Nini cha kufanya unaponyimwa haki ya dhamana

gsmsolution2009

Senior Member
May 7, 2013
120
195
Wadau kama kuna mtu anajua naomba anifahamishe nini natakiwa kufanya kama maaskari wanakataa kutoa dhamana katika kesi ya madai kwa sababu mfungua mashtaka anakataa mtu huyo asipewe dhamana na wao wanamsikiliza yeye
 
Dragoon

JF-Expert Member
Nov 24, 2013
7,032
2,000
Wadau kama kuna mtu anajua naomba anifahamishe nini natakiwa kufanya kama maaskari wanakataa kutoa dhamana katika kesi ya madai kwa sababu mfungua mashtaka anakataa mtu huyo asipewe dhamana na wao wanamsikiliza yeye
Kesi gani ya madai isiyo na dhamana? Kesi isiyo na dhamani ni jinai, tena baadhi ya makosa kama uhaini na unyang'anyi wa kutuma silaha. Katika kesi ya madai mfungua mashtaka hana udhibiti wowote wa mdaiwa. kuwa mkweli mkuu, sema tu kosa lililofanyika. Kihalisia kesi ya madai hata hao askari hawahusiki.
 
gsmsolution2009

Senior Member
May 7, 2013
120
195
Hata mie naelewa hivyo ila kinachoonekana hapa ni mfungua mashtaka anatumia nguvu ya pesa na vilevile ndugu yangu alikamatwa tangu alhamisi wamemweka ndani halafu jalada la mashtaka imefunguliwa jana jumamosi
 
BISECKO

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
542
1,000
Wadau kama kuna mtu anajua naomba anifahamishe nini natakiwa kufanya kama maaskari wanakataa kutoa dhamana katika kesi ya madai kwa sababu mfungua mashtaka anakataa mtu huyo asipewe dhamana na wao wanamsikiliza yeye
Suala la kufanya kama mtu ananyimwa dhamana na anashikiliwa kinyume na matakwa ya sheria, waweza omba amri ya mahakama ili huyo aliyeshikiliwa kinyume na sheria aletwe mahakamani ili ijulikane hatia yake ama kosa lake. Amri hiyo huitwa Harbeas Corpus kwa mujibu wa sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai.
 
soskeneth

JF-Expert Member
Jul 2, 2016
585
250
Wadau kama kuna mtu anajua naomba anifahamishe nini natakiwa kufanya kama maaskari wanakataa kutoa dhamana katika kesi ya madai kwa sababu mfungua mashtaka anakataa mtu huyo asipewe dhamana na wao wanamsikiliza yeye
Halafu mnapokuwa mnauliza maswar weken maswar kweny mstari ulionyooka,,hyo dhamana amenyimwa Kwa kosa gan? Anyway nisiende huko

Labda Kwa kifup kuna sababu kadhaa ambazo MTU a naweza akanyimwa dhamana,

1. Sababu ya usalama wako ww yaan mtuhumiwa,,labda ukipewa dhaman usalama wako baada ya kutoka pale utakuwa co mzur Wenda ukauawa kutokana na watu bado kuwa na hasira NA ww

2. Ulishapewa dhamana mwanzo halafu ukishindwa Ku comply na mashart ya dhamana uliyopewa,,Kwa hyo wanahisi wakikupa tena utarudia kama ulivyofanya mwanzo.

Hzo n baadh ya sababu ambazo mtuhumiwa a naweza akanyimwa dhamana,,zipo nyingi sana

KWA HYO KWA UPANDE MWINGINE USILAUM TU AMENYIMWA DHAMANA LAZIMA UJUE NI SABABU GAN WALIZOTOA WENDA NI NJEMA KWAKE
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom