Nini huwa sababu ya Penzi kuisha ghafla ama kuwa chungu?

mmmuhumba

JF-Expert Member
Nov 8, 2017
491
476
Mapenzi uumiza, ushawahi jiuliza inakuwaje amani imetawala, bata unazila, mapenzi yamenoga alafu ghafla mpenzio/mwenza wako anakuambia "mimi na wewe basi".

Zipo sababu za kujifunza kuyaepuka haya na pia kuwa tayari kuyapokea mapya usiyo yatarajia kwenye mapenzi.

1. Uoga wa maisha.
Mpenzi/ mwenza aliye na uoga wa maisha, uona mtu aliye naye ni mzigo. Uona ni bora awe pekeake aya mudu maisha na wengine uona bora awe pekeake ili aweze kuwa huru na wengine aonao wanaweza mpa mahitaji.

2. Kuiga maisha ndani ya mapenzi.
Kuna kundi, wao kama wao hawawezi kuishi kwa mtindo wao wa mahusiano. Fikra zao utawaliwa na kutaka mengi wasiyo nayo kihisia, kivitendo na kiuchumi ila utaka yatokee kwao. Kwa hii kila anapomtazama mwenzie uona kama atendewi haki, uona mwenzio anapungufu, hivyo kuondoka ni suluhu kwake.

3. Kupenda kumuwekea vipimo vya mapenzi mwenzio. Vipimo siri shida ila vinapozidi uzaa kukinai penzi, wapo watu wanapenda kumuendesha mtu, na mtu huyo akavumilia sana kwa kutenda vile utakavyo, kipindi wewe unafurahia na kuhisi pia anakufurahia, kumbe mwenzio anaumia na anavumilia. Ghafla, anaamua kuutua mzigo wake wa uvumilivu na kwenda.

4. Kuvumilia kupita kiasi.
Uvumilivu upo lakini unaleta matumaini ikiwa mwenzio anaonyesha juhudi katika gumu lolote. Kuna watu hawataki na uchi zao, hawataki na muda wao, hawataki na pesa zao, hawataki hata kupambana na hali zao. Mvumilivu ufika ukomo na kuamua kwenda kupambana nje ya wewe.

5. Ubinafsi.
Kuna watu wapo ni kama pochi, kazi yao ni kupokea tu siyo wanaume siyo wanawake, ni wachoyo kwa wapenzi wao. Chake ni chake ila chako ni chake, hamuwezi kuwekeza chochote pamoja iwe kwa kingi wala kidogo. Na hata mkiwekeza anataka kikae mahali pake.

6. Mtu kuishi nje ya jinsia yake.
Kuna watu wanapenda kukumbushwa kila mara majukumu yao, hii ukela, eti una mume alafu unaumwa nyege, una mke alafu unaumwa nyege ni tatizo, una mpenzi/mwenza na kwake unakuwa omba omba, kila kitu mpaka uombe, yeye hawezi kujiongeza ni shida. Kuna watu hawafanani na jinsia zao na hawataki kuwajibika kwa jinsia zako.

7. Maono ya familia na ndoto za maisha.
Unaweza pata mtu ajuaye mapenzi, ila hana mapenzi na familia yako na hana mtazamo juu ya maisha ya leo na kesho. Kuna watu ni matajiri ila utajiri wao ni siri yao, akifa anayemuacha hata pakuanzia hana na kuna watu maskini ili hawana hofu na maisha, uishi kama ndege na bora hata ndege wanakumbuka ; watu mahakama yao ni watu, maamuzi yao ni watu na njia yao sahihi ya kupata habari ni watu. Maisha yao yametawaliwa na masikio ya majungu ya wapenzi wao.

8. Mfumo dume na mfumo jike.
Hawa watu ni pasua vichwa, ashakumu! siyo matusi ila ukiwa na mwanamke mbuzi na mwanaume mbuzi ni kama upo gerezani tena gereza la mateso. Kuliacha penzi siyo ajabu, utakubali kuwa mtumwa wake ila mwisho wa siku ukipata pa kutokea, unapotea mazima.

9. Kuishi kwa kusikiliza sana watu.
Kuna watu mahakama yao ni watu, maamuzi yao ni watu na njia yao sahihi ya kupata habari ni watu. Maisha yao yametawaliwa na masikio ya majungu ya wapenzi wao. Imani kwa wapenzi wao ni kutoka kwa watu na siyo wao wenyewe. Uishi kama bendera, kuvunja moyo wa wenzao ni rahisi na uishi kwa majuto wanapopoteza wanapoujua ukweli baadae.

10. Kutobadilika maisha yako ya anguko. Kuna mapenzi ni matamu, ila anapokukosea kosa lake hata kama ni mara moja kwa mwaka, ila uwa ni kosa lile lile. Hii ufuta yote mema uliyotendewa na mwenzio. Ni bora ufanye kosa jipya, utaeleweka ila lile lile uchukiza na kuona mbele kuna kubwa zaidi laja ama wewe hujali kuhusu yeye na anafanya sana ila tu kwa siri.

Mapenzi huwa haya mwangaza wa moja kwa moja ila kuyatambua mapunguzu machache ni kujiimarisha kimawazo.
#imarika
Na mmmuhumba.
textgram_1688851494.jpg
 
Vijana wa kiume acheni kutimiza majukumu ya mume kwa girlfriends zenu (wanawake ambao hamjawaoa)

Ni kupoteza muda na pesa zenu

Mwanamke wa kumtunza na kumhudumia ni mke tu
 
Back
Top Bottom