Exclusive: Mastaa wenye nguvu zaidi Afrika Mashariki - 2015

Kidingi

JF-Expert Member
Aug 11, 2012
1,872
1,832
Kiwanda cha burudani katika eneo la Afrika Mashariki kimeendelea kuchangamka zaidi kadri miaka inavyokwenda. Kwa sasa hakuna ubishi kuwa Afrika Mashariki inatoa upinzani wa kueleweka kwa nchi za Afrika Magharibi na Kusini ambazo kwa miaka mingi zimeendelea kuwa kitovu cha burudani barani Afrika.

Hii ni orodha ya Bongo5, ya mastaa 15 walio na nguvu zaidi mwaka 2015, kutoka nchini za Afrika Mashariki. Baadhi ya mastaa hawa sio mastaa tu wa Afrika Mashariki ama barani Afrika pekee, bali kwa sasa wanajulikana dunia nzima.

1. Lupita Nyong'o – Kenya
Lupita Nyong'o ni jina maarufu mno duniani kwa sasa. Umaarufu wake kwa Afrika Mashariki ulianzia kwenye tamthilia ya mwaka 2009, Shuga. Umaarufu wake duniani, ulitokana na kuigiza filamu iliyoshinda tuzo za Oscar, '12 Years A Slave.' Kwenye filamu hiyo aliigiza kama Patsey, mtumwa wa kike aliyejikuta akipata shida kubwa kwa kazi ngumu za mashambani.

Uhusika wake kwenye filamu hiyo ulimfanya mwaka jana ashinde kipengele cha muigizaji msaidizi wa kike bora kwenye tuzo za Oscar. Ushindi huo ulimfanya kuwa muigizaji wa kwanza kutoka Afrika kuwahi kushinda tuzo hizo za thamani. Pia aliigiza kama mhudumu wa ndege kwenye filamu ya action ya mwaka jana, Non-Stop akiwa na Liam Neeson na Julianne Moore. Mwaka huu ameigiza filamu iitwayo Queen of Katwe na Star Wars Episode VII: The Force Awakens.

Umaarufu wake ulimpa deals zaidi ikiwa ni pamoja na kuwa kisura wa kampeni ya Miu Miu akiwa na walimbwende wengine, Elizabeth Olsen, Elle Fanning na Bella Heathcote. Alionekana kwenye majarida makubwa ya fashion duniani yakiwemo Dazed & Confused huku akiwa mwanamke wa pili wa Afrika na wa nane mweusi, kukava jarida la Vogue. April mwaka jana, jarida la People lilimtaja Lupita kama mwanamke mrembo zaidi duniani katika issue yake ya '50 Most Beautiful.' 2015, Nyong'o alikava jarida la Lucky, Harper's Baazar's (UK) na MujerHoy la Hispania. Wiki hii Lupita amerejea nchini Kenya ambako alitangazwa pia kuwa balozi wa taasisi ya WildAid inayojihusisha na kampeni dhidi ya ujangili hususan wa tembo.

2. Diamond Platnumz – Tanzania
Diamond amekuwa si jina maarufu Afrika Mashariki peke yake na sasa miongoni mwa wasanii wakubwa kabisa barani Afrika. Mwaka huu peke yake ametengeneza nyimbo kubwa na collabo na wasanii maarufu Afrika zilizoshika charts kwenye vituo vya redio na runinga vikubwa.

March 27 aliachia video ya wimbo wake wa Mduara, ‘Nasema Nawe' aliomshirikisha Khadija Kopa ambao haukuishia kufanya vyema Afrika Mashariki peke yake, bali Afrika nzima.

Hadi sasa video yake imeangaliwa kwenye mtandao wa Youtube kwa zaidi ya mara milioni 2.7. Collabo yake kubwa kwa sasa ni ‘Nana' aliyomshirikisha Flavour ambayo licha ya kushika chart za redio na TV Afrika ikiwa ni pamoja na kuwa namba moja kwenye kituo cha Trace TV, video ya wimbo huo ni miongoni mwa zile zinazoangaliwa kwa kasi zaidi kwenye Youtube barani Afrika, ikiwa na views zaidi ya milioni 2.1 tangu iwekwe May 29.

Bila kusahau mwaka jana alishirikishwa kwenye nyimbo zilizohit za wasanii wa Nigeria, likiwemo kundi la Bracket na Waje. Hivi karibuni tu video mbili za nyimbo alizoshirikishwa na wasanii wakubwa wa Nigeria zimetoka – Nakupenda aliyoshirikishwa na Iyanya na Love Boat aliyoshirikishwa KCEE.

Pia aliingia studio kurekodi wimbo aliorekodi na msanii wa Afrika Kusini, Donald. June 13 alishinda tuzo mbili kwenye KTMA 2015.

Mwaka huu ametajwa kuwania vipengele vitatu kwenye tuzo za MTV MAMA na ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza July 18 kwenye utoaji wa tuzo hizo, Durban, SA. January mwaka huu staa huyo alikuwa mmoja wa wasanii waliotumbuiza kwenye tuzo za Glo CAF jijini Lagos, Nigeria.

3. Wema Sepetu – Tanzania
Umaarufu wa Wema Sepetu na kuendelea kutengeneza vichwa vya habari Afrika Mashariki, unaendelea kuwepo kutokana na uhusiano wake uliokufa na Diamond miongoni mwa mambo mengine. Wema bado ameendelea kuwa staa wa kike mwenye mashabiki na ushawishi mkubwa nchini Tanzania.

Mwaka huu alishinda tuzo ya muigizaji wa filamu wa kike anayependwa zaidi kwenye Tuzo za Watu. Alisafiri hadi nchini Ghana kwenye kutengeneza filamu na muigizaji wa maarufu wa huko, Van Vicker, ambayo inatarajiwa kutoka mwishoni mwa mwaka huu. Ameendelea kutengenezwa vichwa vya habari kutokana na kutangaza nia ya kuwania nafasi ya ubunge wa viti maalum kupitia CCM, mkoani Singida.

Kama mambo yakimwendea vyema, huenda jina lake mwaka huu likabadilika na kuwa Mheshimiwa Wema Sepetu.

4. Zari the Bosslady – Uganda
Kabla ya kukutana na Diamond, Zari The Bosslady alikuwa maarufu nchini Uganda. Alijulikana kwa urembo wake na utajiri mkubwa aliokuwa nao kupitia aliyekuwa mumewe, Ivan. Alifahamika kama mwanamke anayemiliki magari ya kifahari, mijengo na biashara kubwa.

Umaarufu wake umekuja kukua zaidi baada ya kukutana na Diamond Platnumz na kuanzisha uhusiano ambao sasa umewafanya kuwa couple yenye nguvu zaidi Afrika Mashariki. Kwa sasa wawili hao wanatarajia kupata mtoto wao wa kwanza. Mtoto huyo bila shaka ana nafasi kubwa ya kuwa mtoto maarufu zaidi Afrika Mashariki.

5. Vanessa Mdee – Tanzania
Vanessa anafahamika kama msanii wa kike kutoka Afrika Mashariki anayejituma zaidi kuliko wote. Mwaka huu ameshiriki kwenye kampeni nyingi za kimataifa. Alishiriki kwenye kampeni ya One Organisation ambapo aliungana na wasanii wengine wa Afrika kuimba wimbo uitwao Strong Girl.

Pia aliungana na mastaa wakiwemo Lupita Nyong'o, Hasheem Thabeet, Jacqueline Ntuyabaliwe na Alikiba kama mabalozi wa WildAid na kampeni dhidi ya mauaji ya tembo. Mwaka huu ametajwa kuwania kipengele cha msanii bora wa kike kwenye tuzo za MTV MAMA. Wimbo wake ‘Nobody But Me' aliomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O, ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri Afrika kwa sasa.

Mwezi ujao ataonekana kwenye jarida maarufu la Marekani la Essence kwenye toleo lake la dunia (global issue). Ni balozi wa Samsung na Crown Paints.

6. Millen Magese – Tanzania
Happiness Millen Magese ladivamillen amejipatia umaarufu mkubwa mwaka huu kutokana na kuwa balozi kwenye kampeni aliyoanzisha mwenyewe ya tatizo la Endometriosis ambalo limepelelekea afanyiwe upasuaji kwa takriban mara 13 na kumfanya awe mgumba.

Millen ameanzisha kampeni ya kukuza uelewa wa ugonjwa huo na kuwataka wanawake wenye tatizo hilo kutooana aibu kujitokeza kuomba msaada lakini pia kuwataka wanaume wenye watu wao wa karibu walio na tatizo hilo kuwavumilia. K

utokana na jitihada hizo pamoja na kuwa mstari wa mbele katika kusaidia watu wasiojiweza, June mwaka huu alitunukiwa tuzo ya Global Good ya BET Awards.

7. Eddy Kenzo – Uganda
Jina la Edrisa Musuuza maarufu kama Eddy Kenzo halikuwa maarufu sana kwa Tanzania na Kenya kabla ya June mwaka huu kushinda tuzo ya BET ((Best Viewers' Choice International Act). Anahamika zaidi kwa hit yake Sitya Loss. Wimbo huu ulifahamika duniani kupitia video ya Youtube ya vijana wa mtaani waliokuwa wakicheza wimbo huu.

Video hii ilikuwa maarufu kiasi cha kuwepo na ombi (petition) ili vijana hao waweze kuhojiwa kwenye The Ellen DeGeneres Show. Hadi sasa video hiyo ina views zaidi ya milioni 11.

Kenzo ameshatumbuiza kwenye majiji 15 ya Marekani. Ametembelea na kutumbuiza kwenye majiji kibao duniani. Alitumbuiza kwenye fainali za mataifa ya Afrika.

8. Sauti Sol – Kenya
Bien-Aimé Baraza, Willis Chimano, Delvin Mudigi na mpiga gitaa wao Polycarp Otieno ndio wanaunda kundi la Sauti Sol.

Mwaka huu walitajwa kuwania tuzo za BET japo hawakufanikiwa kushinda. June 13, walichukua tuzo ya wimbo bora wa Afrika Mashariki kwenye KTMA 2015 na wimbo wao uliokuwa anthem ya Afrika Mashariki, ‘Sura Yako.'

Mwaka huu wanawania kipengele cha kundi bora kwenye tuzo za MTV MAMA. Kwa sasa wapo kwenye ziara ndefu nchini Marekani.

9. Alikiba – Tanzania
King Kiba kama anavyojiita, aliufungua mwaka 2015 kwa kishindo na hakuna anayeweza kubisha kuwa jamaa huyu ana ushawishi mkubwa nchini Tanzania. Milango yake ya umaarufu nje ya Tanzania imefunguka tena mwaka huu baada ya kuwa kimya kwa takriban miaka mitatu.

Video ya wimbo wake ‘Chekecha Cheketua' ilichezwa kwa mara ya kwanza kwenye kituo cha Trace Urban na kuendelea kupata rotation ya mara tano kwa siku. Mwaka huu Alikiba alishinda tuzo ya muimbaji wa kiume anayependwa kwenye Tuzo za Watu na kushinda tuzo takriban sita kwenye KTMA 2015. M

waka huu pia ameungana na wasanii wengine wa Afrika kwenye msimu wa tatu wa kipindi cha Coke Studio Afrika huku akitengeneza timu na msanii wa Kenya, Victoria Kimani. Pia aliungana na Lupita Nyong'o, Vanessa Mdee na K-Lynn kama balozi wa WildAid katika kampeni dhidi ya mauaji ya tembo.

10. Idris Sultan – Tanzania
Ushindi wa $300,000 wa shindano la Big Brother Africa mwaka jana, umemfanya Idris kuwa miongoni mwa mastaa wakubwa Afrika kwa sasa. Japokuwa hajaanza kufanya miradi mingi, ukubwa wa shindano hilo umeendelea kuliweka jina lake kwenye headlines. Lakini pia uhusiano wake na mshiriki mwenzie wa shindano hilo, Samantha umewafanya wawili hao kuokota headlines za hapa na pale kwenye vyombo vya habari vya Afrika.

Idris anafahamika kwa vituko vyake na huenda akawa na nafasi kubwa ya kuingiza fedha nyingi kupitia kipaji hicho miongoni mwa vingi alivyo navyo.

11. Jaguar – Kenya
Jaguar alitengeneza headlines mwaka huu kwa mambo mengi ikiwemo kurushiana maneno na msanii wa Nigeria, Iyanya aliyemshirikisha kwenye remix ya wimbo wake ‘One Centimeter. Ugomvi ulitokana na shutuma ya Jaguar dhidi ya msanii huyo kuwa alikuwa akimletea mapozi wakati wa mipango ya kufanya video ya wimbo huo. Iyanya alijibu kwa kumwelezea msanii huyo kama ‘asiye serious' na muziki.

Pamoja na kufanya muziki, Jaguar ameendelea kuandikwa zaidi kutokana na juhudi zake za kuwainua watu wanaoishi kwenye mazingira magumu na kazi zake kwenye taasisi za serikali ikiwemo NACADA. Hivi karibuni alijitolea kumsomesha kijana mwenye umri wa miaka 16 aliyeruka uzio wa ikulu ya Kenya ili kwenda kukutana na Rais Uhuru Kenyatta ili amsaidie kumlipia hela ya studio kurekodi muziki.

"Promised to look for him after jumping statehouse and i have found him . . ..he is 16yrs and best i can do for now is take him to school… he dropped form 1 coz of lack of fees……he has a kikuyu song titled Jubireeeee bt muziki baadaye," aliandika Jaguar kwenye Instagram.

12. Jose Chameleone – Uganda
Chameleone ni miongoni mwa wasanii wa Afrika Mashariki wanaoingiza fedha nyingi zaidi kupitia show nyingi za ndani na za kimataifa. Mwaka huu ameingia kwenye tuzo za MTV MAMA kwenye kipengele cha Evolution Award. Pia naye ameungana na wasanii wengine wa Afrika kwenye msimu wa tatu wa Coke Studio Africa.

Video ya wimbo wake ‘Wale Wale' ilifanya vizuri barani Afrika ikiwa ni pamoja na kushika chart za muziki wa bara hilo kwenye kituo cha runinga cha Trace Urban.

13. Victoria Kimani – Kenya
Victoria Kimani aliungana na Vanessa Mdee na wasanii wengine kwenye kampeni ya One kurekodi wimbo ‘Strong Girl.' First Lady huyu wa Chocolate City ameendelea kufanya vizuri kwenye muziki wa Afrika ikiwa ni pamoja na mwishoni mwa mwaka uliopita kutoa hit single, ‘Show.'

Nyimbo zake zinapata rotation kubwa kwenye redio za Afrika pengine kuliko msanii yeyote wa Kenya. Mrembo huyo wiki hii ameshinda tuzo ya ‘Most downloaded Female In Africa' kwenye Mdundo Awards 2015 aliyokabidhiwa na Alikiba. Kimani na Alikiba wanashiriki pamoja kwenye Coke Studio Africa.

14. AY – Tanzania
Mwishoni mwa mwaka uliopita, (Dec 9) na mwanzoni mwa mwaka huu (Feb), AY aliachia video za collabo za kimataifa. Ya kwanza ni wimbo wake ‘Love Me' aliomshirikisha Sean Kingstone na Ms Trinity na ‘It's Going Down' aliyowashirikisha Ms Trinity na Lamyia Good. Video hizo zilishika charts kadhaa kwenye runinga za Afrika.

Alikuja kuachia hit single yake ‘Zigo' ambayo hadi sasa imeendelea kuwa miongoni ma ngoma zinazochezwa zaidi redioni nchini Tanzania. Beat ya wimbo huo inatarajiwa kutumiwa na wasanii wengine wengi kutengeneza version zao. Wasanii walioonesha interest ya kuitumia ni pamoja na Jose Chameleone na Wizkid wa Nigeria.

AY ameendelea kuwa msanii anayeheshimika zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki ikiwa ni pamoja na mwaka huu kushiriki kama mentor kwenye shindano la Maisha Superstar.

Pamoja na muziki, AY ni mjasiriamali aliyefanikiwa. Ni mwanzilishi mwenza wa kipindi cha TV ‘Mkasi' kilichoshinda kwa miaka miwili mfululizo tuzo ya kipindi cha runinga kinachopendwa katika Tuzo za Watu 2015.

Pia ni mwanzilishi mwenza wa kipindi kingine cha TV, Siaza za Siasa.

15. Bebe Cool Mwaka huu Bebe Cool anawania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha video bora ya mwaka. Wimbo wake ‘Love You Everyday' umehit sana katika kipindi cha mwaka 2014/15 na video yake ndio inayowania tuzo hiyo.

Bebe Cool ameendelea kuwa miongoni mwa wasanii wanaoheshimika zaidi nchini Uganda.


Chanzo: Bongo5
 
Hiyo na idris kuwa namba 10 juu ya Chameleone naikataa" Chameleone alibidi awepo kwenye top 10
 
Hiyo na idris kuwa namba 10 juu ya Chameleone naikataa" Chameleone alibidi awepo kwenye top 10

Teh Teh hata ya Wema na Vannesa kuwa kweye hii list bado sijaelewa kabisa kinacho pimwa kama ni mafanikio au idadi ya mashabiki?
 
Watoe
1. Ali Kiba
2. Vanessa Mdee
3. Eddy Kenzo
4. Jaguar
5. Lupita Nyongo
6. Iddriss Sultan

Hao hawana nguvu yeyote.
List yangu:
1. Diamond Platnumz
2. Wema Sepetu
3. Zari Zarina
4. Jose Chamilione
5. AY
 
Teh Teh hata ya Wema na Vannesa kuwa kweye hii list bado sijaelewa kabisa kinacho pimwa kama ni mafanikio au idadi ya mashabiki?

Naona wamebase kwenye followers zaid hawajui kua unaweza kuta Wema 85% ya followers wake wanatoka Tanzania sasa how come useme anaushawishi mkubwa EA. Wameangalia followers tu kwa kiasi kikubwa naona.
 
Naona wamebase kwenye followers zaid hawajui kua unaweza kuta Wema 85% ya followers wake wanatoka Tanzania sasa how come useme anaushawishi mkubwa EA. Wameangalia followers tu kwa kiasi kikubwa naona.

Nilitegemea watwambie mafanikio ya mtu tena kwa mali na vitu anavyo miliki vilivyo tokana na umaarufu na kazi yake!
 
Hata mfalme wa vichaa yupo nakata rufaa haiwezekani kabisa
 
Nilitegemea watwambie mafanikio ya mtu tena kwa mali na vitu anavyo miliki vilivyo tokana na umaarufu na kazi yake!

Kweli mkuu hii list haina maana. Kuna vitu vingi sana ilibidi waangalie sio Instagram tu" unaweza ukawa na ushawishi mtandaoni lkn kwenye jamii zero
 
Hapo vikubwa walivyoangalia nadhani ni

+ Mafanikio yako katika carrier uliyopo (ambayo ni kubwa zaidi)

+ Thamani (value) yako kama celebrity je ni kivipi wa gharama na ni kwa kiasi kipi watu wapo tayari hata kulipa pesa kubwa kukuona tu!!

+ Nguvu uliyonayo kwenye social media na si followers pekee coz kuna watu kama instagram jokate, anazaidi ya followers 520k, shilole zaidi ya 400k, jide zaidi ya 200k twitter, but hawamo..

Hii nguvu kwenye social media ina range kutokea hao followers, (facebook, insta, twitter sababu inaonyesha ni jinsi gani watu wanakufuatilia na kutaka kujua mengi juu yako), Ni kivipi unatokea kwenye blogs mbalimbali mitandaoni, ni kivipi unatokea kwenye magazeti tofauti.... Na sio kuandikwa tu, je habari zako zinasomwa kwa kiasi gani?

Hivi vyote nadhani vinajenga hiyo list..
 
Watoe
1. Ali Kiba
2. Vanessa Mdee
3. Eddy Kenzo
4. Jaguar
5. Lupita Nyongo
6. Iddriss Sultan

Hao hawana nguvu yeyote.
List yangu:
1. Diamond Platnumz
2. Wema Sepetu
3. Zari Zarina
4. Jose Chamilione
5. AY

Kwa vigezo vipi?
 
Kwenye Muziki na Movie Tanzania tuko juu Afrika ya Kati na Mashariki
 
Kanumba angekuwa hai tungekuwa hatukamatiki kwenye entertainment, huku Kanumba kule Diamond

Yule jamaa alikufa mapema sana, alikiwa kavuka sana kwenye movie na movie zake watu walizipenda sana...
Yaani sasa hakuna movie ya maana kabisa Lulu kwanini ulimuua kijana wa watu mapema vile?
 
Watoe
1. Ali Kiba
2. Vanessa Mdee
3. Eddy Kenzo
4. Jaguar
5. Lupita Nyongo
6. Iddriss Sultan

Hao hawana nguvu yeyote.
List yangu:
1. Diamond Platnumz
2. Wema Sepetu
3. Zari Zarina
4. Jose Chamilione
5. AY

kwel hyo n list yako maana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom