Nini chanzo cha neno "kibanda-umiza".

orangutan

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
757
773
Kibanda-umiza ni neno la kiswahili lenye maana ya maeneo ambayo watu hukusanyika na kulipia huduma ya kuangalia michezo mbalimbali kama mpira wa miguu kwa njia ya televisheni. Naomba kujua kwanini wataalamu wa lugha wakaamua kuvipachika hivi vibanda kwa jina la vibanda-umiza. Nani anaeumia hapo?
 
Umiza kweli,
mfano; msiombe mvua ikanyesha ni tv tu itabaki salama vingine vyote vitalowa,
sehem za kukaa mchukua pesa ndio ana kiti chenye unafuu wenyine waliobaki watakaa kwenye benchi, tofali, chini, kreti
mda wa mchana mchanganyiken joto kali mjin, Jasho+harufu=kero ila kwasabab ndio uswaz unazoea tu
 
Hahahaaaa umenifungua macho mkuu
Umiza kweli,
mfano; msiombe mvua ikanyesha ni tv tu itabaki salama vingine vyote vitalowa,
sehem za kukaa mchukua pesa ndio ana kiti chenye unafuu wenyine waliobaki watakaa kwenye benchi, tofali, chini, kreti
mda wa mchana mchanganyiken joto kali mjin, Jasho+harufu=kero ila kwasabab ndio uswaz unazoea tu
 
Vibanda hivi mara nyingi vipo ovyo sana utakuta kimezungushiwa makuti au mabati chakavu na chini huwa havina sakafu ni mwendo wa mabenchi halafu chini vumbi balaa. Na havina sheria, mwingine anaingia na bia mwingine anavuta sigara ili mradi kila mtu kalipia 500 yake huwezi kumpangia chochote. Ukichelewa basi wewe kusimama mwanzo mwisho kuna kuhusu. Pia lugha za matusi na kupigana ruksa na usiombe timu yako ifungwe utajuta. Ki ufupi ndio maana kinaitwa kibanda umiza. NO RULES
 
Kibanda-umiza ni neno la kiswahili lenye maana ya maeneo ambayo watu hukusanyika na kulipia huduma ya kuangalia michezo mbalimbali kama mpira wa miguu kwa njia ya televisheni. Naomba kujua kwanini wataalamu wa lugha wakaamua kuvipachika hivi vibanda kwa jina la vibanda-umiza. Nani anaeumia hapo?
Huwa hakina comfortability.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom