Kwa wale waliobahatika kufika uarabuni au kusimuliwa habari za huko uarabuni, nini asili ya neno Arab? Je mtu / watu mweusi / weusi wanaoishi uarabuni wametokea wapi? Je ni wote walipelekwa huko kutokana na utumwa?
Je unafahamu mafarao wa kwanza walikua na ngozi nyeusi na nywele za kipilipili kama zetu? Ukifika Saud Arabia utawakuta watu wengi tu weusi tena kuliko waafrika wenyewe. Hawa asili yao ni uarabuni hata kabla waarab wa leo ngozi nyeupe tunaowajua! Hawako huko kutokana na ile biashara ya utumwa kama wengi tujuavyo.
Maana ya neno Arab ni mtu mweusi!
Kwanza kabisa kuna dhanna uliyokwisha ikubali na haiko sawa kimantiki. Unaposema "Uarabuni", Uarabuni ni neno la kuashiria kuwa huko kuna Waarabu, kuna Uarabuni Igunga, kuna Uarabuni Bujumbura na waliopaita Uarabuni hapo Igunga na Bujumbura hawajakosea kabisa, waliashiria kuwa hapo kuna Waarabu. Na Uarabuni si nchi au Taifa fulani au sehemu fulani maalum, Uarabuni inaweza kuwa popote tu.
Hapa Dar kwa sisi wa zamani, kuna Uzunguni, Uhindini, Uswahilini. Hakuna kosa katika hayo, ndipo sehemu ulipokuwa unawaona Wazungu, Wahindi na Waswahili wakiishi na iliashiria hivyo.
Neno Arab.
Neno Arab linatokana na neno "Arabiya" kwa maana "caravan" au msafara. Waarabu ni watu wa misafara waliokuwa wakiongea lugha yao ya Kiarabu (lugha ya watu wa misafara), Uarabu si Taifa wala si Kabila wala si rangi ya watu fulani, Uarabu ni lugha.
Wengi wa hawa Waarabu asili na kwao haswa ni Afrika, na ndipo wanapopatikana kwa wingi kuliko popote kwingine duniani. Na lugha ya Kiarabu ndiyo llugha inayotumika sana Afrika na kwa watu wengi zaidi kuliko kwingine kokote duniani.
Kumbuka pia, bara la Afrika na Asia lilikuwa halina mpaka wala kizuizi cha kuingiliana misafara mpaka hapo mwaka 1859 mfereji wa Suez ulipoanza kujengwa na kuigawa Afrika na Asia, ndipo misafara na muingiliano wa bila kizuizi wa mabara haya mawili ulipoingia dosari.
Uarabu ni Uafrika halisia, ulimwagikia tu Asia kwa kuwa kulikuwa hakuna kizuizi na biashara za enzi na enzi ziliruhusu muingiliano huo usio na kizuizi na kufanya Kiarabu kizagae sana hususan Kaskazini ya Afrika na Mashariki ya Afrika na Magharibi ya Asia. Hakuna shaka kuwa maneno ya Kiarabu yalizagaa mpaka kusini mwa Afrika tunapokutana na Shaka Zulu, Shaka = Sheikh.
Hayo ni kwa ufupi na uchache na katika hili nipo tayari kupokea maswali na unapohitajika ufafanuzi zaidi ntakuwa tayari kufanya hivyo.