Nini asili ya neno bodaboda?

Nini asili ya neno bodaboda?

Hii biashara ilianzia Kenya,Na Kenya wanatumia maneno mengi ya English katika maongezi yao,neno border kwa English ni mpaka wa baina ya kijiji na kijiji,wilaya na wilaya,mkoa na mkoa,nchi na nchi,kwa hiyo wakimaanisha,wakikubeba nikutoka ulipo mpaka mwisho wa safari yako,hawakushushi kwenye kituo cha bus kama daladala.Ni.mbinu yakutangaza biashara zao,kuwa ukipakia bodaboda,inakuchukuwa uliko,huna haja ya kwenda kituo cha bus,na kukufikisha unakokwenda,hawakushushi njiani,kwa sababu pikipiki tofauti na gari na bajaj,inapenya hata kichochoro au daraja la wapita kwa miguu.
Sio kweli, asili yake ni kutoka uganda mkuu na sio Kenya kama walivyoeleza wadau hapo juu
 
Asili ya neno Bodaboda inatokana na neno/maneno ya kiingereza 'boader to boader' ikimaanisha 'mpaka hadi mpaka'. Biashara ya ukodishwaji wa pikipiki kama chombo cha kusafiria ilianzia zaidi mipakani hasa maeneo ya Congo, Uganda na Rwanda, ambako wafanya biashara wa biashara (halali na haramu) walitumia zaidi usafiri wa pikipiki za kukodi kusafiria, lakini zaidi kutoka mpaka mmoja hadi mpaka mwingine, au hadi kuvuka mpakani kuingia nchi nyingine. Abiria alimwambia dereva wa Bodaboda kwamba 'nipekele kutoka boda hii hadi boda ya upande mwingi (Bodaboda)
Umemaliza kila kitu mpaka nimekosa cha kumuongeza.
 
Wadau nawasabahi Nimekuwa nasikia Waendesha Pikipiki za biashara wanaitwa BODABODA binafsi sijui kwanini wanaitwa jina hiyo .Ombi kwenu nini Asili ya jina hilo mpaka Wakaitwa hivyo?
Kwa watu wa Kyela ni jina la miaka na miaka enzi za kina Kaka, mabasi ya Kyela yalikuwa yakifika karibu na Kyela mijini akina Matemabeach, Zainab, Railway na mengineo yanasimama njiapanda ya kwenda Kasumulu ambako ni mpaka wa Tanzania na Malawi, hapo njiapanda walikuwepo vijana wenye baisikeli zenye viti vipana kwa kubeba abiria, basi likisimama vijana hao huanza kuita abiria kwa kusema "BODA" wakiwa na maana ya kuwapeleka Kasumulu kwenye mpaka wa Tanzania na Malawi, hicho ndicho chanzo cha jina Bodaboda.
Dar na kwingineko kusikokuwa na mpaka wa nchi na nchi wameiga tu jina bila kujua ili uite Boda lazima uwe na mpaka, hata hivyo jina ni jina litumikapo halina tafsiri tena.
 
BH
Asili ya hilo neno ni huko mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kuna mizigo ilikuwa inaenda kuchukuliwa Uganda sasa ili kuingia Uganda lazima uvuke mpaka yaani border tamka boda.
Hivyo dereva wa pikipiki akiwa ananadi usafiri wake utamka boder border akimaanisha usafiri huu unaenda mpakani
Ni kweli, kwa kuongezea tu; ilianza na baiskeli, ndio zilikua zinaitwa bodaboda, hata Kampala mjini.
 
Mara ya kwanza kuona bodaboda ni uganda 2005 kwenye nyimbo ya chameleon SHIDA ZA DUNIA..!!2005 Tz biashara hio hakuna na ukimiliki pikipiki wewe ni gumzo mtaani mana hata Kumiliki TV nyumba 50 mtaani kwenu wenye tv hawazidi 7..!!
 
Back
Top Bottom