Nini hatma ya wafanyakazi wa Azam Habari kama kipindi chao hakitaonekana tena?

LICHADI

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
4,153
11,203
Ni miezi karibia mitatu sasa Azam Habari wamepotea hewani na hawaonekani tena Stesheni ya Azam two, katika king'amuzi chao. Lakini chakushangaza wanadai taarifa yao ya habari inaonekana mda uleule kupitia kwenye app.

Lakini ikumbukwe kuwa kwenye app yao hamna watazamaji wengi kama waliokuwepo kwenye king'amuzi chao, hivyo kwa sasa taarifa yao ya habari inawatazamaji wachache sana tofauti na mwanzo.

Ikumbukwe kuwa kipindi hujiendesha kutokana na idadi ya watu wanaotazama, kupitia matangazo ya wadhamini na malipo ya ving'amuzi ambayo ndiyo hulipa mishahara ya wafanyakazi .

Je kama Azam Habari haionekani tena kwenye king'amuzi chao na tayari washapoteza wateja wengi ambao hawalipii tena kutokana na kukosekana kwa taarifa ya Habari, Watawezaje kuwalipa wafanyakazi wote ikiwemo watangazaji waandaaji na mariporter wao waliopo nnchi nzima? .

Je sio Kwamba wanafanya kazi kwa Hasara?, siku uvumilivu ukimshinda Mwajiri kutokana na Hasara ni nini Hatma ya wafanyakazi wote hawa wa Azam Habari?.
 
Tunamalizia hizi za kawaida soon tunaingia za kirumi, tuvumiliane.
 
Wanajaribu lakini hawatoweza na juzi juzi wameajiri wafanyakaz wapya sijui wanajiamini kitu gani hawa watoto wa mzee SSB
 
Back
Top Bottom