Kuna kitu nimekuwa nikifikiria sana, na kila nikirudi kwenye hoja ile ile, naendelea kuona kwamba mengi tunayoyasikia sasa ni propaganda tu—njia ya kutafuta uungwaji mkono kutoka kwa watu wasiopenda kuchambua mambo kwa undani.
Kabla ya maandamano, Watanzania tulisema wazi kabisa:
Tunataka katiba mpya
Tunataka uchaguzi huru na wa haki
Tunataka heshima kwa sauti ya wananchi
Haya malalamiko yalikuwa ya wazi, ya amani, na ya miaka mingi. Lakini CCM na wale wanaowazunguka wakayachukulia kama mzaha—kana kwamba wananchi hawajui wanachotaka. Walijaribu vitisho, wakadhani vitamaliza kilio cha watu. Haikufaulu.
Viongozi wa dini wakatoa wito wa busara: serikali isipuuzie kilio cha wananchi. Badala ya kusikiliza, wakawaona kama wavuruga amani. Na siku ya uchaguzi, kila mmoja ni shahidi wa yaliyotokea.
Baada ya hapo, CCM wakaanza kutoa visingizio kila kona:
Ni wageni wamechochea
Vijana hawakujua walilokuwa wanafanya
Wamelipwa pesa
Hivi vyote ni vya nini? Mbona havina msingi?
Wakaona hoja hizo hazikubaliki, wakaanza kuleta udini—kama tiba ya kuficha ukweli. Lakini hata hilo limewashinda, kwa sababu Watanzania wa leo si wale wa zamani. Sasa dunia inawaangalia pia; jumuiya ya kimataifa imeanza kuhoji kubinywa kwa demokrasia nchini. Badala ya kujibu hoja, tena wanakuja na kauli za kuogofya: Wanataka kuiba rasilimali za nchi.
Kwa nini tunapoteza muda na mbinu hizi zote?
CCM, kwa nini msisikilize tu wananchi? Kwa nini mkatae kutatua chanzo cha tatizo? Madai ya wananchi si uchochezi. Ni haki. Ni demokrasia. Ni mustakabali wa taifa letu.
Kama kweli tunapenda amani, basi njia rahisi na salama ni moja tu:
Sikilizeni wananchi, siyo kuwatisha. Sikilizeni wananchi, siyo kuwagawa. Sikilizeni wananchi, na taifa litaepuka misukosuko isiyohitajika.