Yaani natumaini umeona jinsi wa Tanzania wanavyotia aibu kwa chuki na kuamua kupigia kura wasanii wa nchi zingine.
Tabu ilianza Kiba aliporudi alitumia maneno ya kuwa yee ni kingi na anataka kiti chake yaani kwa kuwa Diamond yupo juu yeye anataka kumpita.
Diamond hajawahi sikika akiongea mabaya au kutamka mabaya juu ya kiba au kitu chochote zaidi ya kusema kama watu wanataka kushindana nae yeye pia anapata kiki ya kufanya bidii zaidi na kutojisahau. Nadhani hii kitu hata yeye atakuwa anashangaa bidii ya alipofika inatakwa ishushwe na wananchi sababu amepata maendeleo mazuri kwa kujituma kufanya vizuri.
Kiba ibabidi abadilike, maana hata jana alikuwa mjini nilipo na mbwembwe sema wengi tulikuwa na harusi bomba hatukwenda bali walioenda walisema sio inavyokuwaga wa Tanzania wakianua kuhudhuria shughuli.
Inabidi aache kuchochea wananchi kutaka kushindana na Diamond sababu hana cha kuonyesha tangu ametudi.
Tuzo sawa ila akumbuke tuzo hazitoi pesa ya kuishi.
Inasikitisha sana tabia ya wanaoonea wivu Diamond kwa mafanikio hawataki afanikiwe zaidi.
Kiba una uwanja na hata siku moja hakuna msanii nwingine amekuingilia ila uwanjani ulipo wewe ni wewe na sio kwamba wengine ndio watakusaidia sema wakishuka hautapanda, Diamond yuko juu kubali shindana nar tuone mambo kuwa na wewe unataka kupaaa.
anhaaa na wachangiaji tuendelee huku tukikusanya maoni
mdau hapo kawasiliaha chanzo ni kauli ya kiba alivyorudi kwenye game.... mwenye kuunga mkono hoja aje na mwenye kupinga pia aje bila kusahau mwenye maoni tofauti
lakini sasa huo ujio wa kiba ulipokewaje na mashabiki na diamond mwenyewe?
bila Kiba diamond asingekuwepo au angechelewa sana kutoka
unaijua historia ya hawa?
unajua kuwa kiba ndie aliyemtoa diamond na diamond alipoona ametoka akaanza dharau?
Kiba kihistoria huwezi ukamtupa kukua bongo flava unless kama umekua juzi
kuanzia nakshi nakshi..... cinderela....n.k
Diamond lazima aheshimu waliomtangulia na waliomsaidia kufika hapo
kiba alimrekodia nyimbo ake bure kabisa hapo awali na ndiye aliye mwambie asiimbe rap
hivi unawezaje ukamdharau mtu kama huyo?
kwa nafasi ya diamond alikuwa na uwezo wa kutojenga makundi na kuheshimu waliomtangulia
kazi anayo, ataenda mbali ila anguko lake litakuwa si la kawaida; usicheze na mtu/watu aliyekutengeneza
ashinde kuroga tu atawapata wengi sana
mkuu hiyo dharau kainonesha kwa mitazamo ipi........ tudadavulie hapa tupate kufumbuliwa macho
Hapana hiii sio sababu. Hata.
Hilo la King limekuja fiesta ila ishu za team, zimeanza before that.
Nakumbuka kuna kipindi kulikuw hakuna maelewano baina ya watu wawili. Mmoja wapo akisema mwenzie kamuibia nyimbo, mara kafuta baadhi ya mistari ya wimbo walioufanya. Hapa kiba alikuwa kimya hakwenda kutoa statemnt kwenye media n.k.
Lakin baadae ikaja gundulika na kuwekwa wazi na Kiba huku akisema ushahid upo kuwa Dai, aliomba kiba akingiez mistar kwenye nyimbo yake na mwisho wa siku jamaa aliingiza na vikolombwezo vyake kadhaaa. Ila baada ya Kiba kumcholea Dai kupiga nyimbo ya Singo boi n single girl, Dai alifuta sauti ya kiba kwenye ule wimbo waliotengeneza. Manen yalifata kwenye media, hasa hapo mashabiki wakaanza kuvutana ku judge nani yupo wrong, team zikaanza hapo. Aliempenda Dai alion kaonewa hakutendewa haki. Waliona Kiba anaonewa wakaamua ku fight back.
So ikawa kama Simba na yanga rememb ushindan huu wa nan kaonewa ikaleta majibizano ya nan yupo juu, nadhan unaelewa majibizan ya namna hiii huibua kauli mbaya, mchezo ukaanzia hapo mseme vibaya K mashabiki watamsema vibaya D
sina clue mkuu tusaidiane hizo link hapa upate kutufumbua macho mimi na wengine wanaojua hizi teams kijuu juubifu la diamond na bob junior, ndilo hilo hilo la diamond na kiba
fuatilia interview za kiba
kumbe hauna clue, nitakuwekea link zote hapa
mkuu hiyo dharau kainonesha kwa mitazamo ipi........ tudadavulie hapa tupate kufumbuliwa macho
Kama unakielewa kiswahili vizuri utakuwa umenisoma, kapata tuzo5 nimesema kapata 8 awanii tuzo za mtv ila nimesema tumpigie kura, ukiamua kuwaelimisha vichaa inabidi uigize kama waoHahahaaa sijui nia yako ninini katika hili! Let me stay away.
Mfano alimdis kiba kwenye Twitter account yake kisa alikopa bank
bila Kiba diamond asingekuwepo au angechelewa sana kutoka
unaijua historia ya hawa?
unajua kuwa kiba ndie aliyemtoa diamond na diamond alipoona ametoka akaanza dharau?
Kiba kihistoria huwezi ukamtupa kukua bongo flava unless kama umekua juzi
kuanzia nakshi nakshi..... cinderela....n.k
Diamond lazima aheshimu waliomtangulia na waliomsaidia kufika hapo
kiba alimrekodia nyimbo ake bure kabisa hapo awali na ndiye aliye mwambie asiimbe rap
hivi unawezaje ukamdharau mtu kama huyo?
kwa nafasi ya diamond alikuwa na uwezo wa kutojenga makundi na kuheshimu waliomtangulia
kazi anayo, ataenda mbali ila anguko lake litakuwa si la kawaida; usicheze na mtu/watu aliyekutengeneza
ashinde kuroga tu atawapata wengi sana
Mfano alimdis kiba kwenye Twitter account yake kisa alikopa bank
Habari wanajamvi,
Nimeguswa mno na hii hali ya utimu inayoendelea.
Nini chimbuko la hizi teams?
Nani ni mchochezi kati ya wahusika na mashabiki?
Wahusika wamewahi toa tamko lolote kuhusu hali inayoendelea? tamko lipi?
Sisi wadau tunataka hatma ya hizi teams iwe nini?
MTAZAMO WANGU
Hizi timu zinakoelekea zinajenga chuki na mipasuko baina ya wasanii husika na wapambe, jambo ambalo ni adui wa kukua kwa muziki wetu. Kiba akipanda kwa juhudi zake binafsi na support ya mashabiki wake nini kitapungua? Sio lazima mtu mwingine ashushwe. Diamond akishuka kimuziki nini faida haswa? Ni lazima kulinganisha Uwezo wa hawa wawili tena pasipo na tija?
MAONI
Mashabiki tuna uwezo wa kuua au kukuza muziki wetu, ifike hatua tuache ushabiki na tutatue tatizo lilipo baina ya hawa wawili kwani kila mmoja ana umuhimu wake.
kukomoa sio njia ya kusolve tatizo especially kwa watu wenye busara na malengo.
Tofauti za kimitazamo, malengo, utumiaji fursa, ubunifu.Ni kitu kikubwa kinachoweza kutofautisha watu wawili wanaofanya kitu cha aina moja. alikiba ni muimbaji mzuri na diamond ni daraja zuri kwa Muziki wetu kutambulika kimataifa na hata wasanii wengine kupenya tuongeze idadi kama wanigeria.
wachangiaji tutoe michango ya kujenga, hapa tunasolve tatizo na sio kulaumu au ushabiki. Na ukileta lawama ni vema ukaweka ushahidi na chanzo husika.
NAWASILISHA.
anhaaa na wachangiaji tuendelee huku tukikusanya maoni
mdau hapo kawasiliaha chanzo ni kauli ya kiba alivyorudi kwenye game.... mwenye kuunga mkono hoja aje na mwenye kupinga pia aje bila kusahau mwenye maoni tofauti
lakini sasa huo ujio wa kiba ulipokewaje na mashabiki na diamond mwenyewe?
Naomba utoe ufafanuzi wa kutosha kuhusu hapo kwenye red.
Ni lini Kiba kachochea wananchi? Na kawachochea kivipi?
Unaposema hana cha kuonesha pia unamaana gani? Diamond ana wimbo gani wa maana wa kushindana na Mwana?
Binafsi nampenda Kiba tokea zamani sana, sikuwa hata na idea ya mitandao ya kijamii kama huu ambao naweza kutoa maoni/kuonesha mapenzi yangu kwake.
Sasa unaposema anachochea wananchi nimekushangaa sana.
Mleta maada nakubaliana nae kwa kiasi fulani maana ametumia busara katika kuwasilisha maoni yake, ila wewe hazihitajiki hata dakika 5 kujua wewe ni mtu wa mrengo gani.