Mzalendo_Mkweli
JF-Expert Member
- Jan 30, 2012
- 2,067
- 1,328
KILA mtu atauchukua mzigo wake mwenyewe, kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe, kila mtu atatoa hesabu yake mwenyewe siku hiyo ikifika
Hiki ni kipande cha wimbo ambao ulivuma na kupendwa sana miaka ya nyuma ambao una maana ya kwamba kila mtu atahusika na matendo kwa kusimama na kutoa hesabu ya matendo yake mwenyewe siku ya hukumu itakapofika.
Nikiwa miongoni mwa wapenzi wa wimbo huu na makala za maonyo ambazo nimekuwa nikiziandika juu ya waimbaji wa nyimbo za Injili, Leo pia natumia kipande cha wimbo huu kufikisha ujumbe kwa wahusika katika kukumbushana nini hasa wajibu wa waimbaji wa nyimbo za Injili mbele ya jamii, hasa kwa kuzingatia kuwa wao ni barua ya kusomwa na watu wote.
Niseme kwamba, kamwe sitanyamaza kutoa maonyo pale ambapo ninaona hapako sawa hasa katika kuichafua misingi halisi ya Ukristo kupitia uimbaji wenu.
Kwa muda mrefu waimbaji wa kwaya hapa nchini wamekuwa wakilalamikiwa kwa tabia zao kwenda kinyume cha maadili ya mafundisho ya neno la Mungu ambayo huyasisitiza kupitia uimbaji wao.
Japo si wote, baadhi ya waimbaji ni wenye tabia za ajabu ajabu ambazo kama zingewekwa haradhani, ungeweza kubaki kinywa wazi, usiamini macho yako kwani wanavyoimba madhabahuni au jukwaani sivyo wanavyoenenda.
Wanaume kwa wanawake, baadhi yao wamekuwa janga kwa ndoa za watu kutokana na kujihusisha kimapenzi na waume au wake za watu, wakiwemo viongozi wao watumishi wa Mungu, waimbaji wenzao ama wazee wa makanisa.
Mbaya zaidi, ni pale inapotokea safari ya kwenda kuhudumu nje ya mkoa waliopo, mambo yanayotendeka ni ya aibu, hayasimuliki, maana hutawaliwa na ndoa za muda.
Ninasema haya kwa uchungu kwa kuwa sidhani kama ndio wito walioitiwa, naelewa wao ni binadamu wanaopitia changamoto za matamanio, lakini
Je, maandiko ya Mungu yanasemaje juu ya hilo?
Je, ni fahari gani kuwa na mahusiano yanayoleta watoto mabazazi ambao kila mmoja ana baba yake?
Je, kwa kufanya hivyo, heshima iko wapi ya watumishi wa Mungu ambao wanapaswa kuyaishi yale wanayoyaimba madhabahuni na jukwaani?
Je, waimbaji hawajui kuwa wao wanapaswa kuwa barua ya kusomwa na watu wote ili hicho wanachokihubiri kupitia nyimbo zao kiweze kuwarudisha kundini kondoo waliopotea?
Ni wazi uimbaji kwenye mazingira haya, ni sawa na kujidanganya bure kwani wahusika watakuwa wakiimba katika malengo ya kimwili zaidi, si kiroho kwa
vile huyo Mungu wanayedai kumwimbia hatakuwa pamoja nao.
Mtu anaweza kusema ninaingilia maisha ya waimbaji wetu, lakini hatupaswi kufumbia macho vitu kama hivi wakati nao ni kondoo wanaopotea licha ya kuonekana wakiiimba madhabahuni kila kukicha.
Najisikia vibaya kuona waimbaji wanasemwa kwa mabaya hasa katika uzinzi, ulevi mambo ambayo yanakwenda kinyume cha mafundisho ya Mungu katika vitabu vitakatifu.
Nayasema haya si kwamba mimi ni mkamilifu na mtimilifu mbele za Mungu, isipokuwa ni kuwakumbusha waimbaji wa Injili kutambua kuwa wao ni barua ya kusomwa na watu wote, hivyo waishi na kuenenda kama waimbavyo.
Kwa kufanya hivyo, ndipo watakapokuwa chachu ya kweli katika kuwarejesha kundini kondoo wote waliopotea, hivyo kumgeukia Mungu wakimwabudu kwa roho na kweli itakayowafanya kuwa huru dhidi ya minyororo ya dhambi.
Kinachonisikitisha ni kuwaona hata baadhi ya watumishi wa Mungu wakiwamo waimbaji mahiri wakienda kinyume cha mafundisho yao, ambayo huyatoa kwa jamii kupitia uimbaji wao ambao pia ni karama kutoka kwa Mungu.
Source : Tanzania Daima – Nini hasa fahari ya waimbaji wa Injili?