Jamaa yuko kwenye harakati kitambo kwenye hii game. AY ndo alianza kuwafumbua macho wasanii kuhusu umuhimu wa kufanya collabo na wasanii wa nje ya nchi.Pia ndo alikuwa msanii wa kwanza bongo kuwa siriaz kuinvest katika video (ki-international zaid) hata Diamond amewahi kulisema hilo kwenye intavyuu zake/kwenye social networks kwamba jamaa ndo kamuinspire.Sasa nashindwa kuelewa why anashindwa kuwa succesful kivile japo anajituma sana, yaani naona kama ka-stack palepale, nilitamani naye niwe namsikia kwenye mambo makubwa makubwa kama 'bwa mdogo' Diamond ili walau tuwe na wawakilishi wengi nje. Mi nazan kama vile watanzania hatumpi sapoti ya kutosha kuanzia media hadi mashabiki, maana eg. huu wimbo mpya alioutoa ft Sean Kingston ni mzuri but sioni ukizungumziwa kihivo. So wadau mnahisi AY anafeli wapi?
Jamaa dawa zake zinashia studio labda, amuulize Platnum anatoa wapi dawa zake.
Sijui tu inakuaje ila mimi kama mimi sijawahi kupenda wimbo wake hata mmoja
hata party zone? aliomshirikisha marco
Nani kakwambia AY ka stack? umetumia vigezo vipi labda ku conclude kua Diamond ana mafanikio makubwa kuliko AY?
Au coz hajatembea na msululu wa wasanii wa bongo muvi ndo unasema hana mafanikio ?
AY ni msanii mwenye mafanikio makubwa kuliko yoyote ukitoa jide ila hapendi kujisifia ni mkimya wala hapendi skendo.
Tatizo lenu mtu anayejionyesha ndio mnajua ana mafanikio .Mimi namfahanu sana AY ana mafanikio makubwa sana na show nyingi anapiga nje mfano show anazopiga Kenya na Uganda ata zinazidi Tz
Uwa apendi kujifagilia na kujionyesha kama wengine ni mkimya pia mfanyabiashara anewekeza Tz ata kenya pia
Nani kakwambia AY ka stack? umetumia vigezo vipi labda ku conclude kua Diamond ana mafanikio makubwa kuliko AY?
Au coz hajatembea na msululu wa wasanii wa bongo muvi ndo unasema hana mafanikio ?