Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,619
Kuna mvutano kati ya Tz na Kenya kuhusu ubunifu na matumizi ya misamiati na istilahi za lugha adhimu duniani ya Kiswahili.
Mvutano huu unakwaza maendeleo ya lugha ya Kiswahili kinachoongelewa kwenye mataifa zaidi ya 100 na kufundishwa kwenye vyuo vikuu 100 duniani.
Ili lugha ipate ithibati ya kutumika kimataifa inatakiwa iwe na mfanano wa misamiati na istilahi ili kutochanganya watumiaji hususan wageni.
Wenzetu Kenya walijiwahi kuingiza Kiswahili chao kwenye google na kukamata dunia. Lakini zaidi Wakenya wan waandishi wa vitabu kwa sababu ari ya kuandika na kusoma vitabu ni kubwa Kenya kuliko Tz.
Nyuma ya Wakenya kuna Wacongo pia ambao wanauza walimu wa Kiswahili duniani hususan soko la EU.
Kiswahili kimegawanyika kwenye kanda kadhaa zilizozalisha utofauti wa isimu ya lugha ya Kiswahili na kupotosha matumizi yake. Hadi sasa kuna kanda za Kiswahili zifuatazo:-
1. Kiswahili cha Mwambao.
2. Kiswahili cha Kikongo.
3. Kiswahili cha Kikenya.
4. Kiswahili cha Kingazija.
5. Kiswahili cha Kitz-bara
6. Kiswahili cha Kitanga (Shaaban Robert)
7. Kiswahili cha Kiunguja (Shafi Adam Shafi)
Mifano michache tu kuthibitisha mvutano kati ya Tz na Kenya kuhusu ubunifu na matumizi ya misamiati na istilahi za Kiswahili ni hii:-
1. DNA
Tz inaita vinasaba Kenya inaita msimbojeni (gene).
2. COMPUTER.
Tz inaita Kompyuta Kenya inaita Tarakilishi au hata Tarakishi.
3. LAPTOP.
Tz inaita Kompyutampakato Kenya inaita Kompyuta ya mkononi. Sijajuwa kwanini wasiite Tarakilishi/Tarakishi ya mkononi.
4. RISASI.
DRC Mashariki inaita Masasi Tz inaita Risasi.
Nk nk nk.
Lini tunatoka kwenye huu mkwamo?