Nini cha kufanya ukimfumania mkeo redhanded huku bado unampenda!!!!!

lara 1

JF-Expert Member
Jun 10, 2012
15,700
29,111
Nawasalimu wadau wa JF!

Mimi ni mzima na wikiend nilikua gonjwagonjwa imelala kitandani, si mwajua dozi na maji ya dhahabu haviendani.

Back to the main topic, waungwana mliioa na kuolewa nawapa BIG UP kubwa sana kwa kuachana na uzinzi usio wa lazima (watu mnapendana alafu hamuoani kazi kuzini tu! na kuongeza msururu wa dhambi wakati wa kitubio), na nyie mabachelor kama mimi, kama mna wapenzi oaneni, uzee waja, na ambao hamjabahatika nawaombea kwa mola muwapate wenzenu.


Mimi sijaolewa, wala mtoto hata wa kusingiziwa sina, ila born town kitambo, na cha kushangaza ndugu zangu na marafiki zangu wengi sana walioolewa/kuoa na waliojipasishia watoto wa watu/waliojipeleka kwa waume zao, wanaifanya mimi comfidant wao sana kwa kunieleza mambo mazito ya ndoa zao, na mimi ni mshauri mkubwa sana kwao. Hii hali maza wangu haipendi kinoma, anadai itanifanya niogope ndoa, hivo akijua mtu ananiomba ushauri anaenda kumpashua, atafute mwanandoa mwenzie amshauri. utasikia "Kama huipendi ndoa yako we sikiliza ushauri wa huyu mtoto, yeye hata kumpata mtu amuweke ndani bado atakushauri nini?" Hajaishia hapo kapiga biti ukoo mzima no mtu kuniomba ushari. Na mimi tumekubaliana nikimshauri mtu tena tunakosana jumlajumla, nikamuahidi kazi ya mama ushauri mimi basi!

Kweli mimi nina moyo wa kuacha hii kazi! ila naipenda sana haswaa part ya kupata maumbea ya ndani kwa watu, si mnajua tena watu unaweza kuwaona wako perfect kinoma, wanakurusha rohooo, ila wakija kukuconsult mazito ya ndani mwao unabaki unaguna tu! Nikiacha hii kazi nitakosa uhondo!( sitangazi kwa mtu ila nafaidi mwenyewe tu umbea)

Baada ya kutoa ahadi ya kutokushauri mtu tena, jana usiku mida ya saa 4, Kaka yangu kabisa kabisa kanipigia simu kuwa kamfumania mkewe wa ndoa ya mwaka! Ishu yenyewe ilikuwa hivi, Bro kasafiri kikazi, sasa akamwambia mkewe anarudi leo jpili, afu wanaaminiana kinoma, sasa kazi zikawahi kuisha, hivo akaona arudi jmosi amuwahi mamsap na baby girl (2yrs) ila hakumwambia mkewe wala nini.

Kufika getini mlinzi kamtolea mijicho kama kabanwa na mlango, kumfokea ndo kafungua geti, akahisi kuna ishu lazima! Hausgeli nae hamwangalii machoni, mke hayupo, kumuulizia beki tatu anababaika mara kaenda dukani, mara kamsindikiza mgeni, ming u saa 7 hiyo. Akwaita beki tatu na mlinzi akawaambia waseme ukweli lasivo asubuhi kazi basi! Mlinzi akaanza kutiririka bwana mkeo kaondoka hii siku ya 4 hajalala hapa! Beki tatu anaulizwa kweli? Kimyaaa! Akachukua simu zao, akawaambia wakalale.

Saa tano leo jpili Wife karudi kwa mbwebwe, hapo kashatuma sms kwa beki tatu apike pilau Mr. anarudi. Ile kufika namkuta Mr. kwenye kochi, si ndo presha kupanda na kushuka! Mume kamtega niambie ukweli wote bila kuficha nitakusamehe manake najua hujalala siku 4! Wifi nae sijui uoga, sijui ubwege, sijui ushamba hata sielewi, si KAFUNGUKA A to z. Bila kupindisha ukweli wowote na kuomba msamaha dobledoble! Kamtaja hadi bwana wake, wana uhusiano toka lini, na mengine kibao yenye kumteketeza zaidi.! Bro kuzama kwenye pochi si ndo kakuta THE PILLS AFTER hizi ndo zile dawa kama umecheza kavukavu ndo unameza kabla ya 72 hrs hupati mimba. Hivo inaelekea wifi hakutumia kinga huko kwenye uasherati wake.( Can u imagine na ukimwi wote huu!)

Basi bro akamwambia we ondoka, nisije kukua bure! Akanipigia njoo haraka, nikamwambia mie naumwa mwenzio kwani vipi!? Kama huji utakuta kaka yako nimejinyonga na usije kwenye mazishi yangu! Mtumeeee! Nikakurupuka kwenda kwake ndo kunielezea A to Z na kutaka ushauri. Nikakumbuka moyoni nishamwambia Maza mi sishauri tena, ila nikabullshit nikasema huyu kaka yangu wacha nimshauri.

Nikamwambia kweli hayo mambo ya aibu bro, tena yataudhalilisha uume wako haswaa, ila nyie mna ndoa ya kanisani, na najua unampenda mkeo, pamoja na yote hasira tu ndo zimekubana, HUU NDO WAKATI WA KUWA MWANAUME HASWAA! Mtizame mwanao 2yrs only, sote binadamu, yeye kateleza ila kuvunja ndoa si sahihi, istoshe wanawake wote wanaksoro. Na kwanza hukumkuta bikra, so we kaza roho. We mtext arudi, usimuulize chochote, endelea kuishi nae kama zamani dhamira yake itamla itammaliza.
Nikamsisitiza hili jambo asimwambie yeyote, tuwe tunalijua watatu tu mimi, yeye na wifi. Sababu wakijua watu wengine alafu asipomuacha atajiaibisha zaidi tu. Akanielewa akamtext nikamuacha wifi karudi yamepo.

Jioni Maza kaanza kunipeleleza kuwa mbona kaenda kwa Bro hakueleweki, Kama kuna jambo na haambiwi! niknyuti mi sijui lolote! Akaninganganiza wewe watakuwa wamekuomba ushauri!, niambie mimi mzazi wenu ujue, sio vizuri, hata kama umeshauri pamoja na kukutaza sitokasirika niambie! Si ndo nikafunguka!

Weeeee! Najuuuta! Maza akapaniki, yaani unamshauri mwenzio alee uzinzi aje kufa na ngoma? Utanizalia mtoto mkubwa kama yule wewe? Hivi unaona aliyofanya wifi yako mazuri? Msinichezeee! Haiwezekani, huyo muasherati aondoke na mengine mengi!

Na wewe (mimi) nilikwambiaje kushauri watu? Kwanini hukumshauri aniambie mimi mzazi wake? Sasa kukukomoa nyie si mmefanya siri ya watu 3 nawaambia ndugu na marafiki woteee, afu nasema ni wewe ndo umeuza mkanda! Tena natahadharisha wewe ni mmbea mkubwa watu waskwambie tena mambo yao! Ndo dawa yako hii! Hapo kanipora simu yangu na kujifungia chumbani! Sijui atawatext au atapiga.

Kichwa kinaniuma! Natamani ardhi ipasuke! Bi mkubwa ndo kawa kama Mbogo! Nawaza watu walioniambia mambo yao mazitomazito wakisikia habari hizi toka kwa mzazi wangu kabisaaaaa! Sijui nitaweka wapi lisura langu! Maskini my bro! na my wifi( japo simpendi kama nini toka kitambo!)

HII INAITWA POINT OF NO RETURN AU NO WAY OUT! I AM WAITING FOR A MIRACLE!!!!
 
Refer to the heading.
Binafsi nikimfunania wife wangu redhanded kwa kuwa nampenda sana, sitomuua nitamtaliki bila kutoa uahai wake.
Kumwachia uhai wake ndiyo feva ambayo nitampa kwakuwa nampenda sana.
 
Yaani sitaki hata itokee nadhani sitakuwa na hamu nae teeeeeeeena, sababu mie sijawahi toka nje ya ndoa yangu seven yrs now!! Aisee mungu ataniusamehe tu hata km ni ndoa ya kanisani sitaweza kula tena ile kitu nikijua kuna mtu alitema cheche zake pale khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Kwa vile unampenda, wasiliana na Jeshi la Marekani ili wammalize kwa drone.

Utabaki na mapenzi yako na utakuwa umepata ufumbuzi/dawa ya wivu wako.

Kama hilo ni gumu, mrudishe ilikomtoa. Kama ulimpata baa, mrudishe baa uliyomuopoa. Kama kwa wazazi wake, warudishie ili wamfunze heshima na kusitiri nyeti zake.

Au "declare" open relationship!!!

Kama na wewe huwa unakosea siku nyingine (unaibia ibia) basi chukulia kuwa ngoma ni "draw". Wewe bahati yako huhitaji morning pills,ushahidi wa kuwa unaibia(unateleza, kufanya kosa, oh bahati mbaya...bla bla )
 
Yaani sitaki hata itokee nadhani sitakuwa na hamu nae teeeeeeeena, sababu mie sijawahi toka nje ya ndoa yangu seven yrs now!! Aisee mungu ataniusamehe tu hata km ni ndoa ya kanisani sitaweza kula tena ile kitu nikijua kuna mtu alitema cheche zake pale khaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Umsamehe tu! kwani ina shombo!?au mabaki yanabaki
 
Refer to the heading.
Binafsi nikimfunania wife wangu redhanded kwa kuwa nampenda sana, sitomuua nitamtaliki bila kutoa uahai wake.
Kumwachia uhai wake ndiyo feva ambayo nitampa kwakuwa nampenda sana.


Mimi nitamsamehe, kwa sharti kama alipitiwa asirudie tena. Ila sitamgeuzia shavu la pili kama YESU anavyotuasa!
 
Wewe watafute vijeba wamtigue huyo jamaa kwa zamu watu wakishuhudiwa. Atanyooka tu. Si anaupenda mchezo? Halafu anyweshwe uji huo.
 
Mimi nikimfumania mke wangu, kwa kuwa analea wanangu, nampotezea tu, namsamehe ila baada ya kumwonesha ni kwa kiasi gani ameniudhi.
 
Hahahahaha! lara 1 kiukweli nimekuvulia kofia.

Ni hilo tu kwa leo.
 
Last edited by a moderator:
umemshauri vyema kaka yako ila ungeongezea kumwambia asifanye nae hadi wakipima ngoma mara 2 zote
 
Mungu anisaidie yasinitokee, kwani naweza kumpiga mpaka afe kama siyo kuzimia...nafikiri hii ni siku ambayo sitaisahau na hataisahau.......Me ameniuzi kabisa, yani nimeuzika....APEWE LIKIZO KWANZA, HAIPENDEZI...MKE WANGU ANALALA NJE SIKU NNE? AMEDHAMIRIA KABISA
 
Hii kitu yako nimeisoma halafu inaonyesha japokuwa ulianza kwa kusema wewe huwa hutoi hizo siri za watu lakini ukweli ni kwamba wewe sio mshauri mzuri na unapenda sana umbea kujua matatizo ya watu halafu uyatangaze kama ulivyofanya kuja kuyatangaza hapa matatizo ya huyo bro wako. Pia Bi mkubwa wako ni kichwa sana, anajua weakness yako hiyo, akaamua kukukataza na alijua ww ni mgombanishi na muuaji, kama ni mimi nisingeweza kumshauri bro wangu aendelee kuishi na muasherati wa aina hiyo, ulivyoanza kuandika uliwashauri watu waoe/waoane ili kuepuka uzinzi halafu tena umemshauri bro wako aendelee kuishi na huyo mzinzi sasa ndo nini? Ushauri wangu kwako ni kwamba usiwe unapenda kujiingiza na kutoa ushauri wa matatizo serious kama hayo kwa wanandoa au wapenzi maana mwisho wa siku lazima wewe uje kuonekana mbaya na tabia yako ya umbea siyo nzuri kijana.
 
Umsamehe tu! kwani ina shombo!?au mabaki yanabaki
Shombo si ndio kawaida yake ile kitu..............lazima wanawake mtasema hayo maneno kuwa asamehewe na hii inaonyesha wazi kuwa michezo hii ndo desturi yenu wengi wenu. Mnataka amsamehe ili baadae aje kumuuwa kwa ukimwi ndo mtafurahi, huyo mwanamke ni kicheche na hawezi kubadili hiyo tabia labda abadilishe mbinu ya kugongwa nje lakini sio kuacha kabisa.
 
Back
Top Bottom