G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Jana kama mlimsikia rais wa Tanzania mheshimiwa John Magufuli akihutubia baraza la eid aliahidi kurejesha mali za waislamu zilizotaifishwa. Mimi kama mdau ningependa kujua ni mali zipi hasa zilitaifishwa kutoka kwa waislamu, kina nani walihusika na kwa nini?
Pia, je huo ni mwanzo wa kurejeshwa mali zote zilizotaifishwa hasa na CCM baada ya mfumo wa vyama vingi? Mali ambazo watanzania walivuja jasho kuzijenga enzi za chama kimoja mfano viwanja mbalimbali vya michezo nchini?
Angalizo: Hatua hii ya mheshimiwa rais inaweza isiishie hapo. Kama MWANANCHI huru nasikitika sana kusema kuwa huenda mheshimiwa rais anaweza kuwa ameongea kitu sahihi ila mahala na wakati siyo sahihi (Pasco) na hili huenda likaibua hisia kali na mpasuko wa aina yake. Tulitazame kwa jicho la mbali na kama wengine nao watadai mali zao mfano wakristu na wahindi basi taifa limepasuka.
Pia zile harakati za sheikh Ponda na marehemu Ilunga huenda zikaibuka upya.
Nimetumia neno "kutaifisha" badala ya neno "kupora/kulangua" ili kulinda hadhi za waliohusika na kama nilivyoandika mwanzo huenda likaendelezwa na kada na dini nyingine!
cc Ritz, FaizaFoxy, [USER=12431]Mohamed Said, THE BIG SHOW, na wadau wengine wanaolielewa jambo hili kwa kina maana sisi wa juzi tunasikia tu kuwa kuna mali zilitaifishwa, kila kukicha tunasikia tu[/USER]