Nini Hukumu Ya Viongozi Mafisadi

Sindbad

Member
Oct 12, 2006
7
0Watanzania wenzangu haya matatizo ua Ufisadi wa viongozi nchini mimi naona kwanza iwepo tume maalimu kuchunguz tuhuma hizo nzito na mkosaji mambo haya yachukuliwe.

1.Kusimamishwa kazi mara moja.

2.Kutaifishwa kabisa mali zote waloiba.

3.Kuhukumiwa adhabu kali sana na kua fundisho kwa wengine.

4.Kuhakikisha hawapati wadhifa wowote tena.

Cheo ni dhamana na wala sio kitu binafsi!
 
Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
225
Na hivi jamani, naomba mnikumbushe au mnijuvye, kati ya hawa "mafisadi watarajiwa" waliomtishia Dr Slaa na wenzake kuwa watakwenda mahakamani, kuna yeyote aliyethubutu kufanya kweli?
 
Atanaye

Senior Member
Oct 31, 2007
153
195
Watanzania wenzangu haya matatizo ua Ufisadi wa viongozi nchini mimi naona kwanza iwepo tume maalimu kuchunguz tuhuma hizo nzito na mkosaji mambo haya yachukuliwe.

1.Kusimamishwa kazi mara moja.

2.Kutaifishwa kabisa mali zote waloiba.

3.Kuhukumiwa adhabu kali sana na kua fundisho kwa wengine.

4.Kuhakikisha hawapati wadhifa wowote tena.

Cheo ni dhamana na wala sio kitu binafsi!

Nafikiri ulitaka kusema tume ya kutunga sheria za watakaopatikana na ufisadi! Tusaidiane

Matatizo yaneleweka, yanafanyiwa uchunguzi-Sheria zipo nakama watakuwa ni wakosaji sheria itaongea!
Naongeza....
Ni swali zuri lakini nafikiri ufumbuzi ulikuwa nao. Swali ni sheria gani itumike kwa hao watakaopatikana nu hujumu hizo?
 
Atanaye

Senior Member
Oct 31, 2007
153
195
Haya nafikiri yameshawahi kujadiliwa humu! Nafikiri wana JF wengi humu wanasisitiza kuwepo na ustawi wa mambo yanayo wagusa watanzania, na mimi nakubali, kwa sababu haya ya ufisadi sasa si news! Changamoto ni nyingi.
Pia nafikiri kuwepo angalau ka wiki kamoja kila mwezi ambao wana JF watachangia kwa umahiri mambo endelevu yote kutoka Utamaduni mpaka Siasa.
Kuwepo na category zote kama maazimio ya biashara na hata vyama vya siasa(maazimio yenye malengo ya kukuza Utamaduni na Siasa na n.k),jinsi ya kukwepa yale yaliyotokea muhimbili,municipal planning,reverse engineering(what is possible?), water shoratge(tuna bahari, na ma-ziwa), tunawezaje kutumia tekelinalokujia la sasa kubadilisha maji chumvi, utumiaji wa mionzi ya jua kwa ajili ya umeme sehemu zilizo mbali na miji au vijiji na kadha wa kadha...kama wana JF wanavyosema!

Changamoto Tanzania ni kabambe!! Siasa tuwaachie waliopo ulingoni na sisi tuwaachie changamoto kabambe kwa kuwa Mavisionary!! wana Vision mpo?
 
KakindoMaster

JF-Expert Member
Dec 5, 2006
1,357
1,225
Na hivi jamani, naomba mnikumbushe au mnijuvye, kati ya hawa "mafisadi watarajiwa" waliomtishia Dr Slaa na wenzake kuwa watakwenda mahakamani, kuna yeyote aliyethubutu kufanya kweli?

Mkuu Mbalamwezi

Hizo huwa ni njama za mafisadi kuweza kupunguza kasi ya mada fulani.

Sasa hivi wanapumua, na wanaendelea kuomba/kutambika upepo upite mbali sana.

Na kwa sababu watanzania huwa wanasahau hawa hawatazungumzia tena suala hilo.
 
Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
225
Mkuu Mbalamwezi

Hizo huwa ni njama za mafisadi kuweza kupunguza kasi ya mada fulani.

Sasa hivi wanapumua, na wanaendelea kuomba/kutambika upepo upite mbali sana.

Na kwa sababu watanzania huwa wanasahau hawa hawatazungumzia tena suala hilo.

Nadhani kwa waandishi makini, hili suala la kuchelewa kumshitaki au kuacha kabisa kumshtaki Dr Slaa & The Gang ni stori kubwa itakayoendeleza moto kwa hawa wala nchi.

Wataalam wetu mu i pick hii as a news idea, muwaulize walipiga mkwara wa kwenda mahakamani wamefikia wapi sasa?
 
DAR si LAMU

JF-Expert Member
Mar 31, 2007
2,929
1,500
..yawezekana wanaandaa kesi moja,mbili au tatu kabambe,ambazo zitakuwa foolproof!na maandalizi kama hayo huchukua muda!

..ila,kimya hiki kina maana sana!deal ni kuing'amua!
 
Mbalamwezi

JF-Expert Member
Sep 30, 2007
800
225
..yawezekana wanaandaa kesi moja,mbili au tatu kabambe,ambazo zitakuwa foolproof!na maandalizi kama hayo huchukua muda!

..ila,kimya hiki kina maana sana!deal ni kuing'amua!

Mhh! Inawezekana...how long does it take for a competent lawyer to (manufacture?) a case? these thugs have all the money they need for this job!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom