Nini hubadilisha mzunguko wa hedhi?

Anapata damu ya hedhi kwa siku tano lakini mwezi huu kapata siku tatu kuanzia tarehe 28,29,30 hapa alipo hana amani anahisi labda tatizo inaweza kuwa nini?

Sababu hasa, hajawahi kutumia dawa za uzazi ni hayo tu naombeni mawazo, ushauri na uzoefu wenu.
 
Pole, me mke wangu hapati siku zake karibu miaka mwili sasa, na bado hatujapata mtoto, nishahisi majanga katika family yangu. Vipimo vinaonesha anapungukiwa hormone ya estrogen. Yani ht sijui nini hatma yake. Nisaidieni tu wataalam
 
sababu nini labda

kuna my friend anatokwa hedhi mfululizo zaidi ya wiki, kaambiwa ni hiyo hormonal imbalance, madhara yake ni nini ? tiba yake je?

Sijui kivile, ila hata stress tu zinasababisha hormonal imbalance, najua Vidonge vya uzazi wa mpango huwa vinasaidia kuweka hali sawa...ila kwa uhakika na ushauri wa kitaalamu mtu mwenye hiyo shida aende hospitali
 
Pole, me mke wangu hapati siku zake karibu miaka mwili sasa, na bado hatujapata mtoto, nishahisi majanga katika family yangu. Vipimo vinaonesha anapungukiwa hormone ya estrogen. Yani ht sijui nini hatma yake. Nisaidieni tu wataalam

Hospitali mmeshauriwaje?
 
Stress kutokula vizur hata mpangilio wake WA vyakula auangalie ukoje ILA Sana stress kuchoka kupita maelezo mwisho hospital wataambia nn cha kufanya Hua zinakua sawa
 
Pole, me mke wangu hapati siku zake karibu miaka mwili sasa, na bado hatujapata mtoto, nishahisi majanga katika family yangu. Vipimo vinaonesha anapungukiwa hormone ya estrogen. Yani ht sijui nini hatma yake. Nisaidieni tu wataalam

akawaone wataalamu, kama tatizo ni Oestrogen basi anaweza kuongezewa kwa kutumia vidonge
 
Yaani haya ni matatizo sana mm mwenyew my wife mwaka huu wote alikuwa na mp ya 32 lkn tulikutana majuzi kila mmoja katoka mbali tulikutana ili tutengeneze mtoto cha ajabu mp kaingia cku 30 na hapo tulikuwa tunasubiri pengine atapata mimba lkn hakuna kitu hata cjui.hata hivyo safar hii hakuumwa tumbo km mp zingine.
 
Sababu ni inaweza kuwa mparanganyiko wa Hormones, kubadilisha mazingira, maambukizi ya vimelea vya magonjwa kama fungus n.k,Uzito kuongezeka,stress kuwa kubwa mfano mawazo,mshtuko n.k. Ovarian cyst .....n.k
 
kuna my friend anatokwa hedhi mfululizo zaidi ya wiki, kaambiwa ni hiyo hormonal imbalance, madhara yake ni nini ? tiba yake je?

Madhara ni kuwa na siku(Menstrual periods) zisizo na mpangilio mtu anaweza akapata heavy bleeding au asipate kabisa. Pili ni Infertility (kutokupevusha mayai) ambapo tatizo lisipopatiwa tiba anaweza kupata ugumba.

Tiba aende hospital ataambiwa nini cha kufanya kulingana na vipimo vitakavyoonyesha.

Kikubwa anaweza Anza na matibabu yake mwenyewe kwa kuzingatia vyakula anavyokula,chakula kinatakiwa kiwe kile Chenye virutubisho muhimu cha mwili ale mlo kamili,vyakula venye kuongeza uzito havifai,vyakula vya mafuta mengi ni tatizo,zaidi apendelee kula nafaka zilizokobolewa, kunywa maji mengi, awe na muda wa kutosha kupumzika. Ajitunze kwa usafi kuhakikisha anakaa mbali na vimelea vya Magonjwa kama fungus n.k
 
Aende hospitali huenda ana uvimbe. Kuna mbegu zinaitwa flax seeds hebu google manufaa yake. Kiufupi zinaregulate hormones. Unasaga kwa blender, then unaweka kijiko cha chakula 3x a day kwenye mtindi, uji ama oats.

Kwa dar zinapatikana shreejee supermarket ya oysterbay
 
Habari ndugu watanzania wenzangu,
Mrs wangu kaingia MP trh 19, jana,
Badala ya trh 28,
Ni baada ya kutumia dawa alizopewa kwa ajili ya mchango,
Maake pia tunatafuta mtt. Kwa sasa kwan n mwaka wa 8 sasa tangu tupate wa kwanza.
Je kwa afya ya uzazi hayo mabadiliko yanamaanisha nini?
 
Tutaenda,
Lkn si mbaya tukapata chochote hapa,
Kwan tuko mbal san na hosptl zeny,wataalam
 
Inaweza kuwa mabadiko ya homoni ama kama amebadili hali ya hewa. Inaweza kuwa ana uvimbe pia. Muhimu ni kumuona daktari, hasa kama ana maumivu

Kwa suala la kutafuta mtoto hii inaweza kuathiri siku za yai kupevuka. Nendeni kwa daktari wa wanawake na kuulizia kuhusu follicular study' . Unaweza kugoogle pia ukajielewesha maana yake. Hii inakupa siku kamili ambapo kuna yai la kupevushwa.
 
Back
Top Bottom