Wakati tunaelekea katika uchaguzi dalili zinaonyesha kuwa kama vyama vya upinzani havijawa makini na kuweza kuja na ajenda ambayo itawawezesha kuaminiana na pia kujenga imani kwa wapiga kura basi kuna hatari ya upinzani hasa kwa upande wa Tanzania bara kuwa extinct.
Vyama vya upinzani na haswa CHADEMA vilikuwa na kila dalili ya kuweza kupata viti vingi vya ubunge na udiwani zaidi ya miaka ya nyuma hadi miezi ya hivi karibuni ambapo hali inaonyesha kuwa imegeuka kabisa.
Yapo mengi yametokea lakini iongoni mwa makubwa ni lile la ubabe wa CHADEMA kumzima mwanasiasa machahcri na mwenye mvuto kuliko wote nchini Zitto Kabwe kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chake na pia kuishiwa nguvu kwa hoja ya UFISADI ambayo mwishowe ilikuja kutekwa na kundi la wajanja wa CCM.
Mimi binafsi nawajua wapiga kura wengi tu wakiwemo vijana mbalimbali ambao sio tu walikuwa wameshaamua kupeleka nguvu zao vyuma ya vyama vya upinzani na haswa CHADEMA lakini pia walikuwa tayari wako katika mikakati ya kusimama katika uchaguzi kupitia vyama hivyo. Wengi wao walikuwa ni wasomi na wenye muamko wa hali ya juu. Hivi sasa wengi wao ama wameamua kuachana na siasa ama kujiunga na CCM.
Hali ni mbaya kiasi ya kwamba yawezekana kabisa bunge lijalo likawa na wabunge kichache zaidi kutoka upinzani. Kitakachookoa ni wabunge wa CUF tu kutoka Zanzibar ambao wao wanafaidika na siasa za historia na mgawanyiko wa kijamii bila ya kujali utendaji wa wanaochagua.
Swali linakuja, NINI KIFANYIKE KUOKOA DEMOKRASI YETU AMBAYO BADO IPO KATIKA NGAZI ZA KUTAMBAA LAKINI INA UMUHIMU MKUBWA KWA UJENZI WA TAIFA LETU?
Kwa maoni yangu ni kuwa;
1. Suala la kuungana vyama vya upinzani sio suala la kupenda bali ni suala la kufa na kupona.
2. Vyama vya upinzani vinapaswa kuja na ajenda ambayo inatofautiana na ya kila siku ya kuleta maendeleo. Mfano ni ajenda ya kufanya mabadiliko ya kimfumo yatakayohusisha watanzania wote yatakayoishia katika kupata katiba mpya ambayo ndio itatumika katika uchaguzi ujao ambao unaweza kufanyika katika kipindi cha miaka miwili - mitatu - minne. Kwa hali ilivyo katika vyama vya upinzani ni vigumu kwa watanzania kuamini kuwa wanaweza kufanya vizuri katika ajenda ya MAENDELEO tofauti na ifanyavyo CCM.
3. Kusimamisha watu wapya kabisa katika siasa za urais lakini wana heshima isiyotia shaka miongoni mwa watanzania ambao wataaminika kupewa jukumu la kuijenga upya Tanzania na kuondoka madarakani mara baada ya kipindi kimoja tu cha uongozi.
4. Kuunda serikali ya mseto ambayo ajenda yake itakuwa ni kuhakikisha political reform kwa kipindi kichache na hawa watatoka katika vyama vyote wakiwemo wa CCM.
Ni imani yangu kuwa wakichukua baadhi ya haya bila ya kuacha la wao kuungana kuanzia ngazi ya urais hadi udiwani na hata kutumia chama kimoja kusimamisha wagombea urais watakaoaminika na vyama vyao hata kama hawatakuwa miongoni mwa wanachama wao, basi sio tu wanaweza kuokoa siasa za demokrasia ya vyama vingi lakini hata kujenga upinzani madhubuti wenye kuonge na kusikika.
Kama hawatafanya hivyo, basi tujiandae kuzika upinzani na kuacha njia ya MAFISADI kushika hatamu hapo mwaka 2015 kama ambavyo wanavyojipanga sasa.
Na wengine tuzikumbuke kadi zetu za TANU
Nakaribisha mjadala