512gb
Ndio unaweza ongeza ram mwenyewe
asante mkuu... naomba usichoke maswali yangu nataka kujifunza.
Tuje kwenye internal battery ya computer desktop, je ni nini hasa huwa kinafanya uwahi kuharibika(kuisha nguvu) au kwa kawaida huwa inachukua mda gani mpaka iishe nguvu?
Internal battery za desktop Ni zipi? Au unamaanisha kile kibattery kama cha saa kinachoitwa CMOS
ndio mkuu... maana hapa PC ilikuwa inalose kumbukumbu za saa na tarehe kila siku... nimeweka battery mpya naona iko poa....
sasa najiuliza ni nini kilifanya battery ife mapema? hii PC ninayo karibu miaka mi5 sasa au ndio kawaida kwa huo mda kuharibika?
HDD ikiwa ni kifupisho cha Hard Disk Drive ni kifaa kitumiwacho na kompyuta kuhifadhi operating system, programu pamoja na makabrasha yote yatumiwayo ama na kompyuta au mtumiaji kompyuta.
Kinachohifadhiwa katika HDD huendelea kuwepo hata kama kompyuta imezimwa, kabrasha limefutwa n.k, kumbukumbu hii ni ya kudumu.
Kama ilivyo kwa RAM, HDD nayo huwa na sifa ya kuwa na memory size, processing speed etc
Yah huwa inakaa miaka around 3 hadi 5 ILA inaweza kuzidisha hapo Ni kawaida tu.
HDD ni kama MMEMORY CARD
Local disk inaweza kuwa majina ya hard disk au majina ya partition za hard disk.
-ukiwa na hdd moja uneifanyia partition na kuwa na sehemu mbili basi itaitwa local disk c na d
-ukiwa na hdd mbili pia zitaitwa hivyo hivyo c na d.
Haya Ni majina tu unaweza ukarename ukaziita panya, kuku, sungura au jina unalolitakawa wewe.
Cha muhimu zaidi Ni alama ya windows IPO local disk ipi hio ndio inaonesha windows yako mahala ilipoekwa na disk hio ndio ukiinstall software by default zitakaa hapo hadi uzihamishe kwenda kwengine.
Angalia hii picha jamaa Ana disk nyingi na windows kaeka D.
nimeelewa mkuu... kwa hiyo hata nikichukua files za kwenye disk C nikihamishia D hakuna tatizo ?? maana nina Hard disk moja na imefanyiwa partition kuweka C na D