Tumekuwa tukisoma na kusikia vyombo vya habari, vyama vya siasa na taasisi za kijamii wakitumia hili neno KATIBA YA WANANCHI hadi kufikia kundi moja la wajumbe wa bunge maalum la katiba kuunga Umoja wao na kujiita UKAWA. Tatizo la neno hili lipo ktk matumizi yake, na weredi umetofautiana sana baina ya Wananchi wenyewe, wanazuoni na wanasiasa na kwa sababu tofauti. Aidha maana hizi zimetumika kwa kuzingatia umuhimu wa katiba yenyewe na utunzi wake ama kutokana na tofauti za wananchi wenyewe ktk ufuasi wa vyama vyao vya kisiasa na upinzani wa kiutawala.
1. Wapo wanaoita mchakato wa katiba hii unalazimika kufuata rasimu yenye Maoni ya wananchi kuwa hii ndio maana halisi ya neno hili na imeungwa mkono kwa idadi kubwa ya wasomi na wanasiasa ambao wameunda umoja huo wa UKAWA kushinikiza rasimu ya Warioba iwe ndio framework ya uandishi wa katiba Mpya. Haya ndio matakwa ya wananchi na lazima yafuatwe..Na sababu kubwa ya kukubaliwa kwake ni kutokana na ukusanyaji wa mawazo ya wananchi wa bara na visiwani ambao walipendekeza mabadiliko makubwa ktk muundo wa serikali, mfumo wa Utawala, Utaifa na mengineyo mengi ambayo wananchi wenyewe walipendekeza kuwa ndiyo yawe mwongozo wa nchi yao.
2. Na wapo wanazuoni ambao wanaamini maana halisi ya Katiba ya Wananchi ni Katiba itokaynayo na wananchi wenyewe, katiba ambayo inayowagusa, inawahusu raia wote pasipo kujali tofauti zao za kijamii kwa kuzingatia matabaka waliyomo ili kuimarisha umoja na Utaifa wao. Katiba ya wananchi ni mwongozo unao wahakikishia wananchi kuwa UHURU na HAKI zao zinalindwa. Katiba ndio sheria mama ya Taifa (Fundamental law), yanye mamlaka ya juu kisheria (supreme legal Authority) hivyo raia wote ktk makabila na matabaka yao, vyombo vya serikali, majeshi, vyama vya siasa, vyombo na taasisi za Umma na mashirika yote binafsi na ya serikali wote kwa ujumla wao wanalazimika KUTII katiba hiyo kama mwongozo wao (a basic norm of conduct) na wote wanawajibika ktk kuheshimu na kuhakikisha katiba hiyo inatekelezeka. Katiba hii haitungwi kwa Mawazo ya wananchi wote ama walio wengi bali ni katiba unayogusa hisia na kuwalinda wananchi wote na Uhuru wa nchi yao..
Imenilazimu kuandika mada hii ili kupanua fikra zetu ktk weredi wa neno hili na matumizi yake hasa baada ya kuwasoma baadhi ya Wanasiasa na Wasomi tena wengine wanasheria wakisema hakuna haja wala haraka ya kuipata katiba Mpya isipokuwa kinachotakiwa zirekebishwe baadhi ya Ibara za kisiasa ktk katiba wanayodai imepitwa na wakati ili kuwezesha uchaguzi ujao uwe wa wazi, haki na usawa kwao wao. Tena inaonyesha wako karibu kufikia muafaka wa kuahirisha katiba ya wananchi ili kulinda maslahi ya wanasiasa wa pande zote mbili ambao hawawajibiki kwa wananchi isipokuwa kwa vyama vyao vya siasa.
Sasa leo hii hiyo KATIBA YA WANANCHI ilosiwamiwa kwa nguvu zote inaonekana kutupwa pembeni na maswala ya muafaka wa kisiasa kuchukua nafasi kusema kweli imesikitisha sana, yaani madai yote ya wananchi iwe kwa mtazamo wa kwanza ama wa pili unawekwa pembeni kupisha uwekekano wa uchaguzi ujao pasipo kupata ridhaa ya wananchi wenyewe ambao pengine (who knows) wapo radhi kwao uchaguzi ujuao uahirishwe hadi hapo katiba yao itakapo patikana kwanza.
Maoni yenu wana Jamii..