Nini asili ya maneno "Jisaidie na Mungu akusaidie"

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
Hili neno Jisaidie Mungu akusaidie limekuwa likitumika sana uswahilini.

Mara nyingi watu wamekuwa wakisema kuwa ni moja ya nukuu ya vitabu vya Mungu(misahafu), lakini ukichunguza kwenye vitabu vya dini zote mbili kubwa Tanzania yaani Biblia na Qur'an huwezi kuikuta nukuu hii.

Mara nyingi nukuu hii huwa inatumika na waganga wa jadi kuhalalisha tiba zao kuwa Mungu amempa wanadamu uwezo wa kujitatulia matatizo yake mwenyewe kabla ya yeye mwenyewe kuingilia kati, kwa hiyo kwenda kwa waganga ni moja tu ya harakati za mwanadamu kutumia privilege hio ya kujisaidia kabla Mungu hajaanza kutoa msaada wake.

Sasa ni ni asili ya haya maneno, ni mafundisho ya kipagani??
Ni mafundisho ya kimungu ambayo yamenyumbulishwa kutoka kwenye maana kuu ya mafundisho ya kimungu ila yakapewa maana nyingine??

Au yalitolewa kwenye diary ya wahenga??
 
Ni msemo uliotumiwa Sana na wagiriki wa zamanu, hats hivyo ulipata umaarufu Sana ulipoanza kutumiwa na viongozi maarufu Kama kina Franklin
Haupo kwenye biblia, na wala hakuna popote biblia imewah kutamka hivyo, hats hivyo ukisoma Zaburi inaonya Sana juu ya uvivu......hadi pengine pametolewa ahadi kabisa kuwa, Kwa wamchao bwana, Jasho la mikono yako utaila.
 
Haya mambo ni ya kujifariji tu,binadamu hana ujanja wowote kama si msaada wa Mungu basi ni giza (shetani),lakini sisi tumeumbwa kwa mfano wa Mungu kwanini ujidai una swaga za kujimudu wakati yeye aliyetuumba anao uwezo wa kutuhudumia kwa vyote........
KUMBUKUMBU YA TORATI 28 :
1 Itakuwa utakaposikia sauti ya Bwana, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo Bwana, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;

2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya Bwana, Mungu wako.

3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.

4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, maongeo ya ng'ombe wako, na wadogo wa kondoo zako.

5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.

6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.

7 Bwana atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.

8 Bwana ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.

9 Bwana atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya Bwana, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.

10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako.

11 Bwana atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi Bwana aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.

12 Atakufunulia Bwana hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.

13 Bwana atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya Bwana, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;

14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lo lote, kwenda mkono wa kuume wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.

15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya Bwana, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
 
Back
Top Bottom