Nini Cha Kufanya Ukishagundua Mwenzi Wako Anatembea Nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nini Cha Kufanya Ukishagundua Mwenzi Wako Anatembea Nje

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Superman, Jul 2, 2009.

 1. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mmmh Ipo Kazi!

  Source: How to Handle a Cheating Partner - wikiHow

   
 2. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Sijui kama wengine mmewahi kusikia hii true story ya miaka mingi iliyopita.

  Kuna mdau wa ambaye ni dereva wa magari ya mizigo yanayosafiri nchi za mbali. Siku moja aliaga anasafiri na kweli alifanya hivyo. Kwa bahati mbaya sana kabla hawajafika mbali gari ilipatwa na matatizo. Mdau akarudi home majira ya kama saa 10 alfajiri.

  Kwa kuwa alikuwa na funguo za akiba hakutaka kumsumbua mke wake, hivyo alifungua na kuingia ndani huku nyuma akifunga mlango. Walikuwa wanaishi yeye na mkewe tu.

  Mdau alipigwa na butwaa baada ya kufika chumbani na kukuta mamaa na jamaa wakila matunda ya mti wa kati. Kwa ustaarabu mkubwa jamaa alimwomba mke wake waongee na kumwacha jamaa ndani asijue cha kufanya. Mdau alimweleza mama kuwa asiwe na wasiwasi. Na alimwomba sana ili kuwe na amani ajifanye kama hakuna kitu kimetokea vinginevyo angeua mtu. ikabidi mama akubali.

  Mdau akaomba shuka akenda kulala sitting room huku akimwacha mama na jamaa wakiwa bedroom hadi majira ya saa kumi na mbili asubuhi. Jamaa alienda kumwamsha mke wake na kumsihi amtayarishie jamaa maji ya kuoga na hatimaye breakfast.

  Baada ya kuoga wote watatu walikaa dining room kupata kifungua kinywa huku mdau akipa story na mbaya wake na kumwakikishi asiwe na wasiwasi na baada ya hapo mdau akamwambia mamaa kuwa wamsindikize jamaa yeye akimwita "mgeni". Walipofika nje baada ya muda jamaa alimwambia mama basi msogeze kidogo mgeni wetu, mimi narudi home.

  Mamaa aliporudi home akamkuta jamaa yuko vizuri tu wala hana noma. Toka siku hiyo jamaa hakuongea chochote kuhusu hiyo issue. Ila hakujamiiana na huyo mkewe tena.

  Mamaa baada ya kama mwezi akawa anazidi kukonda tu kwa msongo wa mawazo asijue cha kufanya. Akajipeleka kijijini kwa wazazi wake na kuwatangazia kuwa ndoa yao ina matatizo. Mdau alipoitwa yaani mume na kuulizwa, aliwajibu wao hawana matatizo yoyote na wanaishi vizuri tu. Basi wazazi wakafurahi kuwa hakuna matatizi ila wakashangaa binti yao alivyokonda.

  Baada ya mwezi tena binti akarudi na kudai wana matatizo. Mr alipoitwa akawaambia yeye hana matatizo na mkewe na kama mkewe andadai kuna shida basi aseme ni shida gani. Ikabidi mama ajifunge bao la kisigini kwa kuelezea dhambi aliyofanya. wazazi wake walimjia juu sana. laki ni Mr aliingilia kati na kuwasihi wamwache mke wake anampenda na alishamsamehe kwa hilo ndiyo maana alisema hawana shida.

  Yule mke alikoma na inasemekana anampenda sana mumewe isivyo kawaida. Wanaume wengine "Fataki" anawaona si deal kabisa.

  My take:

  Kumwadhibu partner ambaye si mwaminifu si lazima umpige, kumtukana au kumfungulia kesi, talaka n.k.

  Lakini je, ni wangapi wana courage hiyo?
   
 3. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...tupo wengi tu! :)
   
 4. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu kama ni kweli basi umebarikiwa sana.

  Ingekuwa wengine baistola au panga mkononi . . . LOL
   
 5. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Duh hii kali superman...nampa jamaa hongera sana. I cannot imagine kama ndo ingekuwa mimi...ningehama hata na nyumba kwa uwoga wa sijui nini kinachoendelea kichwani mwa jamaa. Nampa dadangu huyo hongera pia. Nimeipenda saa hii article, congrates! Naomba kuja chumbani tuongee kitu.
   
 6. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mh!
  Wivu Sina.....................
   
 7. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Penny kuna visa vingine katika maisha ukivisikia machozi yanaweza kukutoka, moja wapo ni hiki. Kwa kusoma inaonekana kama ni kitu rahisi tu, lakini katika hali halisi inataka moyo sana.

  Unataka kuja chumbani wapi tena Penny? Au una maana kuni-PM? Karibu sana. Niko na my wife wangu hapa.
   
 8. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Naam ndugu yangu, kosa sio kosa...atapolirudia ndio litakuwa kosa hapo nitakuwa na hiari ya kumsikiliza kulikoni na kumsamehe au ndio hivyo tena.

  Kuhusu bastola na panga aaarrgghh, hiyo itakuwa murder case. Kwani unadhamiria kumtoa nani roho?, ...mke/mume au huyo "anayekula" mali zako?
   
 9. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Jamani kwa lipi tena G loho iiumeee!
   
 10. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...Penny, you have been warned! :D
   
 11. Penny

  Penny JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 577
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Hiyo ni tadhari tuu nisije kuharibu hali ya hewa.
   
 12. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu, hapa hekima yako nimeikubali.

  Sina uhakika kama ningeweza kuua na ni yupi katika hayo.

  Lakini unajua katika hali kama hiyo anything can happen.
   
 13. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu, sasa baada ya kurudi kijijini mara ya pili, je, waliendelea kula tunda au mgomo uliendelea?
   
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa kutia chumvi! hahah sikuwezi
   
 15. Bonnie1974

  Bonnie1974 JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 407
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wacha wewe Mkuluuuu
  Hi
  Longtime.

  Huyo mshikaji alikuwa na Mtu kabla ya hilo tukio alilohadithi Superman,ndiyo maana alikuwa Muungwana.

  Most of the time MTU AKIWA MUUNGANA SANA KWA VITENDO VYA HOVYO VYA MKEWE LAZIMA ATAKUWA NA MTU.HIYO NI FORMULA.

  Yule ANAYEPIGA KELELE, OH MYWIFE WANGU "HIVI NA VILE" huyo mara nyingi utakuta "HAPO NDIPO ANAPATEGEMEA"
   
 16. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #16
  Jul 3, 2009
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Wataalam wa saikolojia wanasema ukitaka kujua hulka halisi ya mtu mpe kitu kimoja kati ya haya mawili,PESA (kwa maana ya utajiri) au MAMLAKA (kwa maana ya power).Binadamu anayeweza kuhimili vitu viwili hivi bila kuvi abuse basi huyo ni shujaa.Hata uzinzi huu tunaoongelea,kutembea nje ya ndoa etc mara nyingi ni matokeo ya mtu kuibuka ghafla na pesa au mamlaka,check it out utaniambia.
   
 17. Akili Unazo!

  Akili Unazo! JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2009
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 2,761
  Likes Received: 2,397
  Trophy Points: 280
  Mkuukwa kweli katika adhabu mbaya kuliko zote hii aliyoifanya huyu jamaa ni adhabu mbaya kuliko zote na mara nyingi hii huwa inaishia kutengana.

  Mfano mzuri hata leo itokee kwako samahani kama hujoa au kuolewa utakuwa na mpenzi au mwenzi wako itokee siku moja umkute mwenzi wako analiwa au anakula uroda na mwingine wewe ufike uone na ushuhudie halafu uwaache waendelee kweli si itakuwa ndo automatic divorse hiyo?

  Binadamu tumeumbwa kusemwa au kugombezwa kwa namna yoyte pale tutendapo kosa ili kesho na keshokutwa tujue kwamba tulichokifany si kizuri kabisa.Sasa unaponikuta natenda kosa halafu husemi kitu huoni kwamba nitakuogopa maana yake siku ya kujakuniadhibu itakuwa ni mauaji.
   
 18. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu, sasa hivi wanafuraia maisha tu. Tunda kama kawa . . .
   
 19. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145

  Mkuu, kuna watu wengine watu wa Mungu sana. wanasemehe pale wanapokosewa na kuombwa radhi.

  Ila kwa binadamu wa kawaida, Ngoma hii ni nzito.
   
 20. Superman

  Superman JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2009
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 5,702
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Mkuu hapa sijakupata vizuri. Una maana Mamaa ndiyo alikuwa na Pesa au Mamlaka au Mume wake au Mgoni? Au ni maoni ya ujumla tu?
   
Loading...