Nini asili ya neno bodaboda?

Nini asili ya neno bodaboda?

Wadau nawasabahi Nimekuwa nasikia Waendesha Pikipiki za biashara wanaitwa BODABODA binafsi sijui kwanini wanaitwa jina hiyo .Ombi kwenu nini Asili ya jina hilo mpaka Wakaitwa hivyo?
Asili ya neno Bodaboda inatokana na neno/maneno ya kiingereza 'boader to boader' ikimaanisha 'mpaka hadi mpaka'. Biashara ya ukodishwaji wa pikipiki kama chombo cha kusafiria ilianzia zaidi mipakani hasa maeneo ya Congo, Uganda na Rwanda, ambako wafanya biashara wa biashara (halali na haramu) walitumia zaidi usafiri wa pikipiki za kukodi kusafiria, lakini zaidi kutoka mpaka mmoja hadi mpaka mwingine, au hadi kuvuka mpakani kuingia nchi nyingine. Abiria alimwambia dereva wa Bodaboda kwamba 'nipekele kutoka boda hii hadi boda ya upande mwingi (Bodaboda)
 
Asili ya hilo neno ni huko mpakani mwa Tanzania na Uganda. Kuna mizigo ilikuwa inaenda kuchukuliwa Uganda sasa ili kuingia Uganda lazima uvuke mpaka yaani border tamka boda.
Hivyo dereva wa pikipiki akiwa ananadi usafiri wake utamka boder border akimaanisha usafiri huu unaenda mpakani
 
Swali zuri,
Kama nakumbuka vizuri niliwahi kusikia kwenye kipindi fulani cha DW TV, kuwa asili ya neno bodaboda ni nchini Uganda ambapo pikipiki zilikua zinatumika zaidi kusafirisha abiria kupeleka maeneo ya mipakani (border) au kuwahamisha toka mpaka moja kwenda mwingine ( border to border) then neno likakua na kutapakaa ukanda wote wa E.Afrika
NB: Zingatia neno kama nakumbuka vizuri
 
Hii ndio koment sahihi
 
Mimi pia nilikuwa sijui hadi nilivyosikia wakielezea BBC kama wadau walivyoelezea hapo juu.
 
Wadau nawasabahi Nimekuwa nasikia Waendesha Pikipiki za biashara wanaitwa BODABODA binafsi sijui kwanini wanaitwa jina hiyo .Ombi kwenu nini Asili ya jina hilo mpaka Wakaitwa hivyo?
Hii biashara ilianzia Kenya,Na Kenya wanatumia maneno mengi ya English katika maongezi yao,neno border kwa English ni mpaka wa baina ya kijiji na kijiji,wilaya na wilaya,mkoa na mkoa,nchi na nchi,kwa hiyo wakimaanisha,wakikubeba nikutoka ulipo mpaka mwisho wa safari yako,hawakushushi kwenye kituo cha bus kama daladala.Ni.mbinu yakutangaza biashara zao,kuwa ukipakia bodaboda,inakuchukuwa uliko,huna haja ya kwenda kituo cha bus,na kukufikisha unakokwenda,hawakushushi njiani,kwa sababu pikipiki tofauti na gari na bajaj,inapenya hata kichochoro au daraja la wapita kwa miguu.
 
Swali zuri,
Kama nakumbuka vizuri niliwahi kusikia kwenye kipindi fulani cha DW TV, kuwa asili ya neno bodaboda ni nchini Uganda ambapo pikipiki zilikua zinatumika zaidi kusafirisha abiria kupeleka maeneo ya mipakani (border) au kuwahamisha toka mpaka moja kwenda mwingine ( border to border) then neno likakua na kutapakaa ukanda wote wa E.Afrika
NB: Zingatia neno kama nakumbuka vizuri
Ni sahihi ,kipindi bodaboda zinaanza kuwa nyingi nilikuwa naishi Bukoba,na wasanii wa bukoba na Uganda walikuwa wanaimba nyimbo za kuusifu huu usafiri,ndipo baadae biashara hii ikaenea kwa kiasi kikubwa sehemu nyingine za tz
 
Neno liligeuzwa sio Bodaboda ni Dabodabo yaani ya kubebea watu wawili wawili. Na ukibeba watatu lazima uanguke.😎😎😎
 
Asili y neno bodaboda linatokana na neno "border to border " au chocho kwa chocho...

Linatumikana kweny kiswahili cha kawaida ....
 
Back
Top Bottom