Nini husababisha mume kumchukia mkewe Kipindi cha Ujauzito?

Anna pita

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
227
425
Watalaam nisaidieni hapa hivi huwa kinatokea nini mwanamme mkuchukia mkewe kipindi cha ujauzito?

Yaani hii imekaaje kitalaam. Unakuta walikua wanaishi vizuri tu before ila baada kupata ujauzito tu mume hana shida na mke yani

Kuna kesi hapa mume kasafiri kikazi wiki nzima hata kupiga simu kumjulia hali mama K wake hamna...

Juz karudi kakuta mkewe hoi na Malaria jioni kasafiri mpaka leo asubuh hajui mkewe anaendeleaje Wala nini na hawana ugomvi
Ni mimba tu imemchukia wife

Hivi hii kitalaam inakuaje?
 
Huyo mume hajitambui na inawezekana ana mchepuko unamsumbua...wanaume wa hivyo ni wale wapenda ngono kupita kiasi, hivyo inawezekana mkewe sababu ya misukosuko ya ujauzito hampi penzi ipasavyo.... Hivyo jamaa kaona jibu ni kusepa...
 
Inatokeaga kwa asilimia chache Sana

Mke anabeba ujauzito ila dalili anazipata mume hasa za kisaikolojia

Nadhani telepathy inahusika ila sijajua kiundani
 
Hakuna wanaume wa hivyo.Wanaume wake zetu wakibeba mimba huwa tunafurahi na kuwapenda zaidi.Hiyo unayozungumzia wewe ni mental case!

Kweli kabisa mkuu me wangu nampenda hatari kila muda nko nae, uyo jamaa hajielewi ndomana watoto wakizaliwa hawana upendo kwa baba kwa mambo kama haya
 
Inatokeaga tu kama vile mwanamke amchukiavyo mwanaume au kupenda kunusa boxer ilivyovuliwa baada ya kuwa mwilini week nzima
 
Hakuna kipindi kitamu kama kipindi cha mke mjamzito. Tumichezo michezo, kudekadeka na ana joto acha. Hapo bado mtoto hajakick ukawa unasikiliza.
 
Hii kitaalamu tunaita technical default misbehaviour. Kwako mwalimu kashashaa
 
Mke wangu mjamzito hataki hata kuniona yaani vurugu mechi. Nakumbuka kabla sijajua ni mjamzito nilikuwa Nikila kitu chochote lazima kirudi full kichefuchefu. Yaani hata nikimgusa napewa shit moja takatifu. Yaani akiniona anasema sijui umekuja kufanya nn bora ungebaki hukohuko. ananichukia balaa. Hizi mimba shida tupu. Hadi baba mkwe ananiambia vumilia tu ni mimba hiyo .
 
Hakuna kipindi kitamu kama kipindi cha mke mjamzito. Tumichezo michezo, kudekadeka na ana joto acha. Hapo bado mtoto hajakick ukawa unasikiliza.
Hahaha kimenipitia sahv kashajifungua nipo nalea kababy
 
Mke wangu mjamzito hataki hata kuniona yaani vurugu mechi. Nakumbuka kabla sijajua ni mjamzito nilikuwa Nikila kitu chochote lazima kirudi full kichefuchefu. Yaani hata nikimgusa napewa shit moja takatifu. Yaani akiniona anasema sijui umekuja kufanya nn bora ungebaki hukohuko. ananichukia balaa. Hizi mimba shida tupu. Hadi baba mkwe ananiambia vumilia tu ni mimba hiyo .
Jiandaeni mtoto wa kiume huyo.
 
Kuna mengi yamejificha hapo yamkini hio mimba imetokana na kiherehere cha mwanamke. Mme hakuwa na mpango wa kupata mtoti kwa mda huo alafu mwanamke kamtegeshea makusudi ili apatea mimba.

Najaribu kuwaza tu kwa maandishi.
 
Huyo mume hajitambui na inawezekana ana mchepuko unamsumbua...wanaume wa hivyo ni wale wapenda ngono kupita kiasi, hivyo inawezekana mkewe sababu ya misukosuko ya ujauzito hampi penzi ipasavyo.... Hivyo jamaa kaona jibu ni kusepa...
Kabisa mkuu.

Walioa kwa sababu ya ngono na umbile la mwanamke pekee,sasa ana mimba hayo yote yanapotea unabaki huna cha kubakia nae kikakufurahisha
 
Zoefu zote nilizonazo, huwa ni kinyume cha huu uzi. Sijawahi kusikia mume anamchukia mkewe mjamzito!
 
Back
Top Bottom